top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Kupumua kwa kasi ni nini?

Kupumua kwa Kasi

Ni hali ambapo mtu anapumua kwa idadi kubwa ya pumzi kwa dakika kuliko kiwango kinachotarajiwa kwa umri na hali yake. Kwa mtu mzima aliyepumzika, kiwango cha kawaida cha kupumua huwa takribani pumzi 12–20 kwa dakika. Kupumua zaidi ya 20 kwa dakika kwa mtu mzima aliyepumzika kunaweza kuitwa kupumua kwa kasi, ingawa maana yake hutegemea hali ya mgonjwa.

Kushindwa kwa ogani

Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi

Kupungua kwa uwezo wa kiungo kufanya kazi ni hali ambayo kiungo cha mwili kinapungua uwezo wake wa kutekeleza kazi zake za kawaida kutokana na ugonjwa, jeraha au hali nyingine ya kiafya. Hali hii inaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na inaweza kuathiri kiungo kimoja au viungo vingi kwa wakati mmoja.

Kuvia damu kwenye perikadiamu ni nini?

Kuvia damu kwenye perikadiamu

Ikifahamika pia kama Mvio wa damu kwenye perikadiamu ni hali ambapo damu hukusanyika ndani ya mfuko unaozunguka moyo (perikadiamu). Hali hii hutokea damu inapovuja kutoka kwenye moyo, mishipa ya damu inayozunguka moyo au mishipa mingine ya kifua na kuingia kwenye nafasi ya perikadiamu.

Kuvimba vifundo vya miguu ni nini?

Kuvimba vifundo vya miguu

Ni hali ambapo sehemu ya chini ya miguu, hasa eneo linalozunguka vifundo vya miguu, huongezeka ukubwa kutokana na mkusanyiko wa maji kwenye tishu. Hali hii huitwa edema na inaweza kutokea kwenye mguu mmoja au miguu yote miwili.

Kuvujiwa kwa valvu za moyo ni nini?

Kuvujiwa kwa valvu za moyo

Ni hali ambapo valvu ya moyo haifungi vizuri, hivyo sehemu ya damu hurudi nyuma badala ya kuendelea katika mwelekeo unaotakiwa. Hali hii pia huitwa upungufu wa valvu au regurgitation ya valvu.

bottom of page