top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Uoto kwenye moyo ni nini?

Uoto kwenye moyo

Ni mkusanyiko usio wa kawaida unaotengenezwa juu ya utando wa ndani wa moyo, hasa kwenye valvu za moyo. Mara nyingi huwa na mchanganyiko wa mabonge ya damu, fibrini, chembe za kinga na vijidudu kama bakteria au fangasi.

Upungufu wa protini mwilini ni nini?

Upungufu wa protini mwilini

Ni hali ambapo kiwango cha protini, hasa alibumini, huwa chini kuliko kiwango kinachotarajiwa katika damu. Alibumini husaidia kushikilia majimaji ndani ya mishipa ya damu, hivyo kiwango chake kinapopungua, majimaji yanaweza kutoka kwenye mishipa na kujikusanya kwenye tishu na kusababisha idima.

Upungufu wa pumzi ni nini?

Upungufu wa pumzi

Ni hali ya mtu kuhisi kuwa anapata hewa kidogo, anashindwa kuvuta pumzi vizuri, au anahitaji kutumia nguvu zaidi ili kupumua. Mtu anaweza kuhisi kama kifua kinabanwa, hawezi kuvuta pumzi ya kutosha au anahitaji kupumua kwa haraka kuliko kawaida. Kwa lugha nyingine ya kitabibu, hali hii huitwa disipnia.

Urethraitis

Urethraitis ni nini?

Urgency

Urgency ni nini?

bottom of page