top of page

Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic

 

 

Kukohoa

Kukohoa ni njia ya mwili kuondoa vikereketa(vimelea wa maradhi au uchafu) kwenye koo ama njia ya hewa(mfumo wa hewa)

Vikereketa huamsha au kushitua mishipa ya fahamu, taarifa hutumwa katika ubongo na kisha hurudishwa kwenye misuli ya koo na mfumo wa hewa na kusababisha kukohoa ili kuondoa vikereketa hivyo kwenye mfumo wa hewa na kooni.

 

Kwa maana nyingine kikohozi ni afya, kwa sababu huondoa uchafu katika njia za hewa. Kukohoa kunakodumu zaidi ya wiki kadhaa au kikohozi kinacho sababisha kutoa makohozi yenye damu huweza kumaanisha kuna shida katika mfumo wa hewa na kuna hitaji uchunguzi na matibabu. Kikohozi huwa hakihitaji matibabu ya dharura sana.

 

Kushikwa na kikohozi huweza kuwa na msukumo mkubwa, inajulikana hewa ya kasi inayoweza kutoka katika kifua wakati wa kukohoa kwa nguvu huweza kutembe umbali wa mile 500 kwa saa na hili huweza kuleta madhara ya kichwa kuuma, kutopata usingizi, kujikojolea, na mbavu kuvunjika.

 

Nini husababisha kukohoa


Sababu za mara kwa mara;

 • Aleji/mzio na vumbi au kemikali fulani

 • Pumu 

 • Maambukizi kwenye mfumo wa mapafu

 • Madhara ya kubeuka


Sababu zingine;

 

 • Homa ya baridi

 • Mafua

 • Kuvuta hewa yenye vikereketa

 • Pneumoni/nimonia

 • Donda koo

 • Kifua kikuu

 • COPD

 • Saratani ya mapafu

 • Moyo kufeli

 • Maambukizi kwenye mfumo wa sauti

 • Magonjwa ya mfumo wa fahamu wa koo

 • Madawa ya kushusha presha au shinikizo la damu la juu jamii ya ACE

 • Maambukizi ya  kirusi cha respiratory syncytial  kwa watoto wadogo

 • Homa ya hay

 

Imepitiwa 3/3/2016

imechapishwa 3/3/2015

bottom of page