top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY Clinic

​

Kontakti demataitizi

 

Ni tatizo la ngozi ambalo husababisha ngozi iwe nyekundu(kwa watu weupe), iwashe na kupata vipele vinavyosababishwa na aleji na kitu Fulani. Tatizo hili ni miongoni mwa aina ya pumu ya ngozi lakini yenyewe husababishwa na mgusano wa ngozi na kitu Fulani chenye aleji na ngozi yako.

 

Je tiba ipo?

 

Tatizo huisha mara moja pale kisababishi kinapoondolewa au kuepukwa, matibabu yapo ya kupunguza dalili tu na si kuondoa kabisa tatizo.

 

Dalili za kontakti demataitizi ni zipi?

​

Kontakti demataitizi huwa na dalilizifuatazo kwenye ngozi

​

  • Miwasho

  • Kutokea kwa malenge

  • Kutokea kwa vipele vigumu na vidogo na kupasuka kwa ngozi

  • Watu wenye ngozi nyeupe ngozi hubadilika na kuwa nyekundu watu weusi huwa na rangi ya brauni mkolezo, zambarau au kijivu

  • Kwa kawaida mwitikio wa ngozi(aleji)hutokea ndani ya masaa machache au siku kadhaa baada ya kukutana na kisababishi

  • Dalili zinaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini hutokea sana mikononi na usoni

  • Kuvimba, kuungua au kuumia ukishika eneo lililopata aleji

 

Visababishi

 

Baadhi ya vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la kontakti demataitizi ni;

​

  • Vichokoza ngozi mfano wake ni

  • Vimiminika vya kusafishia/kuoshea au kufulia

  • Spiriti ya kupaka

  • Mafuta ya kufanyia blichi

  • Sabuni za kukausha ngozi na zenye pafyumu au kemikali

  • Shampuu

  • Uchafu kwenye hewa kama vile vumbi la mavi ya ng’ombe na manyoya

  • Mimea kama muembe na poleni za maua

  • Mbolea na dawa za kuulia wadudu

  • Kuvaa vidani vya madini ya niko

  • Matumizi ya krimu/dawa za kunywa zenye antibayotiki(haswa penicillin)

  • Matumizi ya vimiminika/nguo/vitunzaji vyenye kemikali ya formaldehyde

  • Pafyumu, deodorant, dai za nywele na baadhi ya vipodozi

  • Mafuta ya kupaka kwa ajili ya kujikinga na mwanga wa jua

  • N.k

 

Watoto huweza kupata dalili kutoka kwenye vitu hivyohivyo na pia kwenye chupi, pampasi, mafuta ya kuzuia kupigwa mwanga wa jua, dai na vinginevyo

 

Vihatarishi

 

  • Kuwa mfanyakazi wa afya

  • Kufanya kazi za kutumia vyuma

  • Wajenzi wa nyumba

  • Kuvaa nywele bandia na kutumia vipodozi

  • Kufanya kazi za kutengeneza magari pamoja na kushika oili

  • Kuogelea(kwa sababu ya kuvaa maski na miwani)

  • Kusafisha au kupiga deki kwa vimiminika au sabuni

  • Kufanya kazi za ukulima (kutokana na matumizi ya mbolea na pembejeo mbalimbali za kilimo)

  • Kupika au kufanya kazi zinazohusika na chakula

 

Madhara

 

Kama mtu akijikwangua mara kwa mara kweye eneo lililoathirika, huweza kupata maambukizina eneo hilo. Daktari akiwa anakutibu atakupa na dawa za kutibu maambukizi kama yapo

 

Namna ya kujikinga

 

Njia pekee ya kuondokana na tatizo la kontakti demataitizi ni kuepuka visababishi vinavyofahamika (vilivyofahamika kwako). Unaweza kujikinga kwa;

  • Kujizuia vichokoza ngozi vilivyotajwa hapojuu

  • Kuondoka au kuacha mara moja kitu kinachochokoza ngozi yako au kukusababishia mzio, oga kama kimekugusa ngozi

  • Tumia sabuni isiyo na pafyumu au kemikali nyingi na maji ya uvuguvugu kujisafisha mwili wote kama umepata aleji na kitu Fulani mara moja.

  • Hakikisha pia unafua nguo au kusafisha kitu chochote kile kilichogusana na kitu ambacho kinakusababishaia aleji kwenye ngozi yako.

  • Oga/jisafishe mara unapopata jasho,jasho husababisha dalili ziwe kali zaidi

  • Kuwa na tabia za kusoma kila unachotumia kwenye mwili wako kuwakina kemikali gani ili ujikinge za zile ambazo zinaleta aleji kwenye ngozi yako

  • Vaa nguo za kukukinga na uchafu kama vile miwani na glavu(endapo una aleji na glavu, tanguliza kwanza pamba) wakati unafanya usafi kwa kutumia kemikali au kufanya kazi kwenye mazingira yenye vichokoza ngozi

  • Kama unavaa mkanda au vidani vyenye madini yanayokuletea aleji kwenye ngozi hakikisha upande unaogusa ngozi ni chuma ili usipate mzio

  • Tumia krimu au mafuta yakukinga ngozi yako dhidi yavichokoza ngozi

  • Tumia losheni ya kuipa ngozi unyevunyevu (kulainisha ngozi) ili kuifanya ngozi isikauke na kupatamzio/aleji kirahisi. Pia unaweza tumia sabuni ya kuongeza inayoipa ngozi unyevu mbadala wa ile inayokausha ngozi yako.

  • Hakikisha unakuwa makini unapohudumia mifugo

 

Namna ya kutambua tatizo

 

Daktari au mtaalamu wa afya atatambua tatizo lako kwa kukuuliza historia yako na mahusiano ya visababishi na tatizo lako.

​

Unaweza kufanyiwa kipimo cha kuangalia kama una aleji kwenye ngozi pia, kipimo hiki hufahamika kama patch test. Hata hivyo ni vigumu kujua unaaleji na kitu gani licha ya kip[imo kuonesha kuwa una aleji

 

Matibabu

 

Kama kisababishi cha tatizo lako kinaweza kutambuliwa na kuepukwa, tiba yako itakuwa imepatikana

​

Lakini kama hakijatambuliwa utapewa dawa mbalimbali za kupunguza dalili na makali yake

​

Unashauriwa kutumia dawa za kuongeza unyevu kwenye ngozi ambayo utakuwa ukiipaka kwenye ngozi yako ili kuizuia isikauke kila siku

​

Tiba nyingine ni kuzuia visababishi kama vilivyoorodheshwa katika sehemu ya visababishi vya tatizo hili.

 

Unapochagua vilainisha ngozi(mafuta ya kufanya ngozi iwe na nyevu) hakikisha unazingatia vitu vifuatavyo;

​

  • Vilainisha ngozi vya krimu huwa vizuri kwa watu wenye ngozi yenye mafuta kiasi

  • Vilainisha ngozi vya mafuta huwa vizuri kwa watu wenye ngozi isiyo na mafuta

  • Tumia sabuni ya kulainisha ngozi mbadala wa sabuni za kukausha ngozi

  • Endapo kilainisha ngozi ni cha uso tu usitumie maeneo mengine ya mwili, kinyume chake pia ni kweli

  • Hakikisha unapaka vilainisha ngozi kwa wingi na kila unapooga, hakikisha unaoga mara tatu au nne kwa siku

  • Unapopaka vilainisha ngozi usijisungue sana(usitumie nguvu nyingi) ili kuepuka kuamsha ngozi na aleji

  • Unapomaliza kuoga, kausha ngozi kwa kutumia taulo ya pamba bila kutumia nguvu na mara moja paka mafuta yako ya kulainisha ngozi

  • Kama unafanya kazi kwenye mazingira yenye vichokoza ngozi hakikisha unapaka mafuta ya kulainisha ngozi kama kawaida

  • Usitumie mafuta ya mtu mwingine

 

Dawa zingine zinazoweza kutumika ambazo utapewa na Daktari ni;

​

  • Dawa  ya kupaka au kunywa jamii ya corticosteroid

 

Matibabu mengine unayoweza kupata ni

​

  • Tiba ya mwanga

  • Dawa jamii ya tretinoin

 

Tiba mbadala

 

Baadhi ya watu wanaweza kutumia tiba mbadala kama mitishamba ya kupaka inayoondoa mzio kwenye ngozi au kula chakula aina Fulani. Ongea na daktari wako kwanza endapo tiba hiyo inaweza kuingiliana na dawa alizokupa.

 

ULY clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa tiba na ushauri kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya

 

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa ushauri na tiba, bonyeza hapa au tumia namba za simu chini ya tovuti hii.

 

Imeboreshwa mara ya mwisho. 21.06.2020

​

Rejea za mada hii

 

  1. NHS. Contact dermataitiz. https://www.nhs.uk/conditions/contact-dermatitis/diagnosis/. Imechukuliwa 21.06.2020

  2. Goldsmith LA, et al., eds. Allergic contact dermatitis. In: Fitzpatrick's Dermatology in General Medicine. 8th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Companies; 2012. http://www.accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 21.06.2020

  3. Contact dermatitis. Merck Manual Professional Version. https:/www.merckmanuals.com/professional/dermatologic-disorders/dermatitis/contact-dermatitis. Imechukuliwa 21.06.2020

  4. Goldner R, et al. Irritant contact dermatitis in adults. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 21.06.2020

  5. ​Dertamaitiznet. https://dermnetnz.org/topics/allergic-contact-dermatitis/. Imechukuliwa 21.06.2020

kontakti demataitizi-ulyclinic
bottom of page