Imeandikwa na madaktari wa ULY-CLinic
Maambukizi kwenye koromeo-Pharyngitis
Maana na Kisababishi
Maambukizi kwenye koromeo kwa watoto husababishwa kwa asilimia kubwa na virusi kama adenovirus, coronavirus, enterovirus, rhinovirus RSV, EBV, HSV, metapneumovirus pamoja na bakteria kundi A B hemolytic streptococcus. Bakteria wengine pia wanaweza kusababisha maambukizi katika koromeo.
Ukubwa wa tatizo
Maambukizi ya virusi katika mfumo wa juu wa hewa huambukiziwa kwa njia ya kukaa karibu na mtu anayeumwa haswa katika majira ya baridi na kucipua. Maambukizi a streptococcal hayatokei kwa watoto sana kabla ya kufikisha umri wa miaka 2 hadi 3, hutokea sana kipindi wakianza kwenda shule na hupotea kwenye ujana na utu uzima. Maambukizi hutokea majira ya kuchipua na baridi na husambaa kati ya wanafunzi marafiki au ndugu wanaoishi pamoja.