top of page

Kupunguza zutito kwa njia ya kutakasa mwili

​

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

 

Utangulizi

​

Katika miaka ya hivi karibuni kutokana kuongezeka kwa watu wenye nyama uzembe au kitumbo na kutafuta tiba dhidi ya uzito uliopita kiasi na nyama uzembe, kupoteza uzito kwa njia ya kutakasa mwili kumewafanya watu wengi kuweka macho kwenye njia hii kuwa ndo njia nzuri na njia moja maarufu zaidi ya kupunguza  uzito haraka.

​

Makala hii inakuambia namnaya kupunguza uzito kwa njia ya kutakasa na faida na madhara yake

​

Nini maana ya kupunguza uzito kwa njia ya kutakasa mwili?

​

Neno kutakasa kama lilivyo na maana kwamba ni kusafisha, katika kupunguza uzito humaanisha kusafisha mwili dhidi ya sumu mbalimbali zilizo ndani ya mwili. Hakuna maana nzuri ya nini maana ya kutakasa mwili na nini haswa vinapaswa kuwepo wakati wa kutakasa mwili.

​

Kwa ujumla kutakasa mwili huhusisha njia ya kujizuia kula aina fulani ya vyakula au kubadili maisha au kutumia dawa aina fulani za miti shamba(dawa asilia)

​

Njia hizi wengne hutumia ili kuondoa sumumwilini,  na wengine hutumia kama njia ya kupunguza uzito, ikiwa pamoja na kupunguza mafuta sehemu fulani tu ya mwili mfano tumbo n.k

​

Baadhi ya njia huhusisha kutumia dawa asilia au mazoezi, nyingine huhusisha kutumia chakula aina fulani ambacho unakula kila siku.

Kuna utofauti kati ya kutakasa mwili na kutumia dawa za kuondoa sumu mwilini?

Ni ngumu kutofautisha kati ya kutakasa mwili na kuondoa sumu mwilini kwa kwa sababu njia zote hazina utofauti kati ya miongozo na nini haswa kiwepo au kifanyike wakati wa kutakasa au kuondoa sumu mwilini. Hivyo maneno haya siku zote yanatumika yakiwa na maana moja.

Kila aina ya njia ina malengo ya kutoa tiba yam da mfupi yaani chini ya mwezi mmoja au siku 30

​

Chakula cha kuondoa sumu

​

Vyakula vya kuondoa sumu mwilini hufanya kazi kwa kanuni kwamba mwili huhitaji msaada wa kuondoa sumu na kemikali hatari mwilini ambazo huzuia wewe kufikia kiwango cha juu cha afya njema.

Sumu hizi zinatuzunguka katika maisha ya kila siku na hupatikana kutokana na maisha ya binadamu  na shughuli wanazofanya; zikihusisha

  • Uchafuzi wahali ya hewa

  • Madini

  • Kemikali za viwandani

  • Dawa za kuua wadudu kwenye mimea au vyakula

  • Viasha mizio( allegen)

​

Chakula cha kuondoa sumu kinaweza kuhusisha, kukuzuia kula aina fulani ya vyakula na kufunga, dawa za asilia, dawa za kuamsha kuharisha, dawa za kulegeza haja kubwa na kuacha kula vyakula aina fulani. Baadhi ya njia huweza kuondoa sumu kwenye kiungo fulani tu cha mwili mfano figo, ini, kibofu cha mkojo au utumbo

​

Kupungua uzito kunaweza kuwa moja ya malengo ambayo unaweza kuyafikia ili kuondoa uchafu na sumu kama vile

  • Viamsha mizio(allergen)

  • Maumivu ya kichwa na kipanda uso

  • Matatizo ya mmengenyo wa chakula

  • Kuchoka

  • Kichefuchefu

  • Chunusi

  • Harara kwenye ngozi

  • Kurekebisha homoni mwilini

​

Ingawa dawa za kuondoa sumu zimekuwa maarufu sana, hakuna ushahidi kuwa njia hizii zinafanaya kazi kwa ufanisi gani.

 

Kutakasa mwili siku zote kunasisitiza chakula

Baadhi ya milo ya kutakasa mwili hufanya kazi kama dawa za kuondoa sumu mwilini, huhusisha kukataza kula baadhi ya vyakula na kupata viinirishe muhimu.

​

Kwa ujumla hulenga kuondoa vyakula visivyo na umuhimu kiafya na vile vyenye kuamshamizio na mdalala wake kutumia vyakula vyenye afya njema, vyakula asilia na visivyo sindikwa

Kupoteza uzito huwa nilengo mojawapo la kutaka samwili, lakini pia kutakasa mwili hulenga kuondoa Matatizo mengi ya kula mfano kuondoa hamu ya kula sana n.k

​

Vyakula ambavyo vinaondolewa kwenye ili kuutakasa mwili ni

  • Sukari

  • Vyakula vya kusindikwa

  • Pombe

  • Maziwa

  • Soya

  • Ngano

  • Mahindi

  • Vyakula vyenye gluten

​

Mifano ya njia mbalimbali za kutakasa mwili ni kama zilivyoorodheshwa hapo chini;

​

Utakaso wa kuacha baadhi ya vyakula

Siku 30 za kuacha kula vyakula kadhaa vya sukari, maziwa, mazao jamii ya kunde, vyakula vitokanavyo na mbegu na pombe. Kipindi hiki utatumia matunda kwa wingi, mboga za majani na nyama nyeupe.

​

Utakaso wa kutumia juisi

Huduma kwa siku 3 hadi 7, utaacha kula vyakula aina zote, na kubakisha juisi tu na maji. Kuna orodha maalumu ya juisi na mboga za majani unazotakiwa kula kwa kipindi hicho

​

Utakaso wa limao

Utakaso wa limao huhusisha kutumia mchanganyiko wa limao na maji pilipili na Mchanganyiko maalumu wa uji w matunda.

Utakaso wa siku 21 wa kutumia viinirishi mbadala na dawa za kulegeza utumbo na matumbo. Huhusisha kusitisha kula vyakula vya maziwa na maziwa, nyama, sukari na vyakula vya kusindikwa.

​

Je njia hizi zinafanya kazi kweli?

Hakuna tafiti ya kisayansi iliyofanyika dhidi ya ubora wa aina fulani ya dawa au tiba ya utakaso ambayo inafanya kazi, hivyo ubora na ufanisi wa aina hii ya tiba bado hazifahamiki.

​

Hata hivyo njia hizi humfanya mtu kutumia nishati kidogo mwilini na hivyo humsababisha kupoteza uzito kwa kuwa anatumia vyakula vyenye nishati kidogo sana.

​

Baadhi ya tafiti zilizofanyika zinaonyesha kwamba kutumia vyakula vyenye nishati kidogo sana kwa siku huwa na mchango mkubwa wa kupoteza uzito.

​

Je kuna madhara yoyote ya kiafya mtu anaweza kupata kutokana na tiba utakaso?

​

Ndio kuna madhara mtu anaweza kupata ikitegemea aina ya njia na hali ya afya ya mtu

Matatizo mengi hutokea kwa watu endapo watapungua uzito haraka mfano, kupata mawe kwenyekifuko cha nyongo, kuishiwa maji mwilini, kupungukiwa viinirishimuhimu mwilini. Upungufu wa vitamin n.k

​

Kwa watu wenye Matatizo ya figo baadhi ya tiba utakaso mfano ile ya kutumia juisi ya mboga za majani kwa wingi inaweza kupelekea kuharibika kwa figo zaidi kwa watu walio na tatizo la figo iliyoferi kwa mda mrefu.

​

Mambo ya msingi kufahamu

​

  • Njia hii ni nzuri kwa kupoteza uzito kwa mda mfupi

  • Ni njia ambayo haina utafiti mwingi wa kisayansi uliofanyika kuhusu kila aina ya njia ya utakaso

  • Ni muhimu kuwa na mtaalamu wa afya mwenye ujuzi na njia hizi akusimamie ili aweze kukukinga na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa kukupa ushauri nini cha kufanya

 

Unataka kupugnuza uzito kwa njia hii? kutana na madaktari wetu kupitia namba za simu chini ya tovuti hii au mawasiliano ya email

​

Toleo la 3

Imeboreshwa 12/2/2019

bottom of page