top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

10 Machi 2021 18:01:47

Abiraterone Acetate na ujauzito

Abiraterone Acetate na ujauzito

Abiraterone acetate, hutumika pamoja na prednisone kwenye matibabu ya saratani ya tezi dume


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Haipatani na ujauzito


Haipatani na ujauzito, ina maana gani?

Matumizi ya dawa hii au zingine zilizo kundi moja na hii au zile zinazofanana ufanyaji kazi na dawa hii kwa binadamu kwenye kipindi chochote kile cha ujauzito, imeonekana kuwa sumu kwenye uumbaji wa kichanga tumboni kwa na kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo cha kichanga au kijusi tumboni. Taarifa za uzazi kwa wanyama, endapo zipo zinathibitisha madhara. Dawa hii isitumike kwenye kipindi chochote kile katika ujauzito.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Haipatani na unyoyenyeshaji


Haipatani na unyoyenyeshaji, ina maana gani?

Kunawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha.


Hata hivyo mkusanyiko wa taarifa zinaonyesha kuwa dawa huweza kuwa sumu kali kwa kichanga, au haishauriwi kunyonyesha endapo dawa itahitajika kutumika kwa mama mwenye anayehitajika kutumia dawa hii. Mama anatakiwa asinyonyeshe anapotumia dawa hii au akiwa na ugonjwa unaotakiwa kutumia dawa hii.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Product information. Zytiga. Janssen Biotech, 2012.

bottom of page