top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

16 Juni 2021 19:28:51

Amphetamine na ujauzito

Amphetamine na ujauzito

Amphetamine ni dawa mojawapo kwenye kundi la simpathomimetiki inayofanya kazi ya kusisimua mfumo wa fahamu wa kati. Dawa zingine zilizo kundi hili ni dextroamphetamine na methamphetamine.


Ingawa matumizi ya dawa za amphetamine kama tiba huonekana kuwa na hatari kidogo kwa kichanga, matumizi yasiyo ya kitiba huwa sumu kali kwa kijusi na kichanga aliyezaliwa. Hivyo hairuhusiwi kutumika kwa matumizi yasiyo dawa kwenye ujauzito.


Kiasi cha dawa hupita na kuingia kwenye mazimwa na mama na imeonekana kuwa haina madhara makubwa kwa watoto wanyonyao, hata hivyo kwa ujumla dawa imeonekana kufanya watoto wawe wasumbufu (kulia lia) na kushindwa kulala vema.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Taarifa za binadamu (wanyama) zinaonyesha hatari ya kupata madhara


Taarifa za binadamu (wanyama) zinaonyesha hatari ya kupata madhara maana yake nini?

Taarifa za matumizi ya dawa hii au zile zilizo kundi moja na hii au zile zinazofanana namna zinavyofanya kazi na hii kwa binadamu na wanyama wajawazito , imeonekana kuwa sumu kwenye uumbaji wa kichanga tumboni kwa na kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo cha kichanga au kijusi tumboni katika kipindi chote cha ujauzito. Hata hivyo hatari inaweza kuvumiliwa endpo shida ya mama inahitaji dawa hii.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga


Hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga maana yake nini?

Inaweza kuwa taarifa juu ya matumizi kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii hazipo au zipo chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Hairuhusiwi kumnyonyesha mtoto unapotumia dawa hii.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

22 Aprili 2022 15:45:35

Rejea za mada hii;

bottom of page