top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

17 Machi 2021 19:57:19

Butoconazole na ujauzito

Butoconazole na ujauzito

Butoconazole hupatikana kama krimu ya kupaka kwa wajawazito wenye tatizo la fangasi. Taarifa chache kutoka kwenye binadamu wajawazito zinaweka dawa hii kwenye kundi la hatari kiasi cha madhaifu kwa mtoto.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito


Hakuna taarifa(taarifa ni chache) ya kuwepo madhara kwa binadamu- inaweza kupatana na ujauzito,ina maana gani?

Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, hata hivyo sifa ya ufanyaji kazi wa dawa inaonyesha kutokuwa na hatari yenye mashiko kusababisha madhara kwa kichanga aliye tumboni. Kwa mfano dawa zingine kwenye kundi moja au zenye kufanana ufanyaji kazi zinapatana na ujauzito au kiwango cha dozi ya dawa kwenye damu hakina mashiko kusababisha madhara. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji


Hakuna taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji, ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Weisberg M. Treatment of vaginal candidiasis in pregnant women. Clin Ther 1986;8:563–7.

2. Hagler L, Brett L. Treatment of vaginal candidiasis in pregnant women. Clin Ther 1987;9:559–60.

3. Weisberg M. Treatment of vaginal candidiasis in pregnant women. Clin Ther 1987;9:561.

bottom of page