top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

15 Machi 2021 19:12:11

Cetrizine na ujauzito

Cetrizine na ujauzito

Cetrizine ni dawa ya antihistamine kizazi cha pili cha H1 receptor antagonist. Dawa hii haipo kwenye kundi la dawa zinazosababisha madhaifu ya maumbile kwa kijusi tumboni na hakuna taarifa za kutosha kuchunguza madhara kwa kijusi kwa binadamu wajawazito. Ingawa cetirizine inaonekana kuwa si sumu kwa kichanga, inapendekezwa kutumia dawa za kunywa jamii ya antihistamine daraja la kwanza kama chlorpheniramine na tripelennamine, endapo kuna uhitaji wa kutumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito. Cetirizine na loratadine zilikuwa zinakubalika kutumika kama mbadala wa chlorpheniramine na tripelennamine, isipokuwa katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa haileti sumu kwenye uumbaji wa kijusi( kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii zote za wanyama waliofanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji ina maanisha nini?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Mazzotta Pet al. Treating allergic rhinitis in pregnancy. Safety considerations. Drug Saf 1999;20:361–75.

2. Horak F, et al. Comparative tolerability of second generation antihistamines. Drug Saf 1999;20:385–401.

3. Position Statement of a Joint Committee of the American College of Obstetricians and Gynecologists and the American College of Allergy, Asthma and Immunology. The use of newer asthma and allergy medications during pregnancy. Ann Allergy Asthma Immunol 2000;84:475–80.

4. Product information. Zyrtec. Pfizer, 2001.

5. Einarson A, et al. Prospective controlled study of hydroxyzine and cetirizine in pregnancy. Ann Allergy Asthma Immunol 1997;78:183-6.

6. Schatz M, et al. Antihistamines and pregnancy. Ann Allergy Asthma Immunol 1997;78:157–9.

7. Wilton LV, et al. The outcomes of pregnancy in women exposed to newly marketed drugs in general practice in England. Br J Obstet Gynaecol 1998;105:882–9.

8. Einarson A, et al. The antiemetic effect of cetirizine during pregnancy. Ann Pharmacol 2000;34:1486–7.

9. Weber-Schoendorfer C, et al. The safety of cetirizine during pregnancy—a prospective observational cohort study. Reprod Toxicol 2008;26:19–23.

bottom of page