top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

2 Septemba 2021 07:07:22

Ciprofloxacin kwa mjamzito

Ciprofloxacin kwa mjamzito

Ciprofloxacin ni dawa ya kutengenezwa jamii ya fluoroquinolone, dawa zingine kwenye kundi lake ni enoxacin, levofloxacin, lomefloxacin, norfloxacin, ofloxacin, sparfloxacin, nalidixic acid na cinoxacin


Matumizi ya ciprofloxacin wakati wa ujauzito hayajaonekana kuongeza hatari ya vichanga kupata madhaifu makubwa ya kiuumbaji. Licha ya kutokea kwa madhaifu mbalimbali ya kiuumbaji kwa vichanga wa wamama waliotumia dawa hii, hakuna muundo wa kueleweka kuhusu madhaifu hayo na kufanya yasiwe na mashiko sana. Hata hivyo imeonekana kuwa uhusiano wa moja kwa moja kusababisha baadhi ya madhaifu ya kimaumbile kwa vichanga ilipotumiwa wakati wa ujauzito.


Kutokana na taarifa hizi za binadamu na zingine za wanyama, matumizi ya ciprofloxacin haswa katika kipindi cha kwanza cha ujauzito( wiki 12 za mwanzo) yafanyike kwa tahadhari sana.


Baadhi ya tafiti zinashauri mjamzito asitumie kabisa dawa jamii ya fluoroquinolones (ciprofloxacin ni moja wapo) kwa sababu ya kuwa na hatari ya kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa kichanga. Tafiti nyingi zinashauri dawa salama zilizopo zitumike kama mbadala wa dawa hii kwa mjamzito.


Madhaifu ya kiuumbaji yaliyotokea kutokana na matumizi ya dawa hii ni madhaifu ya maumbile ya moyo,kinywa (mdomo sungura), vidole(kuwa na vidole vingi zaidi ya vitano), miguu na mikono( kuwa mifupi) na ya maumbile ya siri ya kichanga wa kiume( tundu la mkojo kufungukia sehemu tofauti na kawaida)



Matumizi kwa mama anayenyonyesha na vichanga


Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha kwa sababu inahusiana na uhalibifu wa maungio ya mwili na kufanya meno ya kichanga kuwa na rangi ya kijani inayodumu.


Matumizi kwa watoto wadogo ambao bado hawajakomaa hayashauriwi kutokana na sababu hizo pamoja na kuambatana na matatizo mengine kama saratani ya ngozi kama ilivyoonekana kwa tafiti za wanyama, kuua bakteria rafiki kwenye utumbo wa mtoto kunakoweza pelekea kupata maambukizi makali kwenye tumbo na mengine.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga


Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga ina maana gani?

Kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi ya ciprofloxacin binadamu kutoka kwenye dawa hii au dawa zilizo kundi moja au zinazofanana namna zinavyofanya kazi yake. Ikijumuisha ujauzito miezi mitatu ya kwanza, inaonyesha kuwa, dawa hii haiwakilishi kuwa na hatari yenye mashiko ya kuwa sumu kwa kichanga tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika muda wowote ule kwenye ujauzito. Taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu zinafanya taarifa za uzazi wa wanyama kutokuwa na mashiko.


Mfano wa tafiti zilizoonyesha madhara kwa vichanga wa wamam waliotumia dawa hii ni hizi;



Tafiti ya kwanza

Kati ya wajawazito 549 waliokuwa wanatumia dawa hii na kufuatiliwa kipindi cha ujauzito, na waliotumiwa dawa kwenye vipindi mbalimbali, matokeo yalikuwa haya;


Wamama waliobeba mimba mpaka kujifungua ni 415 ( wamama 390 walitumia dawa ndani ya kipindi cha wiki 12 za ujauzito , 22 kipindi baada ya wiki 12 za ujauzito na 18 haikufahamika kipindi gani cha ujauzito)


  • Watoto 356 walizaliwa kawaida bila matatizo ya kimaumbile

  • Watoto 15 walizaliwa kabla ya kukomaa

  • Watoto 6 walizaliwa wakiwa na wadogo kuliko wiki zao za ujauzito

  • watoto 20 walizaliwa wakiwa na madhaifu ya viungo mbalimbali vya mwili ( vichanga 19, mama zao walitumia dawa katika kipindi cha kwanza cha ujauzito)

  • Watoto 18 walipata madhaifu baada ya kuzaliwa yasiyohusiana na kuzaliwa kabla ya kukomaa


Madhaifu yaliyojitokeza kwenye tafiti hii ni;

  • Angioma

  • Kufanyika vibaya kwa nyonga

  • Trisomi

  • Haipospadiasisi( kufunguka kwa tundu la mkojo sehemu tofauti na kawaida

  • Kutofanyika vema kwa sikio la nje

  • Kuumbika chini ya kiwango(umbile) ubongo wa Cerebellum

  • Kupooza kwa mshipa wa fahamu wa oculomotor palsy

  • Kudumaa kwa mtoto tumboni

  • Kutozaliwa na mkono wa kulia

  • Kukunjamana kwa ngozi ya uso

  • Henia pande zote za kinena

  • Kutokuwa na moyo (mimba ilitoka)

  • Meno kuwa na rangi isiyo ya kawaida

  • Kutokuwa na tundu la sikio

  • Sindromu ya Rubinstein–Taybi

  • Kutofanyika kwa mfupa paja

  • Kuungana kwa mfupa ya mundu ya mnguu

  • Kuwa na vidole vingi zaidi

  • Madhaifu ya moyo, trakia, umio , mrija wa urethra, puru na kibofu cha nyongo

  • Madhaifu ya mifupa


Mtafiti alishauri kuwa dawa salama zaidi zitumike wakati wa ujauzito badala ya ciprofloxacin.



Tafiti ya pili

Tafiti hii ilifanyika kwenye makundi mawili yanayohusisha wamama 200 waliopewa dawa hii na wamama 200 ambao hawakupewa dawa hii na matokeo yake yalikuwa kama yafuatavyo;


Waliotumia dawa, mimba 18 zilitoka wakati wale ambao hawakutumia dawa ni mimba 10 zilitoka

Hakuna utofauti uliokuwepo kwa watoto waliozaliwa hawajakomaa, shida ya upumuaji, njia ya kujifungua na kuzaliwa na uzito kidogo.


Madhaifu ya kiuumbaji yalitokea kwa watoto 3 katiya 133 waliozaliwa kwa wamama waliotumia dawa, na 5 kati ya watoto 188 waliozaliwa kwa wamama ambao hawakutumia dawa. Madhaifu yaliyotokea kwa watoto wa mama waliotumia dawa ni madhaifu ya moyo ( VSD) na kutofunga kwa mshipa wa ductus arteriosus, wakati madhaifu kwa wamama ambao hawakutumia dawa ni madhaifu ya moyo, (VSD na ASD), kufunguka kwa tundu la mkojo sehemu isiyo sahihi na fupa nyonga kutokaa sehemu yake asili.


Kuna tafiti zingine nyingi zilizofanyika ambazo unaweza kusoma kwenye rejea za mada hii.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Ina uwezekano mkubwa kuwa sumu


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii isitumike kwa mama anayenyonyesha.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

22 Aprili 2022 15:26:04

Rejea za mada hii

1. Norrby SR, Lietman PS. Safety and tolerability of fluoroquinolones. Drugs 1993;45(Suppl 3):59–64.

2. Schaefer C, et al. Pregnancy outcome after prenatal quinolone exposure. Evaluation of a case registry of the European Network of Teratology Information Services (ENTIS). Eur J Obstet Gynecol Reprod Biol 1996;69:83–9.

3. Product information. Cipro. Miles Pharmaceutical, 1993.

4. Polachek H, et al. Transfer of ciprofloxacin, ofloxacin and levofloxacin across the perfused human placenta in vitro. Eur J Obstet Gynecol Reprod Biol 2005;122:61–5.


5. Bomford JAL, et al. Ciprofloxacin use during pregnancy. Drugs 1993;45(Suppl 3):461–2.

6. Berkovitch M, et al. Safety of the new quinolones in pregnancy. Obstet Gynecol 1994;84:535–8.

7. Koul PA, et al. Ciprofloxacin for multiresistant enteric fever in pregnancy. Lancet 1995;346:307–8.

8. Leung D, et al. Treatment of typhoid in pregnancy. Lancet 1995;346:648.

9. Pastuszak A, et al. New postmarketing surveillance data supports a lack of association between quinolone use in pregnancy and fetal and neonatal complications. Reprod Toxicol 1995;9:584.

10. Skannal DG, Dungy-Poythress LJ, Miodovnik M, First MR. Pregnancy in a combined liver and kidney transplant recipient with type 1 primary hyperoxaluria. Obstet Gynecol 1995;86:641–3.

11. Baroncini A, Calzolari E, Calabrese O, Zanetti A. First-trimester exposure to ciprofloxacin (abstract). Teratology 1996;53:24A.

12. Wilton LV, Pearce GI, Mann RD. A comparison of ciprofloxacin, norfloxacin, ofloxacin, azithromycin, and cefixime examined by observational cohort studies. Br J Clin Pharmacol 1996;41:277–84.

13. Ludlam H, Wreghitt TG, Thornton S, Thomson BJ, Bishop NJ, Coomber S, Cunniffe J. Q fever in pregnancy. J Infect 1997;34:75–8.

14. Loebstein R, et al. Pregnancy outcome following gestational exposure to fluoroquinolones: a multicenter prospective controlled study. Antimicrob Ag Chemother 1998;42:1336–9.

15. Wogelius P, et al. Further analysis of the risk of adverse birth outcome after maternal use of fluoroquinolones. Int J Antimicrob Agents 2005;26:323–6.

16. Cooper WO, et al. Antibiotics potentially used in response to bioterrorism and the risk of major congenital malformations. Paediatr Perinat Epidemiol 2009;23:18–28.

17. Giamarellou H, et al. Pharmacokinetics of three newer quinolones in pregnant and lactating women. Am J Med 1989;87(Suppl 5A):49S–51S.

18. Cover DL, Mueller BA. Ciprofloxacin penetration into human breast milk: a case report. Ann Pharmacother 1990;24:703–4.

19. Gardner DK, Gabbe SG, Harter C. Simultaneous concentrations of ciprofloxacin in breast milk and in serum in mother and breastfed infant. Clin Pharm 1992;11:352–4.

20. Harmon T, et al. Perforated pseudomembranous colitis in the breastfed infant. J Pediatr Surg 1992;27:744–6.

21. Lumbiganon P, et al. Ciprofloxacin in neonates and its possible effect on the teeth. Pediatr Infect Dis J 1991;10:619–20.

22. Committee on Drugs, American Academy of Pediatrics. The transfer of drugs and other chemicals into human milk. Pediatrics 2001;108:776–89.

bottom of page