top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

19 Machi 2021 19:21:24

Delavirdine na ujauzito

Delavirdine na ujauzito

Taarifa chache za matumizi kwa binadamu wajawazito hazitoshi kutoa utabiri wa hatari ya matumizi ya dawa hii kwa wajawazito. Taarifa za wanyama zinaonyesha kuwa dawa hii ni hatari kwa kijusi anayekuwa tumboni mwa mama. Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa za kutosha, endapo dawa hii inapaswa kutumika, isisitishwe kutokana na ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni


Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni, ina maanisha nini?

Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, lakini faida ni kubwa zaidi zikitumiwa na mama kuliko madhara yanayofahamika au kutofahamika kuwa yanaweza kutokea kwa kijusi-kichanganya tumboni. Kwa mama dawa zinazidi madhara yanayofahammika. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Haipatani na unyoyenyeshaji


Haipatani na unyoyenyeshaji , ina maanisha nini?

Kunawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha. Hata hivyo mkusanyiko wa taarifa zinaonyesha kuwa dawa huweza kuwa sumu kali kwa kichanga, au haishauriwi kunyonyesha endapo dawa itahitajika kutumika kwa mama mwenye anayehitajika kutumia dawa hii. Mama anatakiwa asinyonyeshe anapotumia dawa hii au akiwa na ugonjwa unaotakiwa kutumia dawa hii.


ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Product information. Rescriptor. Pfizer, 2006.

2. Carpenter CCJ, et al. Antiretroviral therapy for HIV infection in 1996. JAMA 1996;276;146–54.

3. Minkoff H, Augenbraun M. Antiretroviral therapy for pregnant women. Am J Obstet Gynecol 1997;176:478–89.

4. Minkoff H. Human immunodeficiency virus infection in pregnancy. Obstet Gynecol 2003;101:797–810.

5. Panel on Antiretroviral Guidelines for Adults and Adolescents. Guidelines for the Use of Antiretroviral

6. Panel on Treatment of HIV-Infected Pregnant Women and Prevention of Perinatal Transmission.

7. Brown ZA, Watts DH. Antiviral therapy in pregnancy. Clin Obstet Gynecol 1990;33:276–89.

8. De Martino M, et al. HIV-1 transmission through breast-milk: appraisal of risk according to duration of feeding. AIDS 1992;6:991–7.

9. Van de Perre P. Postnatal transmission of human immunodeficiency virus type 1: the breast feeding dilemma. Am J Obstet Gynecol 1995;173:483–7.

bottom of page