top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

17 Machi 2021 20:20:15

Flucytosine na ujauzito

Flucytosine na ujauzito

Flucytosine huvunjwa mwilini kuwa kemikali ya 5-fluorouracil, kemikali inayofahamika kuwa teratogen(husababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa mtoto) hivyo endapo inawezekana, usitumie kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito


Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito, ina maanisha nini?

Ushahidi wa dawa hii au dawa zingine zinazofanana nah ii unaonyesha kuwepo kwa hatari ya kuleta sumu kwenye uumbaji wa kichanga tumboni kwa na kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo cha kichanga au kijusi tumboni katika kipindi cha kwanza tu na sio kipindi cha pili au tatu. Taarifa za madhara ya dawa hii kwa binadamu zinamashiko zaidi kuliko taarifa za tafiti kwa wanyama.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu, ina maanisha nini?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii isitumike kwa mama anayenyonyesha.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Chen CP, Wang KG. Cryptococcal meningitis in pregnancy. Am J Perinatol 1996;13:35–6.

2. Chotmongkol V, Siricharoensang S. Cryptococcal meningitis in pregnancy: a case report. J Med Assoc Thai 1991;74:421–2.

3. Curole DN. Cryptococcal meningitis in pregnancy. J Reprod Med 1981;26:317–9.

4. Diasio RB, et al. Evidence for conversion of 5-fluorocytosine to 5-fluorouracil in humans: possible factor in 5-fluorocytosine clinical toxicity. Antimicrob Agents Chemother 1978;14:903–8.

5. Philpot CR, Lo D. Cryptococcal meningitis in pregnancy. Med J Aust 1972;2:1005–7.

6. Product information. Ancobon. ICN Pharmaceuticals, 2000.

7. Schonebeck J, Segerbrand E. Candida albicans septicaemia during first half of pregnancy successfully treated with 5-fluorocytosine. Br Med J 1973;4:337–8.

8. Stafford CR, et al. Cryptococcal meningitis in pregnancy. Obstet Gynecol 1983;62(3 Suppl): 35s–7s.

bottom of page