Mwandishi
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
19 Machi 2021, 18:44:11

Isoniazid na ujauzito
Isoniazid haionekani kuwa kundi la dawa zinazofahamika kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii wakati wa ujauzito. Inashauriwa kuendelea kutumia dawa hii endapo imechaguliwa kutumika kwa sababu hatari za TB kwa mama ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto kutokana na kutumia dawa hii.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni
Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni, ina maanisha nini?
Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, lakini faida ni kubwa zaidi zikitumiwa na mama kuliko madhara yanayofahamika au kutofahamika kuwa yanaweza kutokea kwa kijusi-kichanganya tumboni. Kwa mama dawa zinazidi madhara yanayofahammika. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji, ina maanisha nini?
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
4 Juni 2025, 18:58:18
Snider DE, et al. Treatment of tuberculosis during pregnancy. Am Rev Respir Dis. 1980;122(1):65–79.
(Inaelezea usalama na matumizi ya isoniazid kwa wanawake wajawazito wanaotibiwa TB.)American Thoracic Society. Treatment of tuberculosis and tuberculosis infection in adults and children. Am Rev Respir Dis. 1986;134(2):355–63.
(Inatoa miongozo ya matumizi ya isoniazid na dawa nyingine za TB kwa watu wote, ikijumuisha wanawake wajawazito.)Medchill MT, Gillum M. Diagnosis and management of tuberculosis during pregnancy. Obstet Gynecol Surv. 1989;44(2):81–4.
(Inajadili uchunguzi na usimamizi wa TB kwa wanawake wajawazito, ikijumuisha usalama wa isoniazid.)Toman K. Tuberculosis case detection, treatment, and monitoring: Questions and answers. 2nd ed. Geneva: World Health Organization; 2004.
(Inashughulikia miongozo ya kimataifa kuhusu matumizi ya isoniazid na dawa za TB kwa wanawake wajawazito.)Centers for Disease Control and Prevention. Managing tuberculosis in pregnancy. MMWR Recomm Rep. 2002;51(RR-18):1–9.
(Rejea hii inashauri matumizi salama ya isoniazid kwa wanawake wajawazito na uteuzi wa matibabu.)Shepard TH. Catalog of Teratogenic Agents. 6th ed. Baltimore: Johns Hopkins University Press; 1989. p. 570–1.
(Rejea ya tathmini ya teratogenicity ya isoniazid katika ujauzito.)