top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

17 Machi 2021 20:05:19

Itraconazole na ujauzito

Itraconazole na ujauzito

Itraconazole ni dawa ya kutibu fangasi jamii ya triazole. Uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwenye ujauzito unaonyesha kuwepo kwa hatari kidogo sana ya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii wakati wa ujauzito. Hata hivyo dawa zingine za triazole fluconazole, imeonyesha mahusiano kusababisha madhaifu ya kimaumbile kwa mtoto, mahusiano hayo yanahisiwa kuhusiana na dozi iliyotumika. Kwa dawa ya itraconazole, taarifa za wanyama haziwezi kujitosheleza kutafsiri kuwa sumu kwa binadamu mjamzito. Hivyo ni vema dawa hii ikazuiwa kipindi cha kwanza cha ujauzito kama ikiwezekana. Endapo matumizi ya dawa hii ni lazima kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito, mama anatakiwa ashauriwe kuwa hatari ya madhaifu kwa kichanga ni ndogo san ahata kama yapo.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo, ina maanisha nini?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa haileti sumu kwenye uumbaji wa kijusi (kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii zote za wanyama waliofanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu ina maanisha nini?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii isitumike kwa mama anayenyonyesha.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. American Hospital Formulary Service. Drug Information 1997. Bethesda, MD: American Society of Health-System Pharmacists, 1997:93–5.

2. Product information. Sporanox. Janssen Pharmaceutica, 2001.

3. Rosa F. Azole Fungicide Pregnancy Risks. Presented at the Ninth International Conference of the Organization of Teratology Information Services, May 2–4, 1996, Salt Lake City,Utah.

4. Wilton LV, et al. The outcomes of pregnancy in women exposed to newly marketed drugs in general practice in England. Br J Obstet Gynaecol 1998;105:882–9.

5. Bar-Oz B, et al. Pregnancy outcome after in utero exposure to itraconnazole: a prospective cohort study. Am J Obstet Gynecol 2000;183:617–20.

6. Bar-Oz B, et al. Reporting bias in retrospective ascertainment of drug-induced embryopathy. Lancet 1999;354:1700–1.

7. De Santis M, et al. First-trimester itraconazole exposure and pregnancy outcome; a prospective cohort study of women contacting teratology information services in Italy. Drug Safety 2009;32:239–44.

bottom of page