top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

17 Machi 2021 19:23:50

Kanamycin na ujauzito

Kanamycin na ujauzito

Kanamycin imeripotiwa kuwa sumu kwenye masikio, hata hivyo hakuna ripoti ya kusababisha madhaifu mengine ya kiumbaji ya maungo mbalimbali ya mwili kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Taarifa za binadamu (wanyama) zinaonyesha hatari ya kupata madhara


Taarifa za binadamu (wanyama) zinaonyesha hatari ya kupata madhara ina maanisha nini?

Taarifa za matumizi ya dawa hii au zile zilizo kundi moja na hii au zile zinazofanana namna zinavyofanya kazi na hii kwa binadamu na wanyama wajawazito , imeonekana kuwa sumu kwenye uumbaji wa kichanga tumboni kwa na kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo cha kichanga au kijusi tumboni katika kipindi chote cha ujauzito. Hata hivyo hatari inaweza kuvumiliwa endpo shida ya mama inahitaji dawa hii.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji ina maanisha nini?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Nishimura H, Tanimura T. Clinical Aspects of the Teratogenicity of Drugs . New York, NY: American Elsevier, 1976:131.

2. Good R, Johnson G. The placental transfer of kanamycin during late pregnancy. Obstet Gynecol1971;38:60–2.

3. Jones HC. Intrauterine ototoxicity. A case report and review of literature. J Natl Med Assoc 1973;65:201–3.

4. Wilson JT. Milk/plasma ratios and contraindicated drugs. In: Wilson JT, ed. Drugs in Breast Milk.Balgowlah, Australia: ADIS Press, 1981:79.

5. O’Brien T. Excretion of drugs in human milk. Am J Hosp Pharm 1974; 31:844–54.

6. Committee on Drugs, American Academy of Pediatrics. The transfer of drugs and other chemicals into human milk. Pediatrics 2001;108:776–89.

bottom of page