Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
10 Machi 2021 19:33:19

Mebendazole na ujauzito
Mebendazole inatumika kipindi cha ujauzito kwenye matibabu ya minyoo jamii ya 'Ascaris lumbricoides' kwa jina jingine ' Roundworm', 'Trichuris trichiura' au 'Whipworm' na 'Enterobius vermicularis' kwa jina jingine 'Threadworm', 'Seatworm' au , 'Pinworm'. Dawa piperazine inaweza kutumiaka pia kwa matibabu ya minyoo hii kama kutokana na mapendekezo ya tafiti zingine.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga
Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga, ina maana gani?
Kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu kutoka kwenye dawa hii au dawa zilizo kundi moja au zinazofanana namna zinavyofanya kazi yake. Ikijumuisha ujauzito miezi mitatu ya kwanza, inaonyesha kuwa, dawa hii haiwakilishi kuwa na hatari yenye mashiko ya kuwa sumu kwa kichanga tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika muda wowote ule kwenye ujauzito. Taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu zinafanya taarifa za uzazi wa wanyama kutokuwa na mashiko.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji, inamaana gani?
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:21:36
Rejea za mada hii
1. D’Alauro F, et al. Intestinal parasites and pregnancy. Obstet Gynecol 1985;66:639–43.
2. Ellis CJ. Antiparasitic agents in pregnancy. Clin Obstet Gynecol 1986;13:269–75.
3. Leach FN. Management of threadworm infestation during pregnancy. Arch Dis Child 1990;65:399 400.
4. Product information. Vermox. McNeil Consumer, 2000.
5. Beard TC, et al. Medical treatment for hydatids. Med J Aust 1978;1:633–5.
6. Shepard TH. Catalog of Teratogenic Agents , 8th ed. Baltimore, MD: Johns Hopkins University Press, 1995:261.
7. Blondheim DS, Klein R, Ben-Dror G, Schick G. Trichinosis in southern Lebanon. Isr J Med Sci 1984;20:141–4.
8. Draghici O, et al. Comments with reference to a trichinellosis focus. Rev Ig (Bacteriol) 1976;21:99–104.
9. June-Seek Choi, et al. Foetal outcomes after exposure to albendazole in early pregnancy. https://www.tandfonline.com/doi/full/10.1080/01443615.2017.1326886?needAccess=true. Imechukuliwa 20.03.2021