top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

10 Machi 2021 18:42:47

Paracetamol na ujauzito

Paracetamol na ujauzito

Acetaminophen (paracetamol au panado) imekuwa ikitumika mara nyingi katika kipindi chochote katika ujauzito. Ingawa ilifahamika kutokuwa na hatari kwa kichanga, kuna baadhi ya ripoti zimehoji kuhusu hili haswa kwa wamama wanaotumia dawa hii kwa muda mrefu au kwa wamama wenye jeni tofauti. Taarifa zaidi zinahitajika kupatikana ili kuthibitisha endapo kweli hakuna madhara yoyote kwa kijusi, hata hivyo inashauriwa isitumike mara kwa mara kipindi cha ujauzito.

Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito

Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga

Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga, ina maana gani?

Kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu kutoka kwenye dawa hii au dawa zilizo kundi moja au zinazofanana namna zinavyofanya kazi yake. Ikijumuisha ujauzito miezi mitatu ya kwanza, inaonyesha kuwa, dawa hii haiwakilishi kuwa na hatari yenye mashiko ya kuwa sumu kwa kichanga tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika muda wowote ule kwenye ujauzito. Taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu zinafanya taarifa za uzazi wa wanyama kutokuwa na mashiko.

Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha

Inapatana na unyonyeshaji

Inapatana na unyonyeshaji, ina maana gani?

Kiasi kidogo cha dawa hii kinawezekana kuingia kwenye maziwa ya mama, kiasi hiki hakina mashiko ya kusababisha sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii haitarajiwi kusababisha madhara kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii.Acetaminophen(parasetamol au panado) imekuwa ikitumika mara nyingi katika kipindi chochote katika ujauzito. Ingawa ilifahamika kutokuwa na hatari kwa kichanga, kuna baadhi ya ripoti zimehoji kuhusu hili haswa kwa wamama wanaotumia dawa hii kwa muda mrefu au kwa wamama wenye jeni tofauti. Taarifa zaidi zinahitajika kupatikana ili kuthibitisha endapo kweli hakuna madhara yoyote kwa kijusi, hata hivyo inashauriwa isitumike mara kwa mara kipindi cha ujauzito.

Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito

Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga

Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga, ina maana gani?

Kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu kutoka kwenye dawa hii au dawa zilizo kundi moja au zinazofanana namna zinavyofanya kazi yake. Ikijumuisha ujauzito miezi mitatu ya kwanza, inaonyesha kuwa, dawa hii haiwakilishi kuwa na hatari yenye mashiko ya kuwa sumu kwa kichanga tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika muda wowote ule kwenye ujauzito. Taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu zinafanya taarifa za uzazi wa wanyama kutokuwa na mashiko.

Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha

Inapatana na unyonyeshaji

Inapatana na unyonyeshaji, ina maana gani?

Kiasi kidogo cha dawa hii kinawezekana kuingia kwenye maziwa ya mama, kiasi hiki hakina mashiko ya kusababisha sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii haitarajiwi kusababisha madhara kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Levy G, et al. Evidence of placental transfer of acetaminophen. Pediatrics 1975;55:895.

2. Char VC, et al. Polyhydramnios and neonatal renal failure—a possibleassociation with maternal acetaminophen ingestion. J Pediatr 1975;86:638–9.

3. Rayburn W, et al. Acetaminophen pharmacokinetics: comparison between pregnant and nonpregnant women. Am J Obstet Gynecol 1986;155:1353–6.

4. Beaulac-Baillargeon L, et al. Paracetamol pharmacokinetics during the first trimester of human pregnancy. Eur J Clin Pharmacol 1994;46:451–4.

5. Rollins DE, et al. Acetaminophen: potentially toxic metaboliteformed by human fetal and adult liver microsomes and isolated fetal liver cells. Science 1979;205:1414–6.

6. Haibach H, et al . Acetaminophen overdose with fetaldemise. Am J Clin Pathol 1984;82:240–2.

7. Wang P-H, et al. Acetaminophen poisoning in late pregnancy. A case report. J Reprod Med 1997;42:367–71.

8. Byer AJ, et al. Acetaminophen overdose in the third trimester of pregnancy. JAMA 1982;247:3114–5.

9. Stokes IM. Paracetamol overdose in the second trimester of pregnancy. Case report. Br J Obstet Gynaecol 1984;91:286–8.

bottom of page