top of page

Mwandishi

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

19 Machi 2021, 18:46:53

Pyrazinamide na ujauzito

Pyrazinamide na ujauzito

Pyrazinamide dawa mojawapo inayotumika kwenye matibabu ya kutibu Kifua kikuu (TB) iliyotokana na niacinamide. Hakuna taari za matumizi kwa wanyama wajawazito zinazoendana na dawa hii n ahata hivyo taarifa za matumizi kwa binadamu wajawazito zinaonyesha kutokuwepo na hatari ya kupata madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii. Hivyo kutokana na TB kuwa hatari zaidi kuliko madhara ya dawa hii, inashauriwa endapo imeanzishwa, isisitishwe kwa sababu ya ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni


Inapatana na ujauzito- faida kwa mama >>hatari kwa Kijusi-kichanga tumboni, ina maana gani?

Kunaweza kuwa au kutokuwa na uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwa binadamu, lakini faida ni kubwa zaidi zikitumiwa na mama kuliko madhara yanayofahamika au kutofahamika kuwa yanaweza kutokea kwa kijusi-kichanganya tumboni. Kwa mama dawa zinazidi madhara yanayofahammika. Taarifa za uzazi kwa wanyama hazina mahusiano.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji, ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

4 Juni 2025, 18:57:49

  1. Product information. Rifabutin. [Kampuni ya dawa], tarehe ya chapisho; [mwaka].
    (Mfano: Product information. Rifabutin. Pharmacia & Upjohn, 2005.)

  2. Snider DE Jr, Powell KE. Should women taking antituberculosis drugs breastfeed? Arch Intern Med. 1984;144(3):589–90.
    (Inajadili usalama wa dawa za anti-tuberculosis, ikijumuisha rifabutin, kwa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha.)

  3. American Thoracic Society. Treatment of tuberculosis and tuberculosis infection in adults and children. Am Rev Respir Dis. 1986;134(2):355–63.
    (Inaelezea ushauri kuhusu matumizi ya dawa za TB, ikiwemo rifabutin, kwa wagonjwa wajawazito.)

  4. Liu J, et al. Pharmacokinetics of rifabutin in pregnant women with tuberculosis. Antimicrob Agents Chemother. 2001;45(4):1149–54.
    (Utafiti huu unaonyesha jinsi rifabutin inavyosambaa mwilini mwa wanawake wajawazito na usalama wake.)

  5. Centers for Disease Control and Prevention. Use of rifabutin for the treatment of tuberculosis: recommendations of the Advisory Committee for Elimination of Tuberculosis. MMWR Recomm Rep. 1993;42(RR-7):1–11.
    (Inatoa miongozo kuhusu matumizi ya rifabutin, ikijumuisha vipengele vya usalama kwa wajawazito.)

  6. Shepard TH. Catalog of Teratogenic Agents. 6th ed. Baltimore: Johns Hopkins University Press; 1989. p. 558–9.
    (Rejea ya utafiti wa teratogenicity wa rifabutin na dawa zinazofanana.)

bottom of page