Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
19 Machi 2021 18:54:59
Rifapentine na ujauzito
Rifapentine ilikuwa sumu na kuhusiana kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa kijusi ilipotumika kwenye majaribio mawili ya wanyama wajawazito kwa kutumia dozi inayokaribia kufanana na ile ya binadamu.Uzoefu kwa binadamu ni kutoka kwa wajawazito watatu, wajawazito wawili waliotumia waliishia mimba kutoka kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito. Ingawa wajawazito hawa walikuwa na vihatarishi vingine vilivyoweza kusababisha pia mimba kutoka, madhara yaliyojitokeza yanatosha kuashiria kutumika kwa umakini dawa hii inapotumiwa wakati ujauzito mdogo. Mpaka pale taarifa zingine zitakapokuwepo kupinga hii, matumizi ya rifapentine yanatakiwa kuepukwa kwneye kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari
Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari , ina maana gani?
Inawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu kwa matumizi kwa binadamu au taarifa chache zilizopo zinaonyesha kutohusiana na matatizo ya kiuumbaji kwa mtoto kama madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa hii inasababisha sumu kwa kwenye ukuaji wa kijusi cha wanyama jamii mbili waliopewa dawa hii kwenye dozi ambayo haisababishi sumu kwa mama mjamzito, dozi iliyo chini ya mara kumu ya dozi ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji, ina maana gani?
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:21:36
Rejea za mada hii
1. Product information. Priftin. Aventis Pharmaceuticals, 2004.
2. Center for Drug Evaluation and Research. FDA. Approval package: Priftin (Rifapentine) 150 mg tablets. Hoechst Marion Roussel, June 22, 1998.
3. Medchill MT, Gillum M. Diagnosis and management of tuberculosis during pregnancy. Obstet Gynecol Surv 1989;44:81–4.
4. American Thoracic Society. Treatment of tuberculosis and tuberculosis infection in adults and children. Am J Respir Crit Care Med 1994;149:1359–74.
5. CDC. Treatment of tuberculosis. MMWR 2003;52(RR11):1–77.
6. World Health Organization. Treatment of Tuberculosis: Guidelines for National Programs . 2nd ed. Geneva, Switzerland, 1997.