Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
13 Agosti 2021 18:59:52
Secnidazole kwa mjamzito
Secnidazole ni dawa mojawapo kwenye kundi la nitroimidazole (inafanya kazi sawa na metronidazole, tinidazole) iliyoruhusiwa kutumika mwaka 2017 na shirika la dawa la Amerika (FDA). Kuna taarifa chache zisizotosha kutoa jumuisho kuhusu usalama wake wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Taarifa za wanyama zimeshindwa kutoa ushahidi wa kusababisha ulemavu wa viungo kwa vichanga wanaozaliwa na wanyama wajawazito waliopewa dawa hii kwenye dozi ya miligramu 100, 300 na 1000 kwa kilo, sawa na mara nne ya dozi inayotumiwa na binadamu.
Madhaifu yaliyoonekana kwa wanyama wajawazito waliotumia dozi kubwa ni kuongezeka uzito, hata hivyo dozi kubwa kwa panya ilisababisha wapunguze kula na hivyo kupungua uzito.
Hakuna ushahidi wa madhaifu ya ukuaji kwa watoto wa panya na sungura ambao wazazi wao walitumia dawa kwenye dozi iliyotajwa hapo huu.
Taarifa za madhara kwa binadamu hazijitoshelezi na mtengeneza dawa hajashauri dawa hii kutumika kwa mjamzito.
Hata hivyo unashauriwa usitumie dawa ambazo hazifahamiki madhara yake, badala yake unapaswa utumie dawa yenye uwezo wa kutibu ugonjwa huo ambayo tayari imetumika kwa muda mrefu na madhara yake yanafahamika.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- hakuna taarifa husika kwa wanyama
Nini maana ya hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- hakuna taarifa husika kwa wanyama?
Hakuna taarifa kuhusu matumizi ya secnidazole kwa binadamu au taarifa za wanyama zinazoendana na matumizi ya dawa hii au taarifa za uzoefu wa matumizi kwa binadamu katika kipindi cha ujauzito ikiwa pamoja na kipindi cha kwanza. Hatari kwa kichanga tumboni, hazifahamiki.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga
Nini maana ya hakuna (chache) taarifa kwa binadamu- inawezekano mkubwa wa kuwa sumu kwenye ukuaji wa kichanga?
Inaweza kuwa taarifa juu ya matumizi ya secnidazole kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii hazipo au zipo chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Hairuhusiwi kumnyonyesha mtoto unapotumia secnidazole.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023 17:20:53
Rejea za mada hii:
1. FDA. Secnidazole. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2017/209363s000lbl.pdf. Imechukuliwa 13.08.2021
2. FDA. Secnidazole. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/nda/2017/209363Orig1s000TOC.cfm. Imechukuliwa 13.08.2021
3. Secnidazole. https://www.fda.gov/drugs/drug-approvals-and-databases/drug-trials-snapshot-solosec. Imechukuliwa 13.08.2021