top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

19 Machi 2021 19:34:16

Telbivudine na ujauzito

Telbivudine na ujauzito

Kuna taarifa chache kuhusiana na matumizi ya dawa hii kwa binadamu wajawazito. Ingawa taarifa za wanyama wajawazito zinatia moyo, taarifa za binadamu wajawazito zinatakiwa kupatikana ili kutoa hitimisho kuhusu usalama wake kwenye ujauzito wa binadamu. Inasemekana kwenye maandishi kwamba, kutumia dawa zenye ufanyaji kazi kama hii huathiri uzazi na huwa sumu kwa kichanga, hata hivyo mambo haya hayajaonekana kwenye tafiti zilizofanyika kwa wanyama na tafiti kwa binadamu hazijafanyika. Endapo itashauriwa kutumika, inashauriwa kutositishwa kwa sababu ya ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo, ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa haileti sumu kwenye uumbaji wa kijusi (kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii zote za wanyama waliofanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili.


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu, ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii isitumike kwa mama anayenyonyesha.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Teerha Piratvisuth, et al. Comprehensive review of telbivudine in pregnant women with chronic hepatitis B. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4807307/#. Imechukuliwa 19.03.2021

2. Lawrence RM, Lawrence RA. The breast and the physiology of lactation. In: Creasy RK, Resnik R. eds. Maternal and Fetal Medicine. 5th ed. Philadelphia, PA: WB Saunders, 2004:146, 148.

3. Bridges EG, Selden JR, Luo S. Nonclinical safety profile of telbivudine, a novel potent antiviral agent for treatment of hepatitis B. Antimicrob Agents Chemother 2008;52:2521–8.

4. Weihui Sun et al.Telbivudine treatment started in early and middle pregnancy completely blocks HBV vertical transmission. https://bmcgastroenterol.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12876-017-0608-7. Imechukuliwa 19.03.2021

5. Ren, Cuicui MD, et al. Efficacy and safety of telbivudine treatment for the prevention of HBV perinatal transmission. https://journals.lww.com/mdjournal/fulltext/2020/06120/efficacy_and_safety_of_telbivudine_treatment_for.44.aspx. Imechukuliwa 19.03.2021

bottom of page