top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

18 Machi 2021 18:33:28

Tinidazole na ujauzito

Tinidazole na ujauzito

Taarifa za uzoefu wa matumizi ya tinidazole kwa binadamu wajawazito zipo chache sana. Hata hivyo kunaonekana kuwepo kwa ongezeko kiasi la vifo vya watoto kwenye ujauzito wa wanyama walipotumia inayokaribiana na ile ya binadamu. Hakuna ushahidi mwingine unaosema kutokea kwa madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga waliozaliwa na wanyama waliotumia dawa hii. Tinidazole hufanana kikemia na dawa ya metronidazole. Itakuwa si hekima hata hivyo kufanya mbadala kutibu magonjwa yanayotibiwa na metronidazole kwa kutumia dawa hii. Tinidazole inatakiwa kutumika pale tu endapo metronidazole imefeli kufanya kazi ya kuondoa maradhi. Hata hivyo ni mpaka pale taarifa zaidi zitakapopatikana, ni vema kuzuia kutumia tinidazole katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari ya wastani


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari ya wastani ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa hii ni sumu kwenye uumbaji wa kijusi( kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii moja mnyama aliyefanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Usinyonyeshe unapotumia dawa hii ( kwa watumiaji wa dawa ya dozi moja tu)


na


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inauwezekano mkubwa kuwa sumu( dozi ya mwendelezo)


na


Usinyonyeshe unapotumia dawa hii ( kwa watumiaji wa dawa ya dozi moja tu) ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Sifa za ufanyaji kazi wa dawa zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kuwa sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii isitumike kwa mama anayenyonyesha


Usinyonyeshe unapotumia dawa hii ( kwa watumiaji wa dawa ya dozi moja tu)

Dawa hii inaweza kuwa haiingii kwenye maziwa au kuingia kwenye maziwa ya mama kwa kiasi kidogo sana, hata hivyo faida za matumizi ya dawa hii kwa mama zinazidi kwa kiasi kikubwa kunyonyesha mtoto. Unyonyeshaji unapaswa kusimamishwa mpaka mama atakapomaliza dozi ya dawa hii na kiwango katika damu kuwa chini ya kiwango cha kitiba.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:21:36

Rejea za mada hii

1. Product information. Tindamaz. Presutti Laboratories, 2004.

2. Karhunen M. Placental transfer of metronidazole and tinidazole in early human pregnancy after a single infusion. Br J Clin Pharmacol 1984;18:254–7.

3. Czeizel AE, et al. Oral tinidazole treatment during pregnancy and teratogenesis. Int J Gynecol Obstet 2003;83:305–6.

4. Nanda N et al. Trichomoniasis and its treatment. Expert Rev Anti Infect Ther 2006;4:125–35.

5. CDC. Sexually transmitted diseases treatment guidelines, 2006. MMWR 2006;55(RR11):1–94.

6. Welling PG, Monro AM. The pharmacokinetics of metronidazole and tinidazole in man. Arzneimittelforsch 1972;22:2128–32. As cited in Mannisto PT, Karhunen M, Koskela O, Suikkari AM, Mattila J, Haataja H. Concentrations of tinidazole in breast milk. Acta Pharmacol Toxicol (Copenh) 1983;53:254–6.

7. Mannisto PT et al. Concentrations of tinidazole in breast milk. Acta Pharmacol Toxicol (Copenh) 1983;53:254–6.

8. Evaldson GR, et al. Tinidazole milk excretion and pharmacokinetics in lactating women. Br J Clin Pharmacol 1985;19:503–7.

9. Committee on Drugs, American Academy of Pediatrics. The transfer of drugs and other chemicals into human milk. Pediatrics 2001;108:776–89.

bottom of page