top of page

USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA  UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Meropenem na ujauzito

Meropenem na ujauzito

Ripoti mbili zimeelezea matumizi ya dawa hii kwenye ujauzito.Licha ya kuwa kuna taarifa chache zinazoruhusu wa madhara ya dawa hii kwenye ujauzito,dawa zingine jamii ya carbapenem zinaonekana kuwa salama kwenyeujauzito wa kuanzia wiki 28 za ujauzito na kuendelea na huenda pia meropenem inaweza kuwa kundi sawa na dawa hii.hatari ya madhara kwa matumizi kabla ya wiki hizi za ujauzito hayafahamiki.

Daptomycin na ujauzito

Daptomycin na ujauzito

Kuna ripoti tatu zinaelezea matumizi ya daptomycin kwenye kipindi cha pili na tatu cha ujauzito. Tafiti za uzazi kwa wanyama zinaonyesha kuweko kwa hatari kidogo, lakini hakuna taariza za kutosha kutoka kwa binadamu hivyo kuzuia kufanya uchuguzi wa madhara ya dawa hii kwa kichanga tumboni.Hata hivyo antibiotic nyingi zenye uzito mkubwa huwekwa kwenye kundi la hatari kidogo kwenye ujauzito, hivyo isisitishwe kwa sababu ya ujauzito.

Clavulanate Potassium

Clavulanate Potassium

Tafiti nyingi zimeelezea matumizi ya amoxicillin na potassium clavulanate kutibu maambukizi mbalimbali kwa mama mjamzito. Tafiti nyingi zimeonyesha kutokuwepo kwa madhara kwa kijusi na mtoto anayezaliwa. Hata hivyo tafiti moja imeripoti kuwa kuna mahusiano kati ya matumizi ya dawa hii na kutokea kwa ugonjwa wa necrotizing enterocolitis (NEC)kwa vichanga wanaozaliwa.

Clindamycin na ujauzito

Clindamycin na ujauzito

Hakuna ushahidi kutoka wa kisayansi unaohusianisha dawa hii na kutokea kwa visa vya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga

Chloramphenicol na ujauzito

Chloramphenicol na ujauzito

Ingawa ya kuwa si sumu kwa kichanga, chloramphenicol inapaswa kutumika kwa tahadhari. Ripoti moja ilidai kwamba watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito walikuwa wanapata gray syndrome. Ripoti za ziada bado hazijapatikana, hata hivyo inafahamika vema kuwa, vichanga wanaotumia dawa hii kwa dozi kubwa huweza kupata gray syndrome. Kwa sababu hii, baadhi ya watafiti wanashauri dawa hii isiwe kwenye kundi la dawa zinazopatana na ujauzito.

Kanamycin na ujauzito

Kanamycin na ujauzito

Dawa hiii imeripotiwa kuwa sumu kwenye masikio, hata hivyo hakuna ripoti ya kusababisha madhaifu mengine ya kiumbaji ya maungo mbalimbali ya mwili kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.

Gentamicin na ujauzito

Gentamicin na ujauzito

Gentamicin hutumika sana kwenye matibabu ya magonjwa kwa mama mjamzito.Uhusiano wa dawa hii na kutokea kwa madhaifu ya kiuumbaji hayajaonekana bado licha ya kutumika sana

Paromomycin na ujauzito

Paromomycin na ujauzito

Paromomycin ni dawa jamii ya aminoglycoside inayotumika kutibu ugonjwa wat umbo wa amebiasis. Hakuna ripoti iliyoandikwa kuzungumzia mahusiano ya dawa hii na madhaifu ya kiuumbaji. Dawa hii hufyonzwa kidogo sana tumboni na inayoingia kwenye damu hutolewa yote kwa asilimia 100 kwenye haja kubwa bila kufanyiwa umetaboli, hivyo hakuna kiasi cha dawa au kuna kiasi kidogo kabisa huweza kuingia kwa kijusi tumboni.

Metronidazole na ujauzito

Metronidazole na ujauzito

Ingawa hitimisho la baadhi ya ripoti zilizowasili zinachanganya kuhusu usalama wa metronidazole kwenye ujauzito, machapisho mbalimbali yanaonyesha dawa hii ina hatari kidogo ya kusababisha madhaifu ya maumbile kwa kijusi tumboni. Kwa sasa pia ni vigumu kuchunguza madai kuhusu hatari ya metronidazole kusababisha saratani kwa watoto, kwa sababu ya uchache wa watoto wanaozaliwa na saratani na uhaba wa taarifa hizo kutoka wamama waliotumia dawa hii, na kukosekana kwa tafiti zilizoangalia matumizi ya metronidazole na mchango wa sababu za kimazingira ambazo zinaweza changia kwa pamoja kusababisha saratani kwa watoto. Mzalishaji wa dawa anasema kwamba dawa hii haipaswi kutumika kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito kutibu ugonjwa wa trichomoniasis au vaginosis iliyosababishwa na bakteria, hata hivyo anashauri kutumika kwenye kipindi cha pili (2) na tatu(3) cha ujauzito kutibu magonjwa hayo. Endapo itahitajika kwa kazi nyingine, dawa hii itumike pale tu endapo hakuna dawa nyingine mbadala wake.

Dexamethasone na ujauzito

Dexamethasone na ujauzito

Dexamethasone ni dawa jamii ya corticosteroid yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kama betamethasone.Matumizi ya dawa hii kipindi cha kwanza cha ujauzito huwa na madhara ya kusababisha mdomo sungura kwa data chache zilizopatikana kwa wamama wanaotumia dawa hii. Hata hivyo matumizi ya dawa hii yafanyike endapo faida kwa mama ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kutokea kwa mtoto.

Dexchlorpheniramine na ujauzito

Dexchlorpheniramine na ujauzito

Kwa ujumla dawa jamii ya antihistamine zimeonekana kutokuwa na hatari ya kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii. Hata hivyo matumizi kwa wajawazito karibia na kujifungua kabla ya wakati kufika huhusiana na kusababisha fibroplasia ya retrolental

Dimenhydrinate na ujauzito

Dimenhydrinate na ujauzito

Kwa ujumla dawa jamii ya antihistamine zimeonekana kutokuwa na hatari ya kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii. Hata hivyo matumizi kwa wajawazito karibia na kujifungua kabla ya wakati kufika huhusiana na kusababisha fibroplasia ya retrolental.

bottom of page