top of page

Mafuta ya Omega 3 hayatengenezwi mwilini!

Imeandikwa namadaktari wa uly clinic

Utangulizi

Mafuta ya Omega-3 ni mafuta muhimu sana mwilini kwani huwa na kazi mbalimbali, mafuta haya huwa hayatengenezwi mwilini hivo tunahitaji kuyapata kwenye chakula tunachokula kila siku au kwenye mafuta yaliyotengenezwa kutoka kwenye vyakula vyenye mafuta haya. Mafuta ya Omega 3 huhusika kusimamia suala zima la ugandishaji damu na kujenga kuta za chembe hai za ubongo

Mafuta haya tena yanafaida nyingi mwilini kama kukinga mwili na maradhi ya magonjwa ya moyo na Kiharusi. Utafiti mpya umeonehsa kwamaba mafuta haya yana  umuhimu wa kupambana na kukinga dhidi ya  magonjwa mengi kama saratani, Ugonjwa wa michomo kwenye tumbo(inflammatory bowel disease), Autoimmune disease kama ugonjwa wa rheumatoid arhtritis na lupus

Mafuta ya omega 3 hupatikana kwenye vyakula gani?

Mafuta haya huweza kupatikana katika vyakula vifuatavyo

  • samaki wa waishio katika maji baridi kama sangara huwa na kiasi kikubwa sana cha mafuta haya

  • Maharage ya soya, Nazi,

  • Mboga za majani kama Spinach, kabegi, chainizi n.k

  • Mchanganyiko wa matunda yenye rangi ya kijani kizungu green salad

Toleo la 3

Imeboreshwa 8/2/2019

bottom of page