Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Jumatano, 7 Julai 2021

Amibiasis kwa watoto
Mara nyingi kimelea cha amiba anaweza kuingia kwenye mfumo wa umeng’enyaji chakula na kuishi bila kusababisha dalili yoyote ile, isipokuwa akivamia kuta za utumbo mpana. Uvamizi kwenye utumbo mpana husababisha dalili za kuharisha damu, maumivu na kunyonga kwa tumbo, kichefuchefu, kukosa hamu ya kula na homa. Amiba anaweza safari kwenda pia kwendaogani nyingine ndani ya mwili na kusababisha maambukizi kwenye Ini, mapafu moyo na ubongo.
Dalili za amibiasis kwa watoto
Watoto wenye maambukizi ya amiba huwa hawaonyesi dalili au kuwa na dalili kizsi tu. Baadhi ya watoto hupata dalili ndani ya siku au wiki chache, lakini wapo baadhi pia hupata baada ya miezi kadhaa kupita.
Endapo dalili zitatokea zinajumuisha;
Maumivu ya tumbo yanayoanza taratibu na kuambatana na choo kilaini au cha majimaji
Kunyonga kwa tumbo
Kichefuchefu
Kupoteza hamu ya kula
Haja kubwa yenye kamasi
Dalili zingine zinazoweza kutokea kwa baadhi ya watoto ni;
Homa
Haja kubwa yenye damu
Wakati gani uwasiliane na daktari haraka endapo mwanao ana dalili za amibiasis?
Wasiliana na daktari haraka kwa matibabu endapo mwanao ana dalili zifuatazo;
Kuharisha damu au kupata kinyesi chenye kamasi
Maumivu ya tumbo ( ataonekana kwa kukunja sura au kujikunja mwili seemu ya tumbo) kwa mtoto mkubwa atasema kuwa ana maumivu ya tumbo
Kuchemka
Kujaa kwa tumbo
Maumivu sehemu ya kulia chini ya mbavu
Vihatarishi vya maambukizi ya amiba kwa watoto
Maambukizi ya amiba hutokea mara nyingi kwenye maeneo yasiyo na mfumo mzuri wa utunzaji wa maji taka. Maeneo hayo hujumuisha maeneo yenye yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na yasiyo na utunzaji mzuri wa kinyesi cha binadamu. Hii ndio maana ugonjwa huu hutokea katika nchi masikini au zile zinazoendelea duniani. Mfano endapo shimo la choo limechimbwa karibu na vyanzo vya maji, maji yenye vimela kutoka kwenye kinyesi hupenya kuingia kwenye vyanzo vya maji iwe kisima, mto au chanzo chochote kilicho karibu na makazi ya watu. kisima, Maji haya yakitumiwa bila kutibiwa, hupelekea kutokea kwa maambukizi ya kujirudia rudia.
Endapo mtu atajisaidia karibu na chanzo cha maji au kumwaga kinyesi kwenye maji au kutumia kinyesi cha binadamu kama mbolea, au kumwagilia maji yaliyo na kinyesi kwenye mazao, hupelekea kusambaza kwa maambukizi kwa kula vyakula hivyo.
Mtoto kula mchanga au udongo wenye mayai ya kimelea pia huwa chanzo kingine cha kupata maambukizi kwa watoto wanaoanza kutambaa.
Namna gani mtoto anapata maambukizi ya amiba?
Mtoto anaweza pata maambukizi ya amiba kwa kunywa maji au kula chakula kilichochanganyika na kinyesi chenye vimelea. Chakula kinaweza kuchanganyika na vimelea kwa njia mbalimbali kama vile;
Kuandaliwa chakula na mtu mwenye maambukizi pasipo kufanya usafi wa mikono kwa maji salama ( mtoto kula tunda lililoshikwa na mwenye maambukizi, au mtoto kula vidole vya mkono ulioshikwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hajanawa mikono kwa maji safi baada ya kujisadia.
Kutumia vyombo vya mtu mwenye maambukizi, mfano kutumia bilauri moja ya kunywea maji, au vyombo vilivyoshikwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hazingatii usafi wa mikono
Kutumia maji ya kunywa yasiyo salama, mfano yaliyochotwa mtoni au ambayo hayajachemshwa
Kula matunda yaliyosafishwa kwa maji yasiyo salama
Kunawa mikono kwa maji yasiyo salama
Kula udongo au mchanga wenye mayai ya kimelea cha amiba
Vipimo vya amiba kwa watoto
Baada ya kuchukuliwa historia ya dalili za mtoto na kufanyiwa vipimo vya awali vya mwili, daktari ataagiza mtoto afanyiwe vipimo mbalimbali. Kinyesi kitakusanywa kisha kupelekwa maabara kwa vipimo vya;
Kuchunguza uwepo wa amiba kwa hadubini
Kupima antijeni za amiba kwenye kinyesi
Matibabu ya amibiasis kwa watoto
Matibabu ya amibiasis hulenga katika kuondoa maambukizi na kuthibiti dalili zilizojitokeza. Dawa inayotumika sana kwa watoto ni metronidazole au Tinidazo (kwa watoto zaidi ya miaka 3) au dawa zingine zinazotumika kwa kuunganishwa zaidi ya moja kama;
Paromomycin (Humatin®)
Dehydroemetine
Tetracycline
Diloxanide Furoate
Diquinol
Matibabu mengine hutegemea hali ya mtoto, endapo mtoto anahara, utashauriwa kumpa maji ya kutosha au maji ya oral (ORS). Endapo mtoto ameharisha sana pia na ana hali mbaya anaweza kuongezewa maji hospitali.
Inachukua muda gani kupona amibiasis baada ya kuanza kutumia dawa?
Kwa kawaida inachukua kati ya wiki 1 hadi 3 kwa maambukizi kuisha kabisa mwilini bada ya kuanza kutumia dawa. Hata hivyo dalili zinaweza kupotea kabia kati ya wiki ya kwanza na pili tangia mtoto amenaz akutumia dawa. Amibiasis nje ya tumbo huweza kuchukua muda mrefu kupona.
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na amibiasis
Sio kila dalili za amiba humaanisha amibiasis, hii inafanya umuhimu wa kuonana na daktari kwa uchunguzi na vipimo kabla ya kuanza kutumia dawa. Magonjwa mengine yanayofanana sana dalili na maambukizi ya amiba kwa watoto ni;
Shigellosis
Salmonellosis
Campylobacteriosis
Homa ya enterohemorrhagic Escherichia coli,
Hata hivyo utofauti wa amibiasis na magonjwa haya ni dalili, dalili za magonjwa hayo huanza haraka zaidi ukiliganisha na amibiasis.
Madhara ya amibiasis kwa watoto
Madhara yafuatayo yanaweza kutokea endapo mtoto hatapata matibabu mapema. Inakadiliwa asilimi 7 hadi 30 ya wagonjwa wanawez akupta madhara haya wasipopata matibabu.
Intusasepsheni
Kutoboka kwa utumbo
Peritonaitiz
Kuoza kwa utumbo ( NEC)
Namna ya kumkinga mtoto kupata amibiasisi
Ili kumkinga mtoto na maaambukizi ya amiba, unaweza fanya mambo yafuatayo;
Tenge vyombo vya mtoto na watu wazima mfano vyombo vya kuogea, vya kunywea maji n.k
Nawa mikono wa maji safi baada ya kutoka chooni
Safisha mboga za majani na matunda kwa maji safi kabla ya kuliwa au kupika. Tumia maji salama yaliyotiwa iodine au chlorine
Jenga choo mbali na vyanzo vya maji
Mfundishe mtoto kutokula mchanga au vidole bila kunawa. Au tumia viziba mdomo ili asile mikono akishika chini
Matibabu ya dawa asilia
Kuna mambo na dawa asilia unaweza kutumia kwa matibabu ya amibiasisi kwa watoto, dawa hizo zinapatikana kwa madaktari wa tiba asilia na zingine zinauzwa internet. Matibabu hayo huweza kuwa;
Maji ya nazi
Maziwa yaliyotolewa siagi baada ya kuchacha
Vinega ya tufaa
Chai nyeusi
Vitunguu swaumu
Kusoma namna gani ya kutumia na vinavyofanya kazi, ingia kwenye makala zingine za dawa asilia ya amiba.
Majina mengine ya maambukizi ya amibiasis kwa watoto
Baadhi ya watu hutumia majina yafuatayo kumaanisha maambukizi ya amibiasisi kwa watoto
Amiba kwa watoto
Ugonjwa wa amoeba kwa watoto
Ugonjwa wa amoebiasis kwa watoto
Matibabu ya amiba kwa watoto