top of page

Mwandishi:

Mhhariri

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt. Peter A, MD

Jumanne, 28 Desemba 2021

Fangasi ukeni

Fangasi ukeni

Maambukizi ya candida ni kisababishi kikuu cha muwasho kwenye maeneo ya uke na kutoka kwa uchafu mweupe kama maziwa ukeni. Tatizo hili huambatana na michomo sehemu za siri inayosababishwa na maambukizi ya fangasi jamii ya candida. Michomo hii hudhihilishwa kwa kubadilika rangi maeneo hayo(kuwa mekundu) kuwashwa.

​

Katika sehemu hii tunazungumzia kuhusu dalili, kutambua tatizo na matibabu

​

Epidemiolojia


Tatizo hili huwa la pili katika kusababisha muwasho sehemu za siri baada ya maambukizi ya bakteria na hutokea sawa kwa wanawake kipindi ambaco wameshabalehe

​

Vihatarishi huwa pamoja na


  • Ugonjwa wa kisukari

  • Matumizi ya dawa za antbiotiki(ambazo huua bakteria walizi wa uke na kuwapa nafasi fangasi kukua)

  • Kuongezeka kwa homoni estrogeni kwenye damu, mfano watu wanaotumia dawa za uzazi wa mpango hupata sana fangasi kwa sababu dawa hizo huwa na homoni ya estrogeni

  • Kushuka kwa kinga mwilini, kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kinga kushuka kama vile, matumizi ya dawa za kushusha kinga mfano dawa jamii ya corticosteroid, chemotherapy, tiba mionzi, ugonjwa wa kisukari na VVU n.k

Kuna baadhi ya vitu au tabia mbalimbali zinazoweza kuleta au kusababisha maambukizi haya ikiwa pamoja na;


  • Matumizi ya vifaa vya uzazi wa mpango, mfano sponji ukeni, kizuizi, au kizuia mimba kinachowekwa ndani ya mfuko wa kizazi.

  • Tabia ya kujamiiana- tatizo la fungasi ukeni kwa kawaida limekuwa likijulikana kuwa sio gonjwa la zinaa kwa sababu hutokea hata kwa wale wasio jamiiana. Hii imekuwa hivyo lakini haimaanishi tatizo hili huwezi kupata kwa njia ya kujamiiana. Endapo mwanamke atakutana na mwanaume mwenye tatizo hili ni rahisi kupata kwa njia hiyo. Tafiti zinaonyesha kuwa mwanamke mwenye mpenzi ambaye anafangas ana uwezekano mara 4 zaidi ya kupata maambukizi hayo ukilinganisha na mwanamke ambaye hana mwanaume mwenye fangasi.

Dalili


Muwasho sehemu za siri huwa dalili tawala kwenye mgonjwa mwenye tatizo la fangasi ukeni

​

Dalili zingine ni

​

  • Kuhisi kuungua sehemu za uke

  • Kubadilika kwa rangi sehemu za siri

  • Kuvimba kwa mashavu ya uke

  • Kutokwa na uchafu mweupe mzito kama maziwa mgando unaonata kwenye kuta za uke unaokuwa na harufu kiasi au bila harufu kabisa au kutokuwa na uchafu kabisa au kutokwa na uchafu mwepesi, majimaji na unaoshindwa kutofautishwa na majimaji mengine yanayoweza sababishwa na magonjwa ya zinaa

  • Kuchubuka kwa ngozi au mipasuko ya uke

  • Dalili pia zinaweza ambatana na maumivu wakati wa kukojoa haswa kwenye mashavu na uke, maumivu wakati wa kujamiiana.

  • Dalili huwa kali Zaidi wiki chache kabla ya kuona hedhi

Uchunguzi

​

Aina ya uchunguzi

​

Ukienda hospitali unaweza fanyiwa vipimo vifuatavyo

​

Kuchukuliwa majimaji kutokakwenye uke kwa kutumia kijiti kisha kupima vitu mbalimbali ikiwemo hali ya aside ya majimaji hayo, nakuchungulia kwenye hadubidi majimaji ili kuona kama kuna fangasi na aina ya fangasi. Kipimo hiki kinaweza tofautisha kama una fangasi au aina nyingine ya vimelea wanaosababisha kuwashwa ukeni

​

Kipimo cha kuotesha fungasi

Majimaji yanayochukuliwa huwekwa kwenye vifaa maalumu ili kuotesha vimelea walio kwenye majimaji hayo, hili husaidia kujua aina ya vimelea waliopo kwenye majimaji. Kipimo huchukua mda mrefu. Kipimo hiki si kila mtu hufanyiwa, ni watu wale tu wenye maambukizi sugu na ambayo hayasikii dawa

​

Vipimo vingine

​

Vipimo vya kuangalia Vinasaba vya vimelea

​​

Vitu/Sababu gani zingine zinaweza sababisha muwasho sehemu za siri?

​

  • Kuwa na mwili wenye mwitikio rahisi(aleji au mzio)- Hasa kwenye kemikali, mafuta, dawa au sabuni n.k

  • Magonjwa ya zinaa

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

28 Desemba 2021, 20:00:02

Rejea za mada hii:

1. Ferri FF. Vaginitis, fungal. In: Ferri's Clinical Advisor 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.12.2021

2. Lobo RA, et al. Genital tract infections: Vulva, vagina, cervix, toxic shock syndrome, endometritis, and salpingitis. In: Comprehensive Gynecology. 7th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2017. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.12.2021

3. Cohen J, et al., eds. Vaginitis, vulvitis, cervicitis, and cutaneous vulval lesions. In: Infectious Diseases. 4th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2017. https://clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.12.2021

4. Bope ET, et al. Vulvovaginitis. In: Conn's Current Therapy 2018. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.12.2021

5. Vaginal yeast infections. Office on Women's Health. https://www.womenshealth.gov/a-z-topics/vaginal-yeast-infections. Imechukuliwa 28.12.2021

bottom of page