Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 28 Oktoba 2021

Kaposi's sarcoma
Saratani ya Kaposi (Kaposi's sarcoma, KS) ilielezewa kwa mara ya kwanza mwaka 1872 na mtaalamu wa ngozi wa Hungarian anayeitwa, Moritz Kaposi.
Saratani hii huathiri katika chembe hai za ukuta wa ndani wa mishipa ya damu. Saratani ya kaposis huwa na hatua tofauti kuanzia kwenye ngozi mpaka kuhusisha viungo vya ndani ya mwili.
Dalili za awali za saratani ya Kaposis sarcoma ni muonekano wa mabaka mekundu au zambarau juu ya ngozi. kisha mabaka haya hukua na kutengeneza vimbe kama vinundu. Inaweza kuleta uharibifu kuanzia kwenye ngozi laini ya midomo na viungo vya ndani ya mwili.
Aina
Aina za saratani ya kaposis ni;
Kaposisi ya UKIMWI
Kaposisi ya kushuka kwa kinga ya mwili
Kaposis ya Classic au sproadic
Kaposisi ya Waafrika
Saratani ya kaosisi inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI, ukilinganisha na aina zingine huwa na madhara ya haraka na mabaya. Saratani aina hii inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI hutokea mara nyingi ukilinganisha na zingine
Dalili za saratani ya kaposis
Saratani ya Kaposisi huathiri ngozi, ngozi laini ya midomo, mitoki, na viungo vya ndani ya mwili pia. Wagonjwa wengi hupata dalili za kwenye ngozi kama kwenye picha hapo pembeni. Saratani ya kaposis huleta uharibifu wa viungo vya ndani vya mwili, ambapo inaweza kusababisha aina mbalimbali za dalili, ikitegemea kiungo gani kimeathiliwa.
Dalili zingine
Kushindwa kupumua-kupumua kwa shida-kama imeathiri mapafu
Fizi kutoka damu
Maumivu ya tumbo
Uvimbe katika miguu
Dalili zingine
Madhara kwenye ngozi huweza kutokea hasa katika maeneo ya miguuni, kichwa na shingo.
Vinundu ama mapele ya saratani ya kaposis huweza kuwa ya saizi ya kati ama makubwa
Karibia vipele vyote huhisiwa kama vikishikwa na huwa haviwashi
Upele na mabaka yanaweza kuwa na sentimeta chache hadi nyingi
Upele ama vinundu huwa na rangi ya brown, zambarau, nyekundu, wakati mwingine ni vigumu kutambua kutokana na rangi ya ngozi ya mtu
Vipele hivi hutokea sana kwenye ngozi laini (mdomo, fizi, macho)
Dalili kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Saratani hii ikihusisha viungo vya mfumo wa chakula wakati mwingi vipele hivyo huwa havitoi dalili za kuonekana nje ya mwili, kama dalili zikionekana basi ugonjwa unakuwa umekua sana na husababisha dalili zifuatazo;
Kushindwa kumeza chakula, ama chakula kushindwa kufika tumboni
Kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo
Kutapika damu, kuonekana kwa damu kwenye haja kubwa ama kupata choo cheusi
Kuziba kwa matumbo ama utumbo
Dalili za kwenye mapafu
Dalili za kaposis ya kwenye mapafu ni;
Kukohoa
Kupumua kwa shida
Kukohoa damu
Maumivu ya kifua
Matibabu
Matibabu ya kukinga madhara ya VVU kwa kutumia dawa za ARV ni moja ya mbinu za kutibu saratani ya kaposis. Dawa za ARV hutumika katika Matibabu ya saratani ya kaposis isiyohusisha viungo vya ndani vya mwili. Kama mtu ana saratani hii katika viungo vya ndani ya mwili, matumizi ya dawa zinazoitwa chemotherapy huongezewa katika matibabu yake
Matibabu yafuatayo yanaweza kutumika kuongeza ubora wa maisha ya mgonjwa mwenye saratani ya kaposis ambayo imeharibu ngozi na kuondoa urembo
Matibabu ya mionzi
Matibabu ya kukata vipele kwa njia ya cryotherapy
Kukata vipele kwa kutumia mionzi ya Laser
Upasuaji wa kukata vipele
Matumiz ya dawa za saratani za vinka alkaloid
Matumizi ya dawa za kupaka aina ya retinoids