Mwandishi:
Mhhariri
Dkt Benjamin L, MD
Dkt. David R, MD
Ijumaa, 17 Desemba 2021
Kusinyaa kwa arteri
Kusinyaa kwa mishipa ya damu ya arteri hufahamika pia kama atheroklerosis ni ugonjwa unaodhuru mishipa mikubwa ya damu na ni kisababishi cha awali cha magonjwa ya moyo na kiharusi. Katika nchi zilizoendelea, husabbaisha asilimia 50 ya vifo vyote, na katika nchi zinazoendelea ni tatizo lonaloongezeka kila kukicha kutokana na kubadilika kwa mtindo wa maisha.
Epidemiolojia inaonyesha kuwa kuna vitu mbalimbali vinavyohusika kusababisha tatizo hili ikiwa pamoja na sababu za kualiwa na za kimazingira.
Maendeleo ya kisayansi katika tiba tambuzi, yamewezesha kufahamu namna ugonjwa huu unavyotokea katika hatua ya kimolekyuli. Vipimo vinaonyesha kuwa kuna mabadiliko hutokea katika umetabolizimu wa lehemu ambao ukiunganika na vihatarishi vingine, hupelekea kuganda kwa mafuta ndani ya mishipa ya damu na hivyo kupelekea mishipa hiyo kusinyaa.
Kwa sasa inafahamika wazi kuwa, kusinyaa kwa mishipa ya damu sio tu kwamba hakuzuiliki kwa kuwa ni ugonjwa endelevu wa uchakavu wa mishipa ya damu kutokana na uzee, huweza kubadilika kutoka ugonjwa sugu kuwa ugonjwa mkali kutokana na kuziba kwa mishipa ya damu na mabonge ya mafuta yaliyonyofoka kutoka kwenye damu iliyoganda.
Visababishi
Visababishi vya kijeni
Kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu za LDL/VLDL
Kupungua kwa lehemu ya HDL kwenye damu
Ongezeko kubwa la mafuta lipoprotein(a)
Ongezeko kubwa la shinikizo la damu
Ongezeko kubwa la kiwango cha homocysteine
Kuwa na historia kwenye familia ya ugonjwa huu
Kisukari na obeziti
Ongezeko kubwa la vigandisha damu
Msongo wa mawazo na matatizo mengine ya kitabia
Kues mwanaume chini ya miaka 60
Magonjwa ya michomo ys kudhuru Zaidi ya mfumo mmoja kama baridi yabisi
Sindromu ya kimetaboliki
Sababu za kimazingira
Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi au lehemu nyingi
Kuvuta sigara
Kiwango kidogo cha viuaji sumu kwenye damu
Kutofanya mazoezi
Maambukizi ya magonjwa kama bakteria Chlamydia pneumoniae.
Utambuzi
Utambuzi wa kuingiza mrija kwenye mishipa ya damu ni njia pekee inayotumika kutambua tatizo la kusinyaa kwa mishipa ya damu. Hata hivyo huwa na hatari kubwa kutokana na kusababisha kunyofoka kwa mabonge ya mafuta yaliyoganda.
Vipimo vingine ambavyo ni salama vinapaswa kugunduliwa haraka ili kuongeza ufanisi katika utambuzi.
Vipimo vingine ambavyo vinaweza kuwa na majibu mazuri ni kipimo cha;
C-reactive protein
Ultrasound
Computerized tomography
Vpimo hivyo ni vya muhimu lakini huwa na vipingamizi vake pia.
Matibabu
Kwa sababu kisaabishi cha kusinyaa kwa mishipa ya damu huwa vingi, matibabu hutegemea ugonjwa husika.
Dawa zinazotumika huwa katika makundi yafuatayo;
Dawa za kuzuia kukusanyika kwa chembe sahani kama vile Aspirin, clopidogrel, ticlopidine, na dipyridamole.
Dawa za kuzuia ugandaji wa damu kama vile warfarin na heparin
Dawa za kupunguza lehemu kwenye damu kama vile simvastatin, atorvastatin, na pravastatin.
Dawa jamii ya sequestrants kama vile colesevelam, cholestyramine na colestipol.
Dawa zingine ni kama nicotinic acid
Dawa za shinikizo la damu. Hutumika kudhibiti shinikizo la damu kwa mgonjwa mwenye tatizo hili.
Dawa asili
Kuna baadhi ya dawa asili zinazosemekana kuzuia na kutibu tatizo la mishipa ya damu kuzinyaa. Unapaswa kuwasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa hizo.
Madhara
Kusinyaa kwa mishipa ya damu huweza sababisha madhara ya fuatayo
Kiharusi
Mshituko wa moyo
Kuganda kwa damu ndani ya mishipa ya arteri
Anurizimu
Kinga
Kinga inaweza kufanyika kwa
Kutambua tatizo kabla halijatokea
Kufanya vipimo vya utambuzi wa kiwango cha LDL, HDL na shinikizo la juu la damu imekuwa ikitumiwa kitambua watu wenye hatari ya kupata ugonjwa huu.
Vipimo vingine vya kutambua jeni zinazohusika na ugonjwa huu vinaweza kuwa vya faida pia kutambua ugonjwa kabla haujatokea au kuleta madhara.
Kubadili mtindo wa maisha
Kubadili mtindo wa maisha huhusisha;
Kuacha kuvuta sigara
Kupunguza kiasi cha lehemu mbaya kwenye damu
Kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu
Kufanya mazoezi
Kula vema kama vile matunda na mboga za majani kwa wingi Zaidi
Kudhibiti shinikizo la damu
Majina mengine ya Makala hii
Kupungua kipenyo cha mishipa ya arteri
Kunenepa kwa kuta za mishipa ya arteri
Kukakamaa kwa ya arteri