Mwandishi:
Mhhariri
Dr. SAlome Adolf, MD
Dkt. Sospeter M, MD
Jumamosi, 16 Aprili 2022

Maji kidogo kwenye chupa ya uzazi
Maji kidogo kwenye chupa ya uzazi humaanisha kuwa na kiwango cha maji cha chini ya kiwango kawaida. Kiwango hiki hugundulika kwa kufanya kipimo cha kutumia picha ya mionzi ya sauti kinachofahamika kama AFI.
Kuna maana nne (4) za maji kidogo kwenye chupa ya uzazi, hata hivyo kuna ugumu ipi ni maana nzuri ya kuelezea kiwango hiki. Kiwango cha maji kwenye chupa ya uzazi kinaweza kuelezewa kwa kipimo cha kina cha maji chenye kifupisho ya AFI. AFI chini ya sentimita 5 au vipimo viwili vya kina kirefu tumboni vikiwa chini ya sentimita 2 au vizio viwili chini ya sentimita za ujazo 15 huashiria kuwa na kiwango kidogo cha maji kwenye chupa ya uzazi. Kuelewa zaidi kuhusu AFI soma makala ya kipimo cha maji kwenye chupa ya uzazi (AFI).
Maji kwenye chupa ya uzazi huzalishwa wapi?
Maji kwenye chupa ya uzazi hutengenezwa awali kutoka kwenye majimaji ya damu ya mama yanayopita na kuingia kwenye chupa ya uzazi. Mara figo za mtoto zinapoanza kufanya kazi, mkojo wa mtoto huchangia katika kuongeza maji kwenye chupa ya uzazi. mkojo wa mtoto na majimaji yanayozalishwa kwenye mapafu.
Kazi ya maji ya chupa ya uzazi
Huzuia mtoto kujeruhiwa kutokana na mgandamizo kwenye tumbo la mama
Huzuia mgaandamizo kwenye kitovu cha mtoto
Huzuia maambukizi ya vimelea kwa mtoto
Hutunza maji na virutubisho vya ziada kwa ajili ya mtoto
Nini husababisha maji kidogo kwenye chupa ya uzazi?
Matatizo kwenye vinasaba/madhaifu ya kiumbaji ( kama madhaifu ya figo na mirija ya mkojo)
Mtoto kukosa hewa ya oksjeni (hupelekea kiwango kidogo cha plazma kwa mtoto na kupungua kwa kiwango cha mkojo)
Ujauzito kupitiliza wiki 40 (mtoto hunywa maji mengi na uzalishaji hupungua/kusimama)
Mama kuishiwa maji (kutokana na kutapika sana, kuhara n.k)
Kupasuka kwa chupa ya uzazi
Magonjwa yanayodhuru kutovu cha mtoto( mfano kifafa cha mimba, shinikizo la damu linaloenelekea kifafa cha mimba, shinikizo la juu la damu lililo sugu, kunyofoka kwa kondo la nyuma, magonjwa ya kuganda kwa damu au matatizo mengine ya kwenye ujauzito)
Sababu zisizofahamika
Madhara ya maji kidogo kwenye chupa ya uzazi
​
Madhara ya maji kidogo hutegemea tatizo limetokea kipindi gani cha ujauzito na kiasi cha maji kilichobakia.
Kufa kwa mtoto
Kudumaa kwa mtoto tumboni
Kukakamaa kwa miguu na mikono ya mtoto
Kuchelewa au kutokomaa vema kwa mapafu ya mtoto
Mtoto kushindwa kuchuka wakati wa kujifungua
Kama tatizo la maji kidogo kwenye chupa ya uzazi limegundulika kwenye ujauzito uliotimiza umri, hii huwa sababu ya kujifungua haraka. Kuna ushahidi unaosema kwamba maji kidogo kwa ujauzito uliopitiliza umri huweza kusababisha mapigo ya moyo ya mtoto kuwa ya kutoridhisha na kujifungua kwa upasuaji. Hata hivyo hakuna tofauti kwa mtoto aliyezaliwa na mama aliye na maji kidogo au mengi kwenye ujauzito uliopitiliza umri.
Matibabu
Matibabu huhusisha;
Vipimo vya mara kwa mara vya kiwango cha maji ndani ya chupa ya uzazi
Kama mtoto hana madhaifu ya kiuumbaji, inashauriwa kujifungua kwa njia itakayofaa
Kupewa baadhi ya dawa
Kuingiziwa maji kwenye chupa ya uzazi kupitia tumbo la mama wakati wa kipindi cha pili cha ujauzito
Kama ujauzito umepitiliza umri, mama anashauriwa kujifungua kwa kuanzishiwa uchungu au kwa upasuaji
Mama kupumzika na kunywa maji au kuongezewa maji kwa njia ya mishipa ili kuongeza kiwango cha maji kwenye chupa ya uzazi husaidia pia katika kuongeza kiwango kidogo cha maji kwenye chupa ya uzazi