Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter M, MD
Jumatatu, 8 Novemba 2021

Matege
Matege husababishwa na hali ya mifupa kuwa laini na dhaifu, hali hii husababishwa na kuwepo kwa upungufu endelevu wa madini ya vitamini D kwa watoto.
​
Vitamini D huongeza ufyonzaji wa madini ya kalisium na fosforazi kutoka kwenye mfumo wa chakula-(utumbo) na kuingia kwenye damu. Upungufu wa vitamini D husababisha uwiano wa madini ya kalisium na fosforazi kuharibika na hivyo mifupa kuwa dhaifu na kupinda na hivyo kuleta mwonekano wa matege
Kama upungufu wa vitamini D ama kalisiumu utasababisha matege, kwa kuongeza vitamin D ama Madini ya kalisium kwenye chakula huweza kunaweza kurekebisha tatizo la matege kwa mwanao. Matege ya kuzaliwa nayo( kutokana na kurithi jeni za matege) huwa ni vigumu kutibika na huhitaji matibabu ya ziada.
Baadhi ya matatizo ya mifupa kutokana na matege huweza kurekebishwa kwa njia ya upasuaji.
Dalili
Dalili za tatizo la matege huwa pamoja ni;
Kuchelewa kukua
Maumivu ya utu wa mgongo, kiuno na miguu
Misuli kuwa dhaifu
Kwa sababu tatizo la matege huathiri chembe za ukuaji wa mifupa, mwisho wake husababisha matatizo ya mifupa kama
Kupinda kwa miguu kuwa kama upinde wa mvua
Viganja na magoti kuwa vinene
Mifupa ya kwenye maeneo ya chuchu kutangulia mbele zaidi(kuwa na mwonekano wa kifua cha njiwa)
​
Visababishi
Mwili wako unahitaji vitamin D ili kufyonza madini ya kalisiumu na phosphorus kwenye chakula kinachoingia tumboni. Tatizo la Matege huweza kutokea endapo mwanao anakosa kiwango cha kutosha cha vitamini D au mwili wake unashindwa kutumia vema vitamin hii kutokana na matatizo katika chembe hai.
Unaweza kupata vitamin D kutokana na
Mwanga wa jua- ngozi huwa na uwezo wa kuzalisha vitamin D endapo itaanikwa kwenye jua haswa lile la asubuhi. Watoto walio kwenye nchi zilizoendelea hukaa kwa kiwango kidongo kwenye mwanga wa jua, na pia hukaa kwenye nyumba zenye vioo ambavyo haviruhusu kupitishwa kwa mwanga wa jua na hivyo kutopigwa na mwanga wa jua na kukosa vitamin D.
Chakula
Mafuta ya samaki, kiini cha mayai. Baadhi ya vyakula siku hizi vimeongezewa madini ya vitamini D kama vile maziwa, vyakula vya nafaka na vinywaji vya matunda. Watoto ambao hawapati vyakula hivi hupata tatizo la matege
Tatizo la ufyonzaji
​
Baadhi ya watoto wamezaliwa na tatizo la kiafya linalo zuia ufyonzaji wa vitamini D kama vile
Ugonjwa wa celiac
Ugonjwa wa infamatori bawel
Ugonjwa wa sistik faibrosis
Vihatarishi
Umri miezi 3 hadi 36 huwa hatarini kupata tatizo la matege kwa sababu mifupa yao hukua haraka sana
Ngozi nyeusi- ngozi nyeusi huwa haipokei mwanga wa jua vema kuliko ngozi nyeusi hivyo huzalisha vitamin D kwa kiwango kidogo.
Mazingira- watu wanaoishi mazingira ya kaskazini mwa dunia hupata mwanga wa jua kwa kaisi kidogo na hivyo hutengeneza kiwango kidogo cha vitamini D.
Kuzaliwa kabla ya umri- watoto waliozaliwa kabla ya umri au watoto njiti huwa na uwezo mdogo wa kufyonza madini ya vitamina D kutoka kwenye maziwa ya mama
Madawa ya kutibu kifafa- huwa na mwingilino katika utumiaji wa vitamini D kwenye chembe za mwili.
Kunyonya maziwa tu-maziwa ya mama huwa hayana kiwango cha kutosha kuweza kuimarisha mifupa. Watoto wanaonyonya maziwa ya mama tu wanatakiwa kupata matone ya vitamini D.
​
Madhara
Madhara ya matege ni;
Kushindwa kukua
Uti wa mgongo kupinda
Matatizo ya maumbile ya mifupa
Matatizo ya meno
Vipimo na utambuzi
Daktari atamchunguza mwanao kwa kubonyehsa kwa kiasi kwenye mifupa ya mwanao kuangalia udhaifu na atatia umakini kwenye mifupa ya;
Kichwa-utosi wa mtoto unaweza kuchelewa kufunga
Miguu-watoto wagodo huonekana na miguu upinde kiasi, ila watoto wenye upungufu wa vitamini D huwa na upinde unaoonekana sana.
Kifua- huchomoza mbele kama mwonekano wa kifua cha ndege
Magoti na viganja- huwa kubwa kuliko kiasi
Kipimo cha picha ya mionzi ya xray pia huweza kuonyesha udhaifu katika mifupa ya watoto
​
Matibabu
Matibabu ya matege huhusisha
Matibabu ya dawa
Kama vitamini D na Madini ya kalisium. Fuata ushauri wa daktari wako kuhusu matumizi ya dawa hizo
Matibabu ya upasuaji
Kama miguu imepinda kama upinde wa mvua, daktari anaweza kukushauri kutumia viatu ama vazi maalimu linaliweza kunyoosha miguu. Matatizo makubwa ya kupinda miguu huweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji.
Kijikinga na upungufu wa vitamini D
Watoto wengi na vijana wanapata kiasi cha kutosha cha vitamini D kutoka kwenye jua. Vichanga na watoto wadogo kabisa huweza kukosa kiasi cha vitamini D kinachohitajika kwa sababu hawakai kwenye mwanga wa jua
​
Kama ndo hivyo basi hakikisha mwanao anapata kiasi cha kutosha cha vyakula vyenye vitamini D kama mafuta ya samaki, kiini cha yai au vyakula vya kusindikwa kama
Maziwa ya kopo
Maziwa
Kwa sababu maziwa ya binadamu huwa na kiwango kidogo cha vitamini D watoto wote wanaonyonya tu wanahitaji kupata vitamini D kiasi cha 400IU kila siku.