Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
DKt. Salome A, MD, Benjamin L, MD
Jumatatu, 7 Aprili 2025

Mguu farasi

Mguu farasini hali ambayo mtoto hawezi kupinda kanyagio la mguu kuelekea juu zaidi ya kiwango cha kawaida. Hii husababisha mtoto kutembelea vidole na kama hajaanza kusimama, akisimamishwa vidole hugusa sehemu ya kukanyagia badala ya kanyagio zima. Kwa watoto wachanga, mguu farasi unaweza kuwa wa kuzaliwa au wa kupata baada ya kuzaliwa, na unaweza kuathiri ukuaji wa kawaida wa kutembea endapo matibabu yatafanyika mapema. Makala hii imezungumzia kwa undani kuhusu epidemiolojia, visababishi, vihatarishi, vipimo, matibabu, lini kumuona daktari, na tiba ya nyumbani ya mguu farasi kwa watoto.
Epidemiolojia

Mguu farasi kwa kawaida huwa hautokei kama udhaifu wa kujitegemea kwa watoto wachanga kwani mara nyingi huambatana na matatizo mengine kama miguu kifundo au mtindio wa ubongo. Tatizo la mguu kifundo, ambalo mara nyingi huambatana na mguu farasi, hutokea takribani kwa mtoto 1 kati ya 1,000 wanaozaliwa hai duniani.
Visababishi
Vifuatavyo ni visababishi vya mguu farasi;
Matatizo ya kuzaliwa
Mguu kifundo
Misuli ya nyuma ya mguu kuwa mifupi au ngumu
Matatizo ya neva
Mtindio wa ubongo
Mgongo wazi
Madhaifu ya Mifupa na misuli:
Distrofia ya misuli
Ugumu wa misuli bila sababu ya kitaalamu (idiopathic)
Madhaifu ya mkao wa mtoto tumboni wakati wa ujauzito
Vihatarishi
Vifuatavyo ni vihatarishi vya Mguu farasi;
Historia ya familia yenye matatizo ya miguu
Magonjwa ya mfumo wa neva
Kuzaliwa kabla ya muda
Kiwango kidogo cha maji ya uzazi
Ujauzito wenye nafasi finyu kwa mtoto
Majeraha wakati wa kuzaliwa
Maambukizi au matatizo ya ukuaji wa neva
Vipimo na uchunguzi
Uchunguzi wa mwili:
Kupungua kwa mjongeo wa kanyagio kwenye juu katika kifundo cha mguu
Utambuzi wa kutembea kwa vidole (kwa watoto waliokaribia umri wa kutembea) au kuwa na mwendo wa kutembea usio kawaida.
Picha za mionzi:
X-ray kwa mifupa
Picha ya mionzi sauti kwa watoto wachanga (hasa kwa mguu kifundo)
Uchunguzi wa neva:
Kuchunguza kama kuna mtindio wa ubongo au mgongo wazi
Vipimo vya vinasaba: Ikiwa kuna mashaka ya kuwa sehemu ya ugonjwa wa kurithi
Matibabu
Matibabu bila upasuaji
Mazoezi ya kuvuta misuli: Kuvuta kifundo cha mguu kuelekea juu kila siku
Fiziotherapia: Mazoezi ya kuimarisha misuli na kuongeza urefu wa misuli
Kuweka plasta za kufunga miguu kwa hatua: Kama sehemu ya matibabu ya mguu kifundo (mfano: njia ya Ponseti)
Vifaa maalumu: Matumizi ya vifaa vya kusaidia kifundo kama AFO
Upasuaji
Kurefusha tendoni ya kisigino (Kuingeza tendoni ya Achilles): Kwa watoto wenye hali kali ambao hawajatibika kwa njia zingine.
Kuhamisha au kukata tendoni: Kwa matatizo yanayotokana na neva au misuli
Lini umpeleke mtoto kwa daktari
Mguu wa mtoto unaonekana kupinda au kuwa kukakamaa kwenye kifundo
Mtoto hapati ukuaji wa kimota kama vile kushindwa kusimamia kanyagio hadi kufikia miezi 9–12
Kutembea kwa vidole au kutotembea kabisa
Mazoezi ya nyumbani hayasaidii baada ya wiki chache
Mguu au miguu kuwa tofauti upande mmoja
Tiba ya nyumbani
Mazoezi ya kunyoosha kifundo: Yafanyike mara kadhaa kwa siku
Kuweka mtoto kwenye tumbo: Husaidia kuimarisha misuli ya mgongo na miguu
Kuchua mguu na misuli ya nyuma ya mguu taratibu
Kufuata ratiba ya kliniki kwa ufuatiliaji wa maendeleo ya mtoto.