Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatano, 10 Novemba 2021
Phecomelia
Phocomelia ni ulemavu wa maumbile ya miguu na mikono unaoonekana wakati wa kuzaliwa na hutokea kwa nadra sana. Ulemavu huu husababisha kutofanyika kikamilifu kwa miguu na mikono au kukosekana kabisa kwa viungo hivi.
Dalili za phecomelia
Miguu na mikono kuwa mifupi au kukosekana kwa vyote
Kiganja cha mkono au vidole vya mikono na miguu kujishikiza moja kwa moja kwenye kiwiliwili
Vidole vya miguu kujisikiza moja kwa moja kwenye nyonga
Kufanyika vibaya kwa mifupa ya uso na kichwa
Dalili zingine
Mbali na dalili za kutoumbika vema kwa miguu na mikono, dalili zingine za phocomelia ni;
Kutapika
Kipanda uso
Ongezeko la shinikizo ndani ya ubongo kutokana na ongezeko la maji ndani ya kichwa
Kuwa na shingo fupi
Madhaifu ya kiakili
Madhaifu ya kizazi, figo, urethra na moyo
Matatizo ya kuganda kwa damu
Visababishi
Nini husababisha phocomelia?
Thalidomide iliyokuwa ikitumika katika matibabu ya homa ya asubuh, wasiwasi uliopitiliza na ukoma wakati wa ujauzito imeonekana kusababisha ulemavu huu wa phecomeli. Nchi nyingi zinazoendelea ambazo bado zimeendelea kutumika thalidomide kama dawa pekee ya ukoma, zimeendelea kupata ulemavu huu.
Mbali na matumizi ya thalidomide kusabaisha phecomelia, watafiti pia wamehusianisha tatizo hili kusababishwa na sindromu ya kijenetiki, licha ya kutokea kwa nadra sana.
Ulemavu unaofanana na phecomelia
Ulemavu unaofanana na phecomelia ni;
Sindromu ya Roberts
Thrombocytopenia with radial aplasia (TAR)
Sindromu ya ulemavu mkali wa mikono na miguu
Vertebral hypersegmentation
Mirror polydactyly
Matibabu
Licha ya ulemavu wa phocomelia kutokuwa na tiba ponyaji, ulemavu huu una tiba saidizi ya viungo vya bandia vinavyoweza kumsaidia mlemavu kuishi kwenye mazingira yake.
Kama mtoto atakuwa na madhaifu kwenye mifupa ya kichwa, atafanyiwa upasuaji wa kurekebisha Kama utahitajika ili kuboresha ubora wa maisha.