top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

Jumatatu, 8 Novemba 2021

Saratani ya tezi dume

Saratani ya tezi dume

Epidemiolojia ya saratani ya tezi dume


Kimataifa Saratani ya tezi dume inaonekana kwa wingi kwenye Bara la Amerika kaskazini , Australia na na Kaskazini na Ulaya ya kati na inaonekana kwa kiasi kidogo zaidi kusini mashariki na kusini ya kati huko bara Asia


Katika bara la America inaonekana kwamba mzungu 1 kati ya wazungu 6 na mwafrika 1 kati ya Waafrika 5 wanapata Saratani hii maishani mwao.

Saratani ya tezi dume ni marachache kugundulika kwa wanaume walio chini ya miaka 40 na pia hutokea marachache kwa wanaume wenye umri chini ya miaka 50. Saratani hii pia imeonekana kwa watu waliokwisha kufa kwa magonjwa mengine ila walipofanyiwa uchunguzi ulionesha kwamba ugonjwa huu ulikuwepo kwa watu hao bila dalili yoyote. hivyo watu wachache huonesha dalili za ugonjwa huu. Asilimia zaidi ya 80% ya wanaume walio na miaka 80 wanaweza kuwa na Saratani hii, katika tafiti zilizofanyika sigara huambatana na ugonjwa huu ukilinganisha na wale ambao hawakuwahi kuvuta sigara maishani mwao kwa mtu aliyevuta sigara nyingi maishani mwake ilionekana kuhusiana kupata Saratani hii kuliko wale waliotumia kwa kiasi kidogo.

Tofauti za kirangi

Tafiti pia zinaonyesha kwamba Waafrika waishio amerika wana hatari zaidi ya kupata Saratani hii kuliko wazungu, Wahispania wana hatari sawasawa ya kupata Saratani hii ukilinganisha na wazungu. Waasia wenye Asili ya Asia wana hatari ndogo kupata Saratani hii

Nini mwisho wa saratani hii?

Vipimo vya msingi vinavyoonesha maendeleo ya Saratani hii ni gleason score grade, ukubwa wa Saratani na kama Saratani imepasua kuta ya tezi

Watu waliogunduliwa na Saratani hii mapema na kutolewa tezi hii, katika miaka 15 asilimia saba tu wanaweza kufa kutokana na Saratani hii. Hii inamaanisha ukigunduliwa mapema, umri wa kuishi bila madhara ya Saratani hii huongezeka

Wanaume wenye matatizo kwenye vinasaba kama mabadiliko kwenye kinasaba p53 wanahatari ya kuishi maisha mafupi kutokana na maendeleo ya kasi ya ugonjwa huu

Saratani ya tezi dume ni ya pili miongoni mwa Saratani zinazoongoza kwa kusababisa vifo kwa wanaume duniani.


Dalili


Zipi ni Dalili za saratani ya tezi dume?

Kutoka kwenye historia ya mgonjwa

Kwa sasa ugonjwa huu hutambuliwa kwa mtu asiye na dalili yoyote na kutambuliwa huko hutokana na kupima kemikali aina ya PSA mwilini inayotolewa na tezi dume na pia kutokana na uchunguzi unaofanyika kwa kupima tezi hii kwa njia ya DRE yaani kupimwa kwa kuwekewa ama kuingiziwa kidole kwenye njia ya haja kubwa na mtaalamu wa afya kutambua kama kuna mabadiliko yoyote. Na pia saratani ya tezi hii huweza kuonekana kwenye vinyama vinapotolewa kwa uchunguzi kwa mtu aliyevimba tezi dume

Dalili za awali

Watu wengi kabla ya ugunduzi wa kipimo cha PSA, walikua wanalalamika dalili kwenye njia ya mkojo kama kubakiza mkojo wakiwa wanakojoa ( urine retension) maumivu nyuma ya mgongo, na kukojoa damu. Dalili hizi kutokea haimaanishi una saratani hii moja kwa moja, bali inaweza kumaanisha magonjwa mengine pia. Kwa mfano mtu anayekojoa mara kwa mara, kushindwa kuzuia mkojo, na kupungua kwa wingi wa mkojo wakati wa haja ndogo maranyingi hutokana na kuvimba kwa tezi dume

Dalili za ugonjwa kusambaa

Hutokana na kusambaa kwa ugonjwa huu sehemu zingine za mwili kwa njia ya damu au mitoki

 • Kupungua uzito

 • Kupungukiwa damu

 • Maumivu ya mifupa pamoja na au bila mifupa kuvunjika

 • Kupoteza hisia (mfumo wa fahamu kuharibiwa)

 • Maumivu miguuni na miguu kuvimba kutokana na kuzibwa njia ya mitoki(lymphatic)

 • Kupanda kwa urea mwilini (uremic symptoms) inaweza kutokea kutokana na kuziba mirija inayotoa mkojo kwenye kibofu na hivo kuletea mtu kuchanganyikiwa na

Dalili zinazoonekana kutokana na vipimo vya dakitari

Kipimo hichi hakiwezi kutofautisha saratani na uvimbe wa kawaia wa tezi dume kwa hivyo kipimo cha kupima nyama (biopsy) hufanyika kuondoa utata huu

 • Kukonda kutokana na Saratani

 • Maumivu ya mifupa ikishikwa

 • Uvimbe miguuni au/pamoja na ugonjwa wa kutokwa damu kutokana na chembe mgando kuisha ama DVT

 • Mitoki kuvimba hasa maeneo ya nyonga

 • Kibofu kuwa kikubwa kwa sababu ya mkojo kuzuiwa ndani ya kibofu

Uchunguzi wa mfumo wa fahamu unaweza kuwa kama kupima uwezo wa mkundu kubana ( sphincter tone) unatakiwa ufanyike ili kugundua kama kuna mkandamizo kweye mishipa ya fahamu ya uti wa mgomgo kutokana na Saratani hii.

Uchunguzi kwenye njia ya haja kubwa DRE

Inategemea uzoefu wa mpimaji, na uchunguzi wa mara kwa mara wa tezi hii huweza kumfanya mtaalamu kutofautisha au kuweza kujua kama kuna uvimbe wa kawaida au usio wa kawaida

Vitu kama tezi kutokuwa na usawa na kubadilika kwa umbo halisi (texture) ..kipimo hiki kinaweza kuofautisha magonjwa tofauti kama vile vifuko vya mvilio wa maji katika tezi dume ama prostate cyst na hivo ni muhimu kuchukua vinyama ili kuweza kupima kama uvimbe huu ni wa kawaia au ni Saratani

Magonjwa gani yanaweza kufanana dalili na Saratani ya tezi dume?

 • Usaa kwenye tezi dume au maambukizi ya ghafla ya tezi dume

 • Maambukizi ya bakiteria kwenye tezi dume( bacterial prostatis)

 • Uvimbe wa kawada wa tezi dume ama BP

 • Maambukizi ya TB kwenye tezi dume (tuberculosis prostatis)

 • Maambukizi yasiyo ya bakiterial kwenye tezi dume (nonbacterial prostatis)


Visababishi


Visababishi ama vihatarishi vya kupata saratani ya tezi dume ni vipi?

Kuna sababu za kiasiri kama vina saba kama ijulikanavyo kwamaba hatari ya kupata Saratani dume ni kubwa zaidi kwa watu wanaoishi Afrika mangalibi na hatari hupungua kwa watu wazaliwa asiri ya bara asia. Kuongezeka kwa iadi kati ya waasia walioamia marekani inaonesha kwamba mazingira huchangia, sanan sana chakula. Na pia Saratani hii pia hutokea maranyingi kwenye familia yenye historia ya Saratani hii

Vinasaba

Mabadiliko ya vinasaba au kuwa na vinasaba vinavyoletea saratani hii kama HPC1 na PCAP inayopatikana kwenye chromosom X ambapo hulithiwa mtoto hadi mtoto. Wanaume wenye ndugu walio na historia ya Saratani hii kwenye familia yao wapo hatarini sana kupata saratani hii na hutokea miaka 6 hadi 7 mapema zaidi na tafiti zingine zinaonesha kuna uhusiano wa Saratani hii na Saratani ya titi kwa wanaume ambapo ikiwa kuna historia ya Saratani hii kwenye familia huongeza hatari zaidi ya kupata saratani ya tezi dume na huwa mbaya zaidi na hutokea kwenye umri mdogo

Chakula

Tafiti zinaonesha kuna uhusiano wa saratani hii na vyakula tofauti, uzito mkubwa(obesity) na ulaji wa mafuta kwa wingi

Vichocheo vya mwili (hormones)

Kutokana na matumizi ya dawa zinazopunguza vichocheo vya mwili viitwavyo androgeni( androgen suppression therapy) huletea kupungua kwa ukuaji wa Saratani hii kwa mtu na pia huifanya kuwa ndogo, hata hivyo wanaume waliohasiwa hawapati saratani ya tezi dume inayoongoa kutokea yaani adenocarcinoma

Kunatafiti zinaonesha kuongezeka kwa vichochezi aina ya luteinizing hormone (LH) na testosterone huongeza hatari kwa kiasi kidogo ya kupata Saratani hii

Dawa za aina ya 5alpha reductase kama finasteride

Katika kupamba na saratani ta tezi dume, dawa hii imetumika, ilitumika kuzuia hatari ya kupata saratani hii na imeonyesha kufanya kazi. Lakini tafiti zinaonesha pia kwamba utumiaji wa dawa hii licha ya kuzuia baadhi ya saratani, baadhi ya watu wamepata saratani yenye makari zaidi kwenye tezi dume

Ndipo Mamlaka ya chakula na dawa Duniani (FDA) mwaka 2010 haikuruhusu dawa hii kutumika kwa matumizi hayo kwa sababu ya kuzuka kwa saratani ya tezi dume yenye makari zaidi kwa baadhi ya watumiaji


Vipimo


Vipimo vipi hufanyika na matibabu gani yaliyopo?


Vipimo vya awali vya kugundua ugonjwa (screening)

Kipimo cha kugundua kemikali inayotolewa na tezi dume (prostate specific antigen ,PSA) na pia kuangalia mabadiliko ya kianatomia katika tezi dume kwa kutumia kidole kupitia njia ya haja kubwa yaani DRE hutumika katika ugunduzi wa mapema wa saratani hii

Kwa watu walio na tezi dume ya kawaida, walio kati ya miaka 45-49 baada ya kupimwa kipimo cha DRE wanatakiwa waludie kupima wafikishapo miaka 50 endapo kipimo cha PSA nacho ni cha kawaida.

Wanaume walio na miaka 50-70 wanaweza kupima kila baada ya mwaka 1-2 . lakini kuna aina tofauti za maoni kwamba vipimo hivi vifanyike kwenye umri gani.

Kupima kemikali aina ya PSA

Kadili ya kiwango cha PSA kinavyoongezeka, uwezekano wa kupata Saratani ya tezi dume huongezeka na ilifikiliwa kuwa kiwango cha juu cha kugundua Saratani ni 4ng/dl lakini tafiti zinaonesha PSA ikiwa 1ng/l Saratani inaweza kugunduliwa kwa kwa asilimia 8% na ikiwa nyingi 4-10ng/l unaweza kugunduliwa kwa asilimia 25% ya watu

Kipimo cha vinyama vya tezi dume

Kipimo hichi huhusisha kukata vinyama kwenye tezi dume na kufanyiwa uchunguzi

Matibabu


Matibabu ya saratani ya tezi dume

Yapo matibabu aina tofauti na yanategemea Saratani imeenea au imesambaa kwa kiasi gani mwilini

 • Matibabu ya upasuaji-kuondoa tezi dume

 • Matibabu ya miozi

 • Matibabu ya dawa za chemotherapy


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

13 Julai 2023 19:03:06

Rejea za mada hii:

bottom of page