top of page

Mwandishi:

Mhhariri

Dkt. Benjamin L, MD

Dkt. Peter A, MD

Jumapili, 14 Novemba 2021

Sunzua

Sunzua

Sunzua ni aina ya uoto utokeao kwenye ngozi laini na ngumu na husababishwa na anuai mbalimbali za kirusi human papillomavirus (HPV).


Kuna anuai zaidi ya 100 ya kirusi HPV, hata hivyo kuna anuai zinazosababisha sunzua maeneo mbalimbali kama vile anuai ya 6 na 11 husababisha sana sunzua kwenye maeneo ya siri.


Matibabu ya suzua yanaweza kuwa magumu na baadhi ya nyakati sunzua huisha zenyewe bila tiba.


Usambazaji


Maambukizi ya HPV yanaweza kutokea kwa kushika sunzua au kwa njia ya kujamiana kama wapo maeneo ya siri. Matukio yoyote yanayoongeza hatari ya kuharibu ukuta wa ngozi huongeza hatari ya kupata sunzua.


Sunzua inaweza kuwa saratani?


Sunzua inaweza kubadilika kuwa saratani kwa baadhi ya watu wenye vihatarishi kama vile wale wenye upungufu wa kinga mwilini na wale wenye maambukizi ya kirusi HPV anuani ya 5, 8, 20 na 47.


Aina za sunzua


Kuna aina mbalimbali za sunzua ambazo zimegawanywa kulingana na sehemu ya mwili iliyoathirika na kirusi

kilichosababisha. Aina hizo ni;


 • Sunzua ya kawaida- Husababishwa sana na anuai 2 na 3 ya kirusi HPV ikifuatiwa na 1, 3, 27, 29, na 57

 • Sunzua bapa:- Husababishwa na anuai ya 3, 10 na 28 ya kirusi HPV

 • Sunzua ya shini ya ngozi ya viganja na kanyagio:- Husabaishwa sana na anuai ya 1 ya kirusi HPV ikifuatiwa na anuai ya 2, 3, 4, 27, na 57 ya kirusi HPV

 • Sunzua ya kifuko cha maji:- Husababishwa na anuai ya 60 ya kirusi HPV

 • Sunzua inayoathiri epithelia:- Husababiswha na anuai ya 13 na 32 ya kirusi HPV

 • Sunzua ya Bucha:- Husababiswha na anuai ya 7 ya kirusi cha HPV


Dalili


Mara nyingi sunzua huwa haina dalili yoyote ile, hata hivyo huweza kuhariu mwonekano wa sehemu ilipoota na kwa wagonjwa wachache inaweza kusababisha maumivu.



 • Sunzua inayoota kwenye kanyagio huambatana na maumivu makali kwa sababu ya mgandamizo unaotokea na wakati mwngine inaweza kutoa damu na kuathiri mjongeo wa mtu.

 • Sunzua ya kawaida huwa kama kipele kidogo kisichoeleweka kontua na chenye urefu kuanzia sentimita 1 nakadharika.

 • Sunzua za kawaida mara nyingi huoekana mikononi au miguuni

 • Sunzua za kawaida zinaoonekana maeneo ya kuzunguka midomo na kope huweza kuwa ndefu na nyembamba.

 • Sunzua kwenye kanyagio na viganja vya mikono huwa na umbo na hupatikana chini ya ngozi kiasi cha kuweza kufikiriwa kuwa ni sugu, hata hivyo sifa zake ni kuwa na maumivu kama maeneo yeye sunzua yakishikwa.


 • Sunzua bapa huonekana kama uoto wenye ukubwa wa milimita 1 hadi 7 na idadi yake huweza mamia.

 • Sunzua ya bucha huonekana kwa watu wanaojihusisha na kushika nyama na mazao ya nyama. Huwa na mwonekano wa kama uyoga bapa unaoota kwenye gome la na huwa mkubwa pia.

 • Sunzua ya epithelia hutokea kwenye kuta za kinywa na midomo. Huonekana kama vipele vidogo vyeupe vyenye ukubwa wa milimita 1 hadi 5 na hukaa kwenye makundi.

 • Sunzua ya kifuko cha maji hutokea kwenye maeneo yanayobeba uzito wa mwili kama vile kanyagio na huwa na kuta laini.


Matibabu ya sunzua


Baada ya kufahamika kwa kuchunguza wa sunzua, matibabu yake hutegemea dalili, uchaguzi wa mgonjwa na gharama. Licha ya kuwa na matibabu aina kadhaa ya sunzua, hakuna matibabu yenye ufanisi mkubwa na mara nyingi hujirudia kwa aina nyingi za matibabu yaliyopo. Unapaswa kuchagua matibabu ya gharama nafuu na yasiyokuletea maumivu.


Matibabu ya dawa

Dawa za kupaka ambazo huandikwa na daktari kama;

 • Salicylic acid

 • Retinoic acid

 • Podophyllin

 • 5-fluorouracil

 • Interferon

 • Imiquimod

 • Cidofovir

 • Cryotherapy

 • Bleomycin

 • Cimetidine


Matiabu yasiyo dawa

Matibabu asili na tiba isiyo dawa ya sunzua huhisisha;

 • Tiba ya makovu

 • Hypnosis

 • Tiba joto

 • Matumizi ya tiba kutoka kwenye viini vya mimea


Matibabu ya upasuaji

Matibabu ya sunzua kwa upasuaji huhusisha;


 • Kukausha sunzua kwa barafu

 • Kukata sunzua kwa mwanga wa laser

 • Kukata sunzua kwa kisu cha umeme

 • Kukata sunzua kwa kisu


Magonjwa yanayofanana


Magonjwa yanayofanana na sunzua kiasi cha kuchanganywa nayo ni;


 • Molluscum contagiosum

 • Seborrheic keratosisi

 • Lichen planus

 • Saratani ya seli za squamous

 • Keratoacanthoma

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

14 Novemba 2021 16:35:14

Rejea za mada hii:

1. Ahmad M. Al Aboud, et al. Warts. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK431047/. Imechukuliwa 14.11.2021

2. U.S. Food and Drug Administration. Some wart removers are flammable. http://www.fda.gov/ForConsumers/ConsumerUpdates/ucm381429.htm?source=govdelivery&utm_medium=email&utm_source=govdelivery. Imechukuliwa 14.11.2021

3. Landis MN, et al. Recalcitrant plantar warts treated with recombinant quadrivalent human papillomavirus vaccine. Journal of the American Academy of Dermatology. 2012;67:e73.

Habif TP. Plantar warts. In: Clinical Dermatology: A Color Guide to Diagnosis and Therapy. 6th ed. Edinburgh, U.K.; New York, N.Y.: Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Accessed March 2, 2017.

Kwok CS, et al. Topical treatments for cutaneous warts. Cochrane Database of Systematic Reviews. http://onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1002/14651858.CD001781.pub3/abstract. Accessed March 2, 2017.

American Academy of Dermatology. Warts. http://www.aad.org/dermatology-a-to-z/diseases-and-treatments/u---w/warts. Imechukuliwa 14.11.2021

bottom of page