Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Peter A, MD
Imeboreshwa:
13 Desemba 2025, 14:03:28

Ugonjwa Leptospirosis
Leptospirosis ni ugonjwa unaoweza kumpaka binadamu na mnyama. Kwa miaka mingi ugonjwa huu umekuwa hautokei sana kwa wanyama hata hivyo hivi karibuni kumekuwa na visa vingi. Kumekuwa na visa mbalimbali vimeripotiwa nchini Tanzania kuhusu Leptospirosis kati ya mwezi wa 6 na 7/2022.
Bakteria wanaosababisha Leptospirosis huenezwa kupitia mkojo wa wanyama walioambukizwa, na wanaweza kuingia ndani ya maji au udongo kisha kuishi huko kwa wiki hadi miezi. Aina mbalimbali za wanyamapori na wa nyumbani hubeba bakteria hao.
Wanyama hao hujumuisha, licha ya kutokuwa wao tu:
Ng'ombe
Nguruwe
Farasi
Mbwa
Panya
Wanyama wa mwituni
Wakati wanyama hawa wanaambukizwa, wanaweza wasionyeshe dalili za ugonjwa. Wanyama alioambukizwa wanaweza kuweka bakteria katika mazingira kupitia kinyesi au mkojo kila mara au kwa kipindi cha miezi michache hadi miaka kadhaa.
Uambukizaji wa bakteria wa Leptospirosis kwa binadamu
Binadamu wanaweza kuambukizwa bakteria wa Leptospirosis kupitia:
Kugusana na mkojo (au viowevu vingine vya mwili, isipokuwa mate) kutoka kwa wanyama walioambukizwa
Kugusana na maji, udongo, au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama walioambukizwa
Namna bakteria wanavyoingia mwilini mwa binadamu
Bakteria wanaweza kuingia mwilini kupitia ngozi au utando wa laini wa ngozi (macho, pua, au mdomo), hasa ikiwa ngozi imepasuka kutokana na kujikata au mikraruzo. Unywaji wa maji machafu pia unaweza kusababisha maambukizi.
Mlipuko wa Leptospirosis kawaida husababishwa na utumiaji wa maji yaliyochafuliwa na vimelea, kama vile maji ya mafuriko. Maambukizi ya kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu mwingine ni nadra sana kutokea.
Dalili za Leptospirosis
Kwa wanadamu, Leptospirosis inaweza kusababisha dalili mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
Homa kali
Kichwa
Baridi
Maumivu ya misuli
Kutapika
Ngozi ya manjano na macho
Macho mekundu
Maumivu ya tumbo
Kuhara
Harara kwenye ngozi
Nyingi ya dalili hizi zinaweza kuchanganywa na dalili za magonjwa mengine. Kwa kuongezea, baadhi ya watu walioambukizwa wanaweza wasionyeshe dalili yoyote ile.
Muda wa ugonjwa wa leptospirosis kuonekana
Mara baada ya kuambukizwa, huchukua siku 2 hadi wiki 4 kwa dalili kuonekana. Mara nyingi ugonjwa huanza ghafla kwa kusababisha homa na dalili zingine.
Awamu za ugonjwa wa leptospirosis
Leptospirosis huweza kutokea katika awamu mbili ambazo ni:
Baada ya awamu ya kwanza (na homa, baridi, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, kutapika, au kuhara) mgonjwa anaweza kupona kwa muda lakini hugua tena.
Ikiwa awamu ya pili itatokea, ni kali zaidi; mtu anaweza kuwa na kushindwa kwa figo au ini au homa ya uti wa mgongo.
Muda wa ugonjwa wa leptospirosis kupotea
Ugonjwa huu hudumu kwa siku chache hadi wiki 3 au zaidi, na pasipo matibabu, inaweza kuchukuchua miezi kadhaa kupona.
Vihatarishi vya kupata leptospirosis
Leptospirosis hutokea duniani kote, lakini ni kawaida katika hali ya hewa ya joto au kitropiki. Watu wafuatao huwa na hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa:
Wakulima
Wafanyakazi wa mgodi
Wazibua vyoo
Wafanyakazi wa machinjio
Wafugaji na walezi wa wanyama
Wafanyakazi wa samaki
Wakulima wa maziwa
Wafanyakazi wa jeshi
Ugonjwa huu pia unaonekana kuenezwa sana kwa watu wanaofanya kazi kwenye maji au kuogelea kwenye ziwani.
Matibabu ya leptospirosis
Leptospirosis hutibiwa kwa antibayotiki kama vile doxycycline au Penisilini, ambayo inapaswa kutolewa mapema wakati wa ugonjwa huo.
Antibiotiki za za mishipa zinaweza kuhitajika kwa watu wenye dalili kali zaidi. Watu walio na dalili zinazoashiria ugonjwa huu wanapaswa kuwasiliana na mtoa huduma ya afya mara moja kwa ushauri na tiba.
Kinga ya leptospirosis
Maambukizi ya Leptospirosis yanaweza kupunguzwa kwa kuacha kuogelea au kufanya kazi kwenye maeneo yenye maji yaliyochafuliwa na vimelea kwa mkojo au kinyesi chao.
Vifaa kinga kama viatu na glavu vinapaswa kuvaliwa kwa wale wanaofanya kazi kwenye maji yaliyochafuliwa na vimelea au wanaofanya michezo mbalimbali katika maji hayo yanayoguswa na wanyama.
Rejea za mada hii:
Surveillance for Waterborne Disease and Outbreaks Associated with Recreational Water Use and Other Aquatic Facility–Associated Health Events—United States, 2005–2006. MMWR. 2008 Sep 12;57(SS09):1–29.
Surveillance for Waterborne Disease and Outbreaks Associated with Recreational Water—United States, 2003–2004. MMWR. 2006 Dec 22;55(SS12):1–24.
Surveillance for Waterborne-Disease Outbreaks—United States, 1999–2000. MMWR. 2002 Nov 22;51(SS08):1–28.
Update: Outbreak of Acute Febrile Illness Among Athletes Participating in Eco-Challenge–Sabah 2000—Borneo, Malaysia, 2000. MMWR. 2002 Jan 19;50(02):21–24.
Public Health Dispatch: Outbreak of Acute Febrile Illness Among Participants in Eco-Challenge Sabah 2000—Malaysia, 2000. MMWR. 2000 Sep 15;49(36):816–817.
Update: Leptospirosis and Unexplained Acute Febrile Illness Among Athletes Participating in Triathlons—Illinois and Wisconsin, 1998. MMWR. 1998 Aug 21;47(32):673–676.
Outbreak of Acute Febrile Illness Among Athletes Participating in Triathlons—Wisconsin and Illinois, 1998. MMWR. 1998 Jul 24;47(28):585–588.
Outbreak of Leptospirosis Among White-Water Rafters—Costa Rica, 1996. MMWR. 1997 Jun 27;46(25):577–579.
Guerra MA. Leptospirosis. J Am Vet Med Assoc. 2009 Feb 15;234(4):472–478.
Levett PN. Leptospira and Leptonema. In: Murray PR, Baron EJ, Pfaller MA, Tenover FC, Yolken RH, editors. Manual of Clinical Microbiology. 8th ed. Washington (DC): ASM Press; 2003.
Levett PN. Leptospirosis. Clin Microbiol Rev. 2001;14:296–326.
Tappero JW, Ashford DA, Perkins BA. Leptospirosis. In: Mandell GL, Bennett JE, Dolin R, editors. Principles and Practice of Infectious Diseases. 5th ed. New York: Churchill Livingstone; 2000. p. 2495–2501.
