Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatatu, 8 Novemba 2021

Uteja wa dawa za kulevya
Uteja ni hali ya mwili kutegemea dawa zisizoruhusiwa au yale yanayoruhusiwa kisheria ambayo huleta hali ya kuufurahisha mwili lakinimwisho wake hupelekea mwili kushindwa kuishi pasipo matumizi ya dawa hizo. Pombe na nicotine ni dawa yanayoruhusiwa lakini huweza kusababisha mtu kuwa teja.
Unapokuwa teja, unakosa uwezo wa kudhibiti mwili kutumia dawa hizo licha ya madhara yanayotokana na matumizi. Uteja wa dawa unaweza kupelekea hali ya mwili kuwa na hamu kuu ya kutumia dawa na mtu anaweza kutaka kuacha kutumia lakini watu wengi hushindwa kuacha kutumia dawa hizo.
Uteja wa dawa unaweza kusababisha matatizo makubwa ya mda mrefu ikiwa pamoja na matatizo ya kimwili na kiakili, mahusiano, kazi na sheria za nchi
Utahitaji msaada kutoka kwa daktari wako, marafiki, makundi maalumu ya kuwahudumia mateja ili kukusaidia kuacha dawa hazo.
​
Dalili
Uteja wa dawa huanza pale mtu anapoanza kutumia dawa hizo kwenye matukio ya kijamii. Kwa baadhi ya watu utumiaji hongezeka na huwa mara kwa mara. Hatari ya kuwa teja na uharaka wa kuwa teja hutegemea aina ya dawa. Dawa nyingine za kulevya huwa ni hatari na husabaisha uteja ndani ya mda mfupi kuliko dawa aina nyingine.
Mda unapozidi kwenda unaweza hitaji dozi kubwa ya dawa ili ikufikishe pale kwenye raha unazotaka. Unaweza kuhitaji dawa tu ili ujihisi vema, uburudike. Matumizi ya dawa yanapoongezeka utajitambua kwamba huwezi ishi bila kupata dawa hizo. Kitendo cha kuacha dawa hizo kinaweza kukusababisha kuwa na hamu kuu isiyozuilika ya kupata dawa hizo na kuumwa mwili(dalili za kuacha dawa)
Dalili za uteja na tabia huhusisha
Kujihisi kwamba unatakiwa kutumia dawa kama kama sehemu ya maisha yako- inaweza kuwa kila siku au mara nyingi kwa siku
Kuwa na hamu kuu kwenye dawa hiyo.
Jinsi mda unavyokwenda unahitaji dozi kubwa ili kupata raha ile unayotaka
Kutumia pesa kununua dawa hata kama huna kipato cha kununulia
Kutofanya majukumu na mikakati yako au kuacha kazi za kijamii, matukio ya kijamii kwa sababu ya matumizi ya dawa
Kufanya matendo ambayo usingeweza kufanya kama usingekuwa unatumia dawa ili tu upate dawa mfano wizi
Kuendesha gali au Kufanya matendo ya hatari ukiongozwa na dawa uliyotumia
Kuwekezam da wako mwingi na nguvu ili kupata na kutumia dawa
Kufeli kuacha kutumia dawa
Kupata dalili za kuacha kutumia dawa unapojaribu kuacha kutumia dawa hizo
Kutambua mtu anayetumia dawa za kulevya katika familia
Ishara
Wakati mwingine ni vigumu kutambua mtu anayetumia dawa kwa vijana wadogo kwa sababu huwa na hali za kubadilika. Ishara zinazoweza kuonyesha kwamba mtoto anatumiadawa ni;
Matatizo shuleni
Kutohudhuria shuleni mara kwa mara au kazini, kutopenda shule au kazi ghafla tu bila sababu, kushuka kwa ufaulu na utendaji kazi.
Matatizo ya kimwili
kukosa nguzu au kishawishi cha kufanya kazi
Mkiwa
Kukosa moyo wa kupenda kuvaa, kujitazama anavyoonekana.
Kubadilika kwa tabia
kuwa msiri mahari anapokwenda na marafiki zake, kukataa mwana familia kuingia katika chumba chake au kubadilika ghafla kwa tabia na mahusiano na wanafamilia.
Kutumia pesa
kuomba pesa bila kuwa na sababu ya kueleweka, kuiba hela au vitu vya ndani ili kuweza kuuza na kununua dawa.
Kutambua viashiria vya dawa au madhara ya dawa mwilini
Dalili na viashiria vya dawa za kulevya hutegemea aina ya dawa, kuna aina nyingi za dawa na dalili pia
Bangi, hashish
Bangi huweza kutumiwa kwa njia ya kuvuta moshi, kula au kuvuta hewa ya mvuke wa dawa. Bangi mara nyingi hutumiwa au hufuatiwa na pombe au dawa zingine za kulevya.
Dalili na viashiria kwa mtu aliyetumia mda mfupi uliopita ni;
Kujihishi furaha ya uongo au kujihisi hauna matatizo yoyote
Kubadilika kwa mirango ya fahamu kam Kuongeze kuona, kusikia na ladha
Kuongezeka kwa shinikizo la damu na mapigo ya moyo
Macho kuwa mekundu
Midomo kukauka
Kukosa mizani kwenye mwili, kama kutoweza kutembea vema n.k
Kushindwa kukumbuka au kujikusanya kiakilikwenye jambo moja
Kuongezeka kwa hamu ya kula
Hisia za kwamba watuwanataka kukudhuru
Kupungua uwezo wa kwendana na mtu katika matendo
Madhara ya mda mrefu ya mtumiaji sugu wa bangi na pombe ni
Kupungua kwa uwezo wa kiakili
Kupungua ufanisi shuleni na kazini
Kupungua kwa marafiki na hali ya kupenda vitu
Dawa ya kutengenezwa aina ya bangi
Furaha ya uongo kujisikia mkubwa
Kuongezeka kwa hali
Kupata tulizo kuu
Kubadilika kwa hisia za kuona, kusikia na ladha
Msongo wa mawazo na kughazilika haraka
Kuisi watu wanataka kumdhuru
Kuhisi watu wanamuongelea
Kuongezeka kwa shinikizo la damu na maigo ya mayo
Kutapika
Kuchanganyikiwa
Cocaine na amphetamine kama ectasy
Dalili na viashiria ni hizi;
Furaha ya uongo
Kuongezeka na kujihusisha na jamii
Kuongezeka kwa nguvu na hali ya kukasilika
Kuongezeka hisia za kimapenzi
Kuongezeka kwa shinikizo la damu na mapigo ya moyo
Maumivu ya kifua
Kuhisi watu wanataka kukudhuru
Tatizo la kupaniki(kupata hou kuu)
Kuona au kusikia watu wanamwongelea
Uzezeta
Tabia za ukichaa na fujo
Dawa aina ya barbiturate ba benzodiazepines
​
Dawa hizi hufanya kazi kwenye mfumo wa juu kwa kupunguza utendaji kazi wa ubongo. Hutumiwa na watu kwa ajili ya tulizo au kwa ajiri ya kusahau au kuhamisha akili au mawazo kwenye jambo au hisia Fulani.
Phenobarbital, amobarbital ni mfano wa dawa hizi. Mfano wa benzodiazepines ni diazepam(valium) alprazolam lorazepam clonazepam n.k
Dalili za mtu aliyetumia hivi punde ni
Kushikwa na usingizi- kuwa mtu akiyezinzia
Kuongea kama mtu aliyelewa
Kushindwa kutembea vema
Furaha ya uongo au kujihisi upo juu
Matatizo ya kumbukumbu na kujikita kiakili kwenye jambo Fulani
Macho kuzunguka yenyewe- Malezu
Kukosa kujizuia
Kupungua kwa shinikizo la damu na kupumua taratibu
Kizunguzungu
Msongo wa mawazo
Cocine na viamsha mwili vingine
Vichochezi mwili kama jamii ya amphetamine, cocaine hutumia mara nyingi mtu anapotafuta kujihisi ananguvu kujihisi yupo juu, kuongeza utandaji kazi shuleni na kazini au kupunguza uzito au kupunguza hamu ya kula.
Dalili na viashiria ni;
Kujiamini kupita kiasi
Kuwa makini
Kuwa na nguvu na kutotulia
Kubadilika tabia na kuwa na hasira
au kuongea maneo mengi yasiyoleta maana kamili(yasiyo na muunganiko unaoeleweka)
kutanuka kwa mboni ya jicho
kusikia au kuona watu wanakuongelea au kuwa na mawazo ya uongo
kutotulia au kubadilika kwa hali ya mtu
kubadilika kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu
kichefuchefu au kutapika na kupungua kwa uzito
uharibifu katika pua kama unatumia wa njia kunusa unga
kukosa usingizi
hisia za kuona watu wanataka kukuua au kukudhuru
msongo wa mawazo kama dawa ikiisha kwenye damu
Visababishi
​​
Kama yalivyo magonjwa ya akili, mambo mengi yanaweza kupelekea mtu kuwa teja wa dawa na utegemezi. Mambo ya msingi ni;
Sababu za kimazingira- imani za familia na kujiweka kwenye makundi yanayotumia dawa za kulevya, huchangia kusababisha mtu kutumia dawa.
Sababu za kijeni-mara unapoanza kutumia dawa, kuwa teja huweza kuchangiwa au kuhamasishwa na mambo ya kijeni ambayo hurithiwa ambapo huweza kusababisha kuchelewa kuwa teja au kuwahi kuwa teja.
Mabadiliko katika ubongo
Mabadiliko ya kifizikia huonekana pale matumizi ya mara kwa mara yanapofanya mabadiliko dhidi ya hisia nzuri.
Uteja wa dawa husababisha mabadiliko katika mishipa ya fahamu ain Fulani katika ubongo. Mishipa ya fahamu hutumia kemikali Fulani kusafilisha habari katika mshipa mmoja na mwingine. Mabadiliko haya huweza kukaa mda mrefu baada ya kuacha dawa.
​
Vihatarishi
​
Mtu wa umri wowote ule, jinsia yoyote na mwenye kipato cha aina yoyote huweza kuwa teja. Hata hivyo baadhi ya mambo huongeza hatari ya kuwa teja.
Historia ya teja katika familia-Uteja wa dawa hutokea sana kwenye familia Fulani na huonekana kuchangiwa na hali ya kijeni(kurithi) kama una ndugu wa damu kama mzazi au wadogo zako au kaka/dada zako wenye matatizo ya kunywa pombe na dawa, wewe pia una hatari ya kuwa teja pia.
Kuwa mwanaume- wanaume wanahatari ya kuwa mateja sana kuliko wanawake. Hata hivyo kasi ya kuwa teja kwa wanawake baada ya kuanza dawa huwa haraka zaidi kuliko wanaume
Kama una tatizo la kiakili ka aADHD au Msongo wa mawazo kutokana na kumbukumbu za kuumizwa una hatarishi ya kuwa tegemezi kwenye dawa ya kulevya
Makundi- makundi ni chanzo kikuu cha kuanza kutumia dawa na kuwa teja haswa kwa watoto wadogo(vijana)
Kutojihisusha na familia-matatizo ya kifamilia au kukosa mshikamano na wazazi wako au ndugu wa damu huongeza hatari ya kutumia dawa, kwa kukosa mwongozo wa wazazi
Msongo wa mawazo, huzuniko kuu na upweke- kutumia dawa kunaweza kumsaidia mtu huyu kuendana na hali yake anayokumbana nayo. Watu wa namna hii huweza kuwa mateja wa dawa.
Kutumia dawa yanayosababisha uteja- baadhi ya dawa kama yale ya kuchochea mwili, cocaine au dawa za kuondoa maumivu huweza kusababisha kuwa teja haraka.
​
Madhara
​
Madhara yanaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu ikitegemea aina ya dawa unayotumia
​
Madhara ya mda mrefu huwa;
​
Kupata magonjwa ya kuambukizwa- UKIMWI, kwa kufanya ngono isiyo salama au kuchangia sindano
Matatizo mengine ya kiafya-matatizo yanaweza kuwa ya mda mfupi au mrefu ikitegemea kwa mda gani umetumia dawa
Ajari- kama ukiw ateja unaweza kufanya kazi au matendo hatarishi katika uhai wako na kupelekea ajri
Kuua- watu walio mateja huua zaidi kuliko watu wasio mateja
Matatizo ya kifamilia- mabadiliko ya kitabia huweza kusababisha matatizo kwenye ndoa na kushindwa kulea watoto
Matatizo kazini- kupungua kwa ufanisi
Matatizo shuleni- kupungua ufaulu katika masomo
Matatizo ya isheria- kwa kumiliki dawa ya kulevya kuuza au kuendesha gari ovyo mara unapokuwa umetumia dawa huweza kusababisha migogoro kwa afisa na sheria za nchi
Matatizo ya kipato- kutumia pesa zote kwenye ununuzi wa dawa, kunamfanya mtu awe kwenye madeni na kujihusisha na matendo maovu yasiyokubalika na jamii
Vipimo na utambuzi
Utambuzi huweza kufanywa kwa kutumia mwongozo wa DSM-5
Vipimo vingine vinavyoweza kufanyika ni vipimo vya damu, mkojo n.k. vipimo hivi husaidia katika matibabu na sio kutambua uteja.
​​
Matibabu
Hatua za matibabu zitakazoelezewa hapa chini zinaweza kusaidia kuachana na utaja na kuacha kutumia dawa ya kulevya na
​
Uteja na Mkakati huhusisha
Matibabu mtu mmoja, kwa makundi, au familia
Kujikita katika kuelewa asili ya uteja na jinsi ya kuzia usijitokeze tena
Aina ya matibabu unayohitaj yanayokidhi mahitaji yako kama vile kulazwa kituoni au kupata matibabu kama mgonjwa wa nje.
Kuondoa sumu mwilini
Madhumuni ni kukusaidia kuacha kutumia dawa ya kulevya haraka iwezekanavyo kwa usalama. Kwa baadhi ya watu wanaweza kupata matibabu haya kama wagonjwa wan je, na baadhi watahitaji kulazwa hospitali au kwenye kituo maalumu cha kutibu watumiaji wa dawa za kulevya.
Kuacha kutumia dawa mbalimbali ya kulevya hleta dalili mbalimbali kwenye mwili. Kuacha kutumia dawa huweza kufanywa kwa kupunguza dozi ya dawa hizo au kupewa dawa mbadala zinazofanya kazi kama kiini kwenye dawa uliyokuwa unatumia. Dawa kama methadone, buprenorphine au muunganiko wa buprenorphine na naloxone hutumika
Ushauri
Kama sehemu ya matibabu, tiba ushauri hutumika. Unaweza kufanywa na mwana saikolojia, mtaalamu wa magonjwa ya akili au daktari kwa kuhusisha wana familia mwathirika na makundi ya watu. Mshauri huwez akufanya yafuatayo
Kukusaidia kutambua njia za kuweza kushinda hali ya shauku kuu ya kutaka kutumia dawa
Kukupa mpango wa kujizuia kutumia dawa ama kujirudia kutumia dawa
Kukupa mwongozo jinsi ya kupambana na hali ya kujirudia kutaka kutumia dawa kama ikitokea
Kuongelea maswala kuhusu kazi, matatizo ya kisheria na mahusianao ya familia na marafiki
Kuhusisha wanafamilia ili kusaidia kuacha matumizi ya dawa.
Makundi saidizi
Mtaalamu atakusaidia kukuelekeza kwenye makundi saidizi na utapata msaada wa kukusaidia kuacha kutumia dawa