Metformin
imeandikwa na madaktari wa ulyclinic
Matumizi
​
Kisukari aina ya 2, wagonjwa wenye uzito mkubwa kutokana na matumizi ya madawa za magonjwa ya akili
Hufanyaje kazi?
Hupunguza ini kuzalisha sukari, hupunguza ufyonzwaji sukari tumboni kutoka kwenye chakula na huongeza hisia za mwili kwenye homoni insulin.
Madhara yasiyotakiwa
-
Kichefuchefu kutapika na kuharisha
-
Kutomengenywa chakula tumboni-tumbo kuharibika- tumia na chakula
-
Ladha ya chuma/metali
-
Kupoteza uzito kiasi
-
Utumiaji wa pombe unaweza kuongeza uzalishaji wa kemikali ya lactic
-
Huwa haisababishi kushuka kwa sukari zaidi ya kiwango kinachotakiwa
Zingatia Jamii muhimu unapotumia dawa hizi
Wazee: tafiti zinaonyesha dozi kwa wazee inatakiwa kuwa chini ya asilimia 33 ukilinganisha na dozi inayotumiwa na mtu asiye mzee. Na endapo unaongeza dozi ongeza kwa kiwango kidogo wanza kuliko kwa mtu asiye mzee.
Tahadhari/madhara makubwa
Mgonjwa akipata kiwango cha juu cha tindikali ya lactic basi dawa isimamishwe hapohapo na mtaalamu afahamishwe kama unapata maumivu ya misuli, kuchoka mwili, kupumua haraka, sononeko lisilo la kawaid. Hizo ni moja ya dalili za kuongezeka kwa kiwango cha kemikali hii. Dawa hizi zikitumiwa pamoja na Pombe ongezeko la uzalishaji kemikali aside ya lactic huongezeka mara dufu. Mgonjwa hatakiwi kutumia pombe iliyozidi kiasi.
Haifai kutumia endapo
-
Udhaifu wa figo endapo kiwango cha kemikali itolewayo kwenye figo ikizidi kwenye damu kwa kiasi cha miligramu 1.5 kwa kila desilita au 1.5mg/dl, kwa wanaume na zaidi ya 1.4 kwa wanawake
-
Kuzidi kwa kiwango cha creatinine kutokana na tatizo lolote lile kama mshituko wa mwili, sumu za bakteria kwenye damu, kuziba kwa mishipa ya damu ilishayo moyo.
-
Ongezeko la asidi kutokana na uchakatuaji wa seli pamoja na DKA
-
Kufeli kwa moyo kunakohitaji dawa,kufeli kwa ini
​
Imeboreshwa 5/11/2018