top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

 

Maambukizi ya minyoo kwa watoto

 

Maambukizi ya mionyoo kwa watoto hutokea kwa asilimia kubwa kwenye nchi zinazoendelea, hata hivyo nchi zilizoendelea pia zina visa vya wagonjwa walio na maambukizi haya. Kuna aina nyingi za minyoo zinazofahamika kusababisha maambukizi kwa watoto na watu wazima. Katika Makala hii utajifunza kuhusu aina za minyoo, magonjwa yanayosababishwa, vipimo na matibabu pamoja na kinga dhidi ya kupata maambukizi ya minyoo hao.

 

Dalili za kuwa na maambukizi ya minyoo

 

Dalili za kuwa na maambukizi ya minyoo hutegemea aina ya mnyoo anayesababisha ugonjwa huo, aina za minyoo na magonjwa yanayosababishwa zimeelezewa hapa chini bonyeza aina ya mnyoo au ugonjwa ili kuusoma zaidi.

 

Dalili zilizoorodheshwa hapa chini zinahusisha dalili kutoka kwenye makundi yote ya aina za minyoo ambazo ni;

 

  • Kuwashwa au kupata harara kwenye ngozi - dalili ya kwanza ya maambukizi ya minyoo aina ya hookworm

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuhara

  • Kukosa hamu ya kula

  • Kupoteza uzito

  • Homa

  • Maumivu ya misuli

  • Kutetemeka mwili

  • Kuvimba kwa ini

  • Kushindwa kupitisha mkojo vema kwa maambukizi ya Schistosomiasis

  • Saratani ya kibofu cha mkojo pamoja na kupooza au kupata degedege kwa maambukizi ya muda mrefu ya Schistosomiasis

  • Uchovu mkali wa mwili

  • Upungufu wa damu mwilini

  • Kuchelewa au kurudi nyuma kwa maendeleo ya ukuaji wa mtoto

  • Kupata hamu ya kwenda haja kubwa mara kwa mara na maumivu wakati wa kupitisha kinyesi ambacho huwa na mrenda mrenda, majimaji au damu kwa maambukizi ya minyoo ya Whipworm

  • Kuchomoza kwa utumbo nje ya njia ya haja kubwa

  • Kuziba kwa utumbo- hutokea kwenye maambukizi ya ascariasis.

  • Kikohozi endapo vimelea wameingia kwenye mapafu haswa kwa ugonjwa wa Ascariasis

 

 

Aina ya maambukizi ya minyoo

 

Kuna aina nyingi za minoo zinazofahamika kusababisha magonjwa kwa binadamu. Baadhi ya magonjwa ya minyoo yanayotokea kwa binadamu ambayo husababishwa na minyoo ni;

 

  • Ascariasis

  • Ttrichuriasis

  • Hookworm

  • Enterobiasis

  • Schistosomiasis(kichocho)

  • Toxocariasis

  • Cysticercosi

  • Filariasis

 

Aina za mnyoo na ugonjwa anaosababisha

​

Baadhi ya ainaz a minyoo na ugonjwa unaosababishwa na mnyoo kwa binadamu ni;

​

  • Ascaris lumbricoides husababisha ugonjwa wa ascariasis

  • Trichuris trichiura (whipworm) husababisha ugonjwa wa trichuriasis

  • Ancylostoma duodenale (hookworm) husababisha ugonjwa wa ancylostomiasis

  • Necator americanus husababisha ugonjwa wa necatoriasis

  • Schistosoma haematobium husababisha ugonjwa wa schistosomiasis(kichocho cha mkojo)

  • Wuchereria bancrofti husababisha ugonjwa wa lymphatic filariasis

 

Njia za kupata maambukizi ya minyoo

 

Njia zilizoorodheshwa hapa chini ni njia za jumla zinazohusisha maambukizi ya minyoo aina mbalimbalio. Baaadhi ya njia ambazo watoto wanawez akupata maambukizi ya minyoo ni

 

  • Kupitia udongo ulio na minyoo mtu anaweza kupata maambukizi ya ascariasis, trichuriasis, hookworm na enterobiasis- minyoo wanaweza kupita kwenye ngozi au kwa njia ya kula ugongo wenye minyoo

  • Kupitia kuogelea kwenye madimbwi yenye maji yaliyosimama na yenye konokono, mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa wa schistosomiasis.

  • Kupitia kula chakula kisichoiva vema mfano nyama au kuishi na wanyama kama mbwa, paka mtoto au mtu mzima anaweza kupata minyoo aina ya toxocariasis na cysticercosis.

 

Vipimo

 

Ili kutambua minyoo kwa watoto ni lazima kwanza daktari atambue sehemu ambapo mnyoo yupo na aina ya kipimo ambacho kinafaa. Hata hivyo kipimo ambacho kinatumika kama kipimo tambuzi cha kuaminika ni kipimo cha kuangalia uwepo wa maambukizi ya minyoo kwenye kinyesi kupitia hadubini (microscopy), kipimo hiki huitwa stool microscopy.

 

Vipimo vingine ni pamoja na;

 

Kipimo cha serology- hupima kiwango cha kinga za mwili zenye jina la antibody zilizotengenezwa na mwili kupambana na minyoo. Huweza kutambua uwepo wa minyoo inayosababisha ugonjwa wa toxocariasis na strongyloidiasis. Kipimo hiki huwa kinafanyika kwenye maabara teule tu.

 

Kipimo cha Polymerase Chain Reaction- kipimo hiki huwa kizuri sana kuliko kipimo cha stool microscopy na serology kwenye utambuzi wa minyoo aina ya Ascariasis lumbricoides, Trichuris trichiura, Schistosoma,   na Ancylostoma duodenale. Hutumia kinyesi kutambua uwepo wa vimelea hawa, huwa na ufanisi sana na ni kipimo ambacho kinaongezeka kuaminiwa na kutumiwa zaidi

 

Matibabu

 

Matibabu ya minyoo yaliyopo yanaweza kuhusisha kupewa kinga kabla ya kupata ugonjwa au tiba ya ugonjwa uliokwisha tokea. kinga hufanyika kwa watoto wote walio kwenye nchi ambazo zina maambukizi ya hali ya juu hususani nchi za bara la Afrika na Ulaya, kwa Tanzania Kinga ya ugonjwa wa minyoo hutolewa wakati wa kliniki na kwa mashuleni.

​

Mababu ya kujikinga

​

Kumbuka Dawa za kinga hutegemea aina ya minyoo na hutolewa na daktari mwenye kibari cha kuandika dawa hiyo, hata hivyo baadhi ya kinga kwenye aina za minyoo ni pamoja na;

​

  • Schistosomiasis- kinga yake ni praziquantel

  • Strongyloidiasis- kinga yake ni  ivermectin au albendazole

 

Matibabu tiba

 

Dawa za kutibu na minyoo huandikwa na kutolewa na daktari, hakikisha umewasiliana na daktari wako kwa utambuzi wa shida yako na kupata matibabu sahihi. Baadhi ya matibabu ya ugonjwa wa minyoo yaliyopo kutokana na ugonjwa ni;

​

  • Ascariasis- Albendazole au mebendazole au ivermectin kama dawa daraja la pili

  • Trichuriasis- Albendazole au mebendazole au ivermectin kama dawa daraja la pili

  • Maambukizi ya Hookworm-  Albendazole au mebendazole au Pyrantel pamoate kama dawa daraja la pili

  • Strongyloidiasis- ivermectin au albendazole kama dawa daraja la pili

  • Enterobiasis- Albendazole au mebendazole au Pyrantel pamoate kama dawa daraja la pili

  • Schistosomiasis- praziquantel au oxamniquine kama dawa daraja la pili

  • Toxocariasis- Albendazole

  • Cysticercosis- albendazole au praziquantel kama dawa darala la pili

 

Kinga

 

Kujikinga na maambukizi ya minyoo au kuwakinga watoto wasipate maambukizi unaweza kufanya mambo yaliyoorodheshwa hapa chini. Hata hivyo kinga hutegemea aina ya minyoo, hivyo kusoma zaidi kuhusu kinga ya aina fulani ya monyoo ni vema ukabonyeza aina ya mnyoo na kusoma kwenye kiopengele cha kinga. Baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kujikinga ni pamoja na;

 

  • Usitembee miguu tupu (hakikisha umemvalisha mtoto viatu ili kuepuka kupata maambukizi kutoka kwenye udongo kupitia vimelea wanaopita kwenye ngozi haswa katika maeneo yenye maambukizi ya juu

  • Zua udongo ulio na vimelea usiguse ngozi endapo upo kwenye maeneo yenye maambukizi ya hali ya juu

  • Tumia choo - endapo watu watatumia vyoo vya shimo kujisaidia au kutupa kinyesi badala ya kutupa au kujisaidia kwenye vichaka au katika mazingira ambayo watu wanapafikia, hii itasaidia kutoacha vimelea hao karibu na mazingira ya watu hivyo kupunguza maambukizi.

  • Usitumie kinyesi cha binadamu kama mbolea kwenye shamba lako ili kuzuia kupata maambukizi kutoka kwenye kinyesi hicho unapokuwa unatembea kwenye shamba lako.

  • Upuka tabia ya kula udongo au usimwache mwanao ale udongo ambao una kinyesi cha binadamu au ule uliotengenezwa kutokwa kwenye udongo ambao ulikuwa na mbolea ya kinyesi cha binadamu au kugusana na majimaji ya kinyesi cha binadamu

  • Nawa mikono yako kwa kutumia sabuni na maji ya uvuguvugu kabla ya kuanza kuandaa au kula chakula

  • Wafundishe watoto wako umuhimu wa kunawa mikono ili kujikinga na maambukizi mbalimbali

  • Safisha mboga au matunda vema kabla ya kula haswa yale ambayo yamezalishwa kwenye maeneo ambayo wanatumia mbolea ya kinyesi cha binadamu

  • Kwa wale wanaofunga nguruwe, hakikisha watoto wanaposhika wanyama hao au kinyesi au udongo wa wanyama hao hawaweki mikono kwenye kinywa kabla ya kunawa mikono hiyo.

 

Imeboreshwa 10.01.2021

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile mara baada ya kusoma makala hii.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' Chini ya tovuti hii.

​

​

  1. Jill E. Weatherhead and Peter J. Hotez . Worm Infections in Children.. Imechukuliwa 09.01.2021

  2. Andrea J. Lack, MD etal. Helminth Infections in Neonates and Young Children. https://www.medscape.com/viewarticle/827262_2. Imechukuliwa 10.01.2021

  3. https://www.cdc.gov/parasites/hookworm/. Imechukuliwa 10.01.2021

  4. https://www.cdc.gov/parasites/hookworm/gen_info/faqs.html. Imechukuliwa 10.01.2021

  5. Parasites - Trichuriasis (also known as Whipworm Infection). https://www.cdc.gov/parasites/whipworm/index.html. Imechukuliwa 10.01.2021

  6. Ascariasis. https://www.cdc.gov/parasites/ascariasis/index.html. Imechukuliwa 09.01.2020

  7. Schistosomiasis. https://www.cdc.gov/parasites/schistosomiasis/index.html. Imechukuliwa 09.01.2021

  8. Schistosomiasis. http://who.int/topics/schistosomiasis/en. Imechukuliwa 10.01.2021

  9. Schistosomiasis (Bilharziasis) Control Program. Imechukuliwa 09.01.2020https://www.cartercenter.org/health/schistosomiasis/index.html. Imechukuliwa 10.01.2021

bottom of page