top of page

Kuvimba Mitoki- Matibabu ya nyumbani

​

Mwandishi:  Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri: Dkt. Peter A, MD

​

Imeandikwa 10/2/2019

​

Utangulizi

​

Kama mitoki ama tezi limfu zimevimba na zinasababisha maumivu zenyewe ama zikishikwa unaweza kufanya mambo yafuatayo;

 

Weka hali ya ujoto- kanda mitoki kwa kitambaa kilichochovywa kwenye maji ya ya uvuguvugu.

 

Tumia dawa za maumivu- Dawa baridi za kupunguza maumivu kama aspirini, ibuprofeni na paracetamol huweza tumika kushusha homa na kupunguza maumivu. Kumbuka dawa hizi hazitibu sababu bali huondoa dalili na pia usimpe mtoto wako aspirini bila kusahuriwa na daktari wako kwa sababu inaweza kusababisha tatizo lijulikanalo kama raye's syndrome-Tatizo hili huweza kuathiri damu, ini na ubongo wa mtoto aliye na maambukizi ya virusi na huweza kuleta madhara makubwa.

 

Pumzika vya kutosha- mara nyingi unatakiwa kupumzika ili kuruhusu kusafishwa kwa maambukizo katika mitoki

 

Mwisho usisahau kumwona daktari kwa matibabu zaidi

​

Wapi utapata maelezo zaidi?

​

Soma maelezo zaidi kuhusu kuvimba mitoki kwenye linki zinazofuata:

​

​

Toleo la 3

Imeboreshwa 06/06/2022

bottom of page