Henia/Ngiri kokoto Hernia kwa watoto na watu wazima
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
Hernia ni tatizo linalotokea kwa wanaume sana ukilinganisha na kwa wanawake. Tatizo hili hutokea sehemu ya kuta za tumbo ambapo kuna udhaifu katika kuta hizo na hivo husababisha vilivyopo ndani ya tumbo kupita katika kuta dhaifu na kuonekana kama uvimbe ama kuzalisha dalili za maumivu kwa mgonjwa ama kutopata choo kikubwa.
Zipo aina nyingi za hernia kama vile hernia inayotokea kwenye kitovu, korodani, ama chini ya kitove
Vihatarishi vya kupata hernia
-
kuongezeka kwa shinikizo ndani ya tumbo
-
Kuwepo kwa udhaifu kwene kuta za tumbo
-
kuwepo kwa udhaifu ndani ya tumbo pamoja na Kuongezeka kwa shinikizo ndani ya tumbo
-
Kukenya wakati wa kutoa haja kubwa ama ndogo, Ama kuwa kupitisha choo kigumu sana
-
Kunyanyua mizigo mizito
-
Maji wenye tumbo
-
Ujauzito
-
Uzito kupita kiasi
-
Tatizo sugu la kukohoa ama kupiga chafya
-
Kuzaliwa njiti
-
Historia ya kuwa na hernia ama histria ya hernia kwenye familia
-
Kuwa mwanaume -Kufanya kazi nzito
-
Kusimama mda mrefu sana
-
Kuwa na magonjwa fulani kama ya mapafu ama magonjwa ya kurithi kama cystic fibrosis
Dalili za hernia
-
Kuvimba kwenye maeneo juu ya mavuzi
-
MAumivu ya kuungua, muungurumo na kuumi kwenye uvimbe uliojitokeza
-
Maumivu ama kutojisiki vema kwenye sehemu za siri kwa mfano ukiwa unainama, kukohoa ama kunyanyua kitu
-
Kuhisi mzigo mzito sehemu za siri
-
Kuhisi msukumo kwenye sehemu za siri
-
Wakati mwingine kuvimba kwenye korodani kunakosababishwa na kuingia kwa utumbo kwenye kifuko cha korodani
Daliliz za hernia iliyoziba
herni isiyoweza kurudi ndani mara baada ya kujitokeza huitwa hernia iliyoziba ama incacerated hernia. Aina hii ya heni inaweza kupelekea kuoza kwa sehemu ya utumbo kutokna na kukosekana kwa damu kwa sababu aina hii ya hernia huweza kujisokota
​
​
Dalili zake huwa hizi zifuatazo
-
kicefuchefu, kutapika au vyote viwili
-
Homa
-
Mapigo ya moyo kwenda kasi
-
Maumivu ya ghala yanayoongezeka kwa haraka
-
Uvimbe wa hernia kubadilika rangi kuwa wa zambarau au wekundu
Matibabu
Matibabu makubwa ya hernia mara nyingi huhusisha upasuaji wa kurekebisha udhaifu ulio katika kuta za tumbo
Hakuna matibabu ya dawa ambayo yanaweza kuondoa tatizo la hernia
​
​
Toleo la 4
Imeboreshwa 8/2/2019