top of page

Kinga ya Gono

Updated: Nov 6, 2021

Namna ya kujikinga na gono


Gono ni ugonjwa mojawapo ulio katika magonjwa ya zinaa, huambukizwa kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye ugonjwa huo. Maambukizi ya gono kwenye koo na njia ya haja kubwa hutokea endapo mtu atagusana na vidonda au majimaji yenye maambukizi au kushiriki kujamiana kinyume na maumbile. Makala hii inazungumzia Zaidi kujikinga na ugonjwa huu wa gono


Gono mara nyingi huwa haiambatani na dalili yoyote ile kwa wanawake, ndio maana mara nyingi wanawake wenye ugonjwa huu huweza kuona kama vile wana UTI ndogo tu bila kufikiria kuwa wana ugonjwa huu wa gono.


Dalili zinazoweza kutokea kwa wanawake hata hivyo ni;


 • Kutokwa na uchafu wa njano ukeni

 • Maumivu wakati wa kukojoa

 • Kukojoa mara kwa mara

 • Kutokwa na damu ukeni katikati ya mwezi

 • Maumivu ya tumbo la chini

 • Kutokwa na damu njia ya haja kubwa kwa wale wanaoingiliana kinyume na maumbile

 • Kutokwa na uchafu njia ya haja kubwa kwa wale wanaoingiliana kinyume na maumbile

 • Maumivu kwenye njia ya haja kubwa kwa wale wanaoingiliana kinyume na maumbile

Kwa wanaume


Dalili za mwanzo ni muwasho katika tundu la njia ya mkojo

 • Maumivu ya kuungua njia ya mkojo wakati wa kukojoa

 • Kutokwa na usaha kwenye njia ya mkojo

 • Kushindwa kabisa kupitisha mkojo

 • Kupitisha mkojo kwa shida ambapo itakua inazidi kadri siku zinavyoenda

 • Kuonekana kwa damu kwenye mkojo

 • Maumivu ya pumbu upande mmoja

 • Kuvimba kwa pumbu upande mmoja

Vipimo


Hakuna haja ya kufanyia kipimo endapo utakuwa na dalili zinazoelezea tatizo hili. Hata hivyo vipimo vinavyoweza kufanyika ili kutambua gono ni pamoja na

 • Kipimo cha culture ya majimaji ya maambukizi kutoka ukeni au kwenye uume

 • Kipimo cha gramu stain

Matibabu ya gono


Gono hutibiwa kwa matumizi ya dawa zinazoitwa antibayotiki, kwa mujibu wa miongozo ya matibabu kwa Tanzania, mgonjwa ataanza kutumia dawa za vidonge kwanza na endapo zikishindikana atatumia dawa ya kuchoma ikifuatiwa na vidonge. Mpenzi wako pia atatakiwa kutumia dawa hizi ili kuzuia kupata maambukizi tena kutoka kwake kwa mara nyingine, endapo una wapenzi wengi ni vema wote pia wakatibiwa.

Madhara


Endapo ugonjwa huu hautatibiwa unawez akuleta madhara sawa na magonjwa mengine ya zinaa ikiwa pamoja na;


Kwa wanawake

Kwa wanaume


 • Kuharibika kwa njia ya kupitisha mkojo na shahawa

 • Ugumba

Namna ya Kujikinga na gono

Ili uweze kujikinga na gono ni vema kuzingatia mambo yafuatayo

 • Kutokufanya ngono zembe

 • Epuka mahusiano ya mpenzi zaidi ya mmoja

 • Epuka kujamiana na mtu wmenye vidonda aina yoyote sehemu za siri

 • Endapo una shiriki sana ngono, hakikisha kila mwaka unapima maambukizi ya gono

 • Muulize mpenzi wako endapo ameshawahi kuugua gono, pata vipimo na matibabu kwa pamoja

 • Fahamu na fanya Matumizi sahihi ya kondomu

 • Unapopata dalili za Gono wahi ukapimwe ili ugonjwa ugunduliwe na kutibiwa mapema bila kuleta madhara.

 • Endapo umetambulika kuwa una gono, hakikisha wapenzi wako wote wanatibiwa kwa kuwa wasipotibiwa watakuambukiza tena

 • Penda kujisomea kuhusu magonjwa ya zinaa ili kupata elimu zaidi na Zaidi

Rejea za mada hii

 1. ACOG. Chlamydia, gonorrhea and syphilis. https://www.acog.org/womens-health/faqs/chlamydia-gonorrhea-and-syphilis. Imechukuliwa 10.11.2020

 2. ULY CLINIC. Gono. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-Gono. Imechukuliwa 10.11.2020

 3. MSD. Gonorrhea. https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/sexually-transmitted-diseases-stds/gonorrhea?. Imechukuliwa 10.11.2020

 4. ULY CLINIC. Ugumba. https://www.ulyclinic.com/ugumba. Imechukuliwa 10.11.2020

375 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page