Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Tatizo la Ugumba
Utangulizi
​
Kama kupata mimba imekuwa ni changamoto kwako na mpenzi wako, basi jua kuwa hauko peke yako na tatizo hili. Asilimia kumi hadi 15 ya wanandoa Duniani ni wagumba (tasa). Utasa huelezewa kuwa ni tatizo la kutokuwa na uwezo wa kupata mimba licha ya kuwa unashiriki tendo la ndoa pasipo kutumia kinga au njia za uzazi wa mpango angalau kwa mwaka mmoja au baada ya miezi sita kwa baadhi ya watu.
Utasa unaweza kusababishwa na sababu moja ama nyingi zilizo kati yako wewe na mpenzi wako, au mchanganyiko wa mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuzuia mimba kutungwa au kuendelea. Kwa bahati nzuri, kuna matibabu mengi ya usalama, ufanisi na Msingi kwa ajili ya kukabiliana utasa-ugumba. Matibabu haya kwa kiasi kikubwa huboresha ama kurudisha nafasi yako ya kuwa mjamzito
Dalili za Ugumba-Utasa
Wapenzi wengi walio wagumba, hupata mimba ndani ya miezi sita ya kwanza ya kujaribu kutafuta mimba baada yha ushauri kutoka kwa daktari. Kwa ujumla, baada ya miezi 12 ya kujamiiana mara kwa mara bila kinga, asilimia 90 yawanandoa hupata mimba. Wengi wa wanandoa wenye ugumba huweza kupata mimba bila matibabu yoyote
Ishara kuu ya utasa ni kukosa uwezo kwa wanandoa kupata mimba.
Mara nyingi hakuna dalili za wazi ama za kuonekana zinazomsema mtu kuwa anaugumba
Baadhi ya wagumba wanaweza kuwa na hedhi ya kawaida au kutokwenda hedhi kabisa. Mwanaume mgumba anaweza kupata dalili za kuharibika kwa usawia wa uzalishaji vichochezi vya uzazi (homoni) kama vile mabadiliko katika ukuaji wa nywele, mabadiliko ya kijinsia, kupungua hamu ya tendo la ndoa, au kuwa na matatizo ya umwagaji wa mbegu kwa mwanaume. Mwanaume pia anaweza kuwa na korodani ndogo au uvimbe katika kifuko cha kutunzia mbegu.
Nini husababisha Utasa-Ugumba?
Ili kuwa na mimba, michakato tata ndani ya mwili inayohusisha utoaji,usafilishaji na uchavushaji wa yai la kike kwa manii hutakiwa kufanya kazi yake ipasavyo pasipo makosa. Kwa baadhi ya wanandoa, matatizo yanayosababisha utasa huweza kuwa yameanza tangu kuzaliwa (congenital) kwa mtu au kupata ukubwani kutokana na mfumo wa uzazi kupata magonjwa au kitu chochote kinachoharibu utendaji kazi wa mfumo wa uzazi.
Sababu zinazosababisha utasa zinaweza kuwa zinatokana na mwanamke au mwanaume huku kila mmoja akichangia asilimia kadhaa
Tafiti zinaonyesha kwamba, zaidi ya theluthi moja ya sababu za utasa hutokana na mwanaume na theluthi moja nyingine hutokana na sababu za mwanamke na zilizobaki huchangiwa sawa sawa na mwanamke na mwanaume
Sababu zinazosababisha Utasa kwa Mwanaume
Sababu za mwanaume zinazoweza kusababisha utasa ni;
-
Uzalishaji au ufanyaji kazi wa manii Usiokuwa wa kawaida kutokana na matatizo mbalimbali, kama vile korodani kutoshuka chini na kuonekana nnje ya mfuko wa kutunzia korodani(pumbu), kasoro za maumbile ya uume na mfumo wa uzazi wa kiume, matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari, magonjwa kama vile ngiri maji, majeraha au kufanyiwa upasuaji wa korodani au maeneo ya kinena.
Mishipa inayotoa damu kutoka kwenye korodani (vein) ikivimba huongeza kiasi cha damu na joto kwenye korodani na hivyo huathiri idadi na sura yambegu.
-
Matatizo ya utoaji wa mbegu-shahawa wakati wa kujamiiana, kama vile kumwaga shahawa mapema, shahawa kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje ya uume wakati wa kufika kileleni, baadhi ya magonjwa ya kuzaliwa, kama vile mitungo ya maji au kusinyaa kwa mirija ya kupitisha mbegu za kiume, kuzibwa kwa mirija ya kutoa mbegu kwenye korodani na kuleta nje ya uume, au uharibifu au kuumia kwa viungo vya uzazi.
Wanaume ambao hapo awali alifunga kizazi kwa kukatwa mirija ya kupitisha mbegu hawezi kupata mtoto mpaka mirija hiyo ifunguliwe kwa upasuajiau au kwa kutolewa mbegu katika korodani na kuwekwa kwa mwanamke ili apate mimba.
-
Kutumi au kukaa karibu na kemikali na sumu aina fulani , kama vile baadhi ya madawa, mionzi, tumbaku moshi, pombe, bangi, na dawa aina ya steroids (ikiwa ni pamoja Testosterone yenyewe). Aidha, kukaa karibu na joto mara kwa mara, kama vile kukaa katika maji ya moto wakati wa kuoga kunaweza kuinua joto ndani ya korodani(pumbu) hivyo kuathiri uzalishaji mbegu.
-
Uharibifu unaosababishwa na saratani au dawa za kutibu saratani kwa njia ya mionzi. Matibabu ya saratani yanaweza kuharibu tendo la uzalishaji mbegu, wakati mwingine matibabu hayo huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume kwa kiwango kikubwa sana. Kuondolewa korodani kutokana na saratani huathiri uzalishaji wa mbegu pia
Sababu za Ugumba-Utasa kwa mwanamke
Sababu za utasa wa kwa mwanamke ni pamoja na:
-
Matatizo ya utoaji mayai, ambayo huzuia mayai kutoka kila mwezi. Mifano ni pamoja na matatizo ya homoni yanayoweza kusababishwa na Matatizo kadhaa kama vile tatizo la Polisistiki ovariani sindromu- hali ambayo inaweza sababisha ovari zako kuzalisha kwa wingi sana vichochezi vya uzazi vya kiume yaani homoni ya Testosterone na prolactine-inayofanya kazi ya kuzalisha maziwa. Sababu nyingine za msingi zinazoweza kusababisha tatizo hili ni pamoja na kufanya mazoezi makali kupita kiasi , matatizo ya kula, jeraha-kuumia au uvimbe ndani ya kizazi.
-
Matatizo katika mfuko wa uzazi, njia za uzazi na mlango wa uzazi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kutofunguka kwa shingo ya uzazi wakati wa kujamiiana kwa sababu ya ute mzito unaoziba shingo ya uzazi ili chochote kiziingie ndani ya uzazi ikiwemo mbegu za kiume, matatizo ya umbo au kuta za ndani ya uzazi.
​
-
Vimbe za fibroid zisizo saratani ndani ya mfuko wa uzazi ni vimbe zinazotokea sana kwa wanawake wengi na vimbe hizi huwa hazisababishi kwa kiasi kikubwa tatizo la ugumba. Vimbe hizi mara chache zinaweza kusababisha ugumba kama zikikua na kuziba mirija ya uzazi inayopitisha mayai kutoka kwenye ovary na kwenda kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Mara kadhaa, vimbe hizi za fibroids zinaweza kuharibu kuta za uzazi na hivyo yai lililochavushwa hushindwa kujipandikiza na kuendelea kukua ndani ya mfuko wa kizazi.
-
Kuziba au kuharibika kwa mirija ya kupitisha mayai, ambapo kwa mara nyingi tatizo hili hutokana na kuvimba kwa mirija hii kwa sababu ya maambukizi kwenye mirija(salpingitis). Maambukizi haya husabaisha magonjwa ya kuungua kwa mfuko wa uzazi yaani (pelvic inflammatory diasease). Maambukizi haya yanaoweza kufika kwenye mfumo wa uzazi ni yale magonjwa ya zinaa
​
-
Tatizo jingine lina sababishwa na kujipandikiza kwa kuta za ndani ya uzazi nnje kizazi yaani endometriosis, tatizo hili husababisha kuungua kwa maeneo ambapo kuta hizi zimejipandikiza hatimaye kuziba kwa mirija ya uzazi
-
Uzalishaji duni wa homoni zinazotolewa na ovary,- tatizo hili hutokea kwa baadhi ya wanawake, uzalishaji wa vichochezi vinavyotolewa na ovari huwa kwa kiwango kidogo au kutozalishwa kabisa kabla mwanamke hajafikia umri wa miaka 40 na wanawake hawa huwa na dalili ya hedhi kukoma mapema zaidi kuliko wanawake wengine ambao huanza kipindi cha komahedhi hedhi kuanzia miaka 45. Ingawa sababu zinazosababisha tatizo hili la uzalishaji duni wa homoni mara nyingi hazijulikani, lakini hali fulani zinasemekana husababisha tatizo hili ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mfumo wa kinga mwilini, mionzi au dawa za kutibu saratani, na uvutaji wa sigara.
-
Makovu kwenye kuta za uzazi, mikunjo ya tishu na makovu yanayotokea baada ya maambukizi ya viungo vya uzazi, maambukizi ya kidole tumbo, au kufanyiwa upasuaji unaohusishaa tumbo na viungo vya uzazi husababisha mishikamano ndani ya mfumo wa uzazi na hivyo kuweka mazingira yasiyopendeza kwa ajiri ya yai lililochavushwa kujipandikiza na hivyo huleta tatizo la ugumba
Sababu zingine kwa wanawake ni pamoja na:
-
Matatizo ya tezi. Matatizo ya tezi ikiwa pamoja na tezi shingo endapo inazalisha kichochezi cha homoni ya thyroid kwa kiwango kikubwa yaani au kidogo sana huweza kuharibu mzunguko wa hedhi au kusababisha utasa.
-
Saratani na tiba zake. Baadhi ya saratani hasa saratani za mfumo wa uzazi - mara nyingi husababisha matatizo ya uzazi. Dawa za kutibu saratani na mionzi inaweza kuathiri uwezo wa mwanamke wa kuzaa
-
Magonjwa mengine. Magonjwa yanayosababisha mtu kuchelewa kubarehekama vile kama vile ugonjwa wa celiac, ugonjwa wa Cushing, ugonjwa wa seli mundu, ugonjwa wa figo au kisukari, huweza kuathiri uzazi wa mwanamke. Pia matatizo ya maumbile yanaweza kusabaisha kutungwa au kukua kwa mimba kwa shida sana.
-
Baadhi ya dawa. Baadhi ya madawa huweza kusababisha utasa kwa muda, endapo dawa hizi zitasimamishwa kutumika basi tatizo hili linaweza kuisha baada ya muda. Dawa hizi mfano wake ni zile dawa za uzazi wa mpango.
​
Vihatarishi vya kupata ugumba kwa mwanamke na mwanaume
Sababu nyingi zinazosababisha utasa kwa mwanamke na mwanaume hufanana. Sababu hizo ni pamoja na:
-
Umri. Uzazi wa mwanamke (uwezo wa kupata mimba) hupungua hatua kwa hatua kulingana na umri unavyoongezeka hali hii huzidi zaidi katika umri baada ya kufikisha miaka 30. Utasa kwa wanawake wenye umri mkubwa huweza kutokana na idadi au ubora wa mayai yanayozalishwa. Umri mkubwa pia huambatana na matatizo ya afya katika viungo vya uzazi. Wanaume wenye umri chini ya miaka 40 huwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya wale walio zaidi ya umri wa miaka 40.
-
Matumizi ya tumbaku. Nafasi ya wanandoa kupata mimba hupunguzwa kama mpenzi anatumia tumbaku. Sigara pia huharibu matibabu ya Matatizo ya uzazi kwa wale wanaotafuta kupata mtoto. Mimba kutoka ama kuharibika hutokea mara nyingi zaidi kwa wanawake wanaovuta sigara. Sigara inaweza kupunguza uwezo wa uume kusimama na pia husababisha uzalishaji mdogo wa manii
-
Matumizi ya pombe . Kwa wanawake, hakuna kiwango cha usalama cha matumizi ya pombe wakati wa kubeba mimba au kulea mimba. Epuka pombe kama unatarajia kupata mimba wiki mbili kabla hujapata mimba. Matumizi ya pombe huongeza hatari na kasoro za uzazi na mtoto, na pia inaweza kusababisha ugumu zaidi wa kupata mimba. Kwa wanaume, matumizi makubwa ya pombe huchangia kupunguza kiwango cha manii na uwezo wa manii kukimbia kwa kasi kuelekea kwenye yai mara inapomwangwa kwenye uke.
​
-
Kuwa na uzito mkubwa zaidi(unene) Uzito kupita kiasi huongeza hatari ya kupata utasa. Aidha, shahawa za mwanamume huwa kwa kiasi kidogo sana kwa wanaume wanene.
-
Kuwa na uzito wa chini sana. Wanawake walio katika hatari ya matatizo ya uzazi ni pamoja na wale wenye matatizo ya kula, kama vile anorexia au bulimia, na wanawake ambao hutumia kiwango kidogo cha kalori katika chakula(kutumia chakula chenye nguvu kidogo)
​
-
Masuala ya mazoezi. Kutofanya mazoezi ya kutosha inachangia kuongezeka uzito na kuweza kusababisha tatizo la utasa. Kwa mara chache sana mazoezi kupita kiasi huchangia kuleta matatizo ya hedhi na ugumba.
​
Wasiliana na daktari wako kwa tiba na ushauri zaidi kabla ya kuchukua maamuzi yoyote kwenye makala hii
​
Unaweza kupata tiba kutoka kwa daktai wa wanawake wa ulyclinic sasa, bonyeza hapa
​
Toleo la 5
Imeboreshwa 29.01.2022
​
Rejea
​
-
Williams Gynecology toleo la &
-
Duta Textbook of Gynecology toleo la 20
​
Sehemu hii utasoma kuhusu
​
Vipimo
​
​