Maambukizi ya kirusi cha HPV mara nyingi husababisha maoteo kwenye ngozi ya ndani na nje ya mwili
Baadhi ya aina fulani ya virusi vya HPV husababisha saratani hatari ikiwepo pamoja na saratani ya koo, njia ya haja kubwa, uume, uke na mashavu ya uke na shingo ya kizazi. Maambukizi haya yamekuwa yakihusiana na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Ikumbukwe kuwa kuna ina zaidi ya 100 ya virusi vya HPV vinavyofahamika duniani, licha ya kuwa na aina hizo nyingi baadhi yao huwa hawasababishi magonjwa na baadhi husababisha magonjwa mbali na saratani ikiwa pamoja na maoteo sehemu za siri, kweney kanyagio na kwenye viganja vya mikono, kuleta malengelenge kwenye ngozi n.k
Comments