top of page

Maambukizi  ya kirusi cha HPV

​

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

​

Utangulizi

​

Maambukizi ya kirusi cha HPV mara nyingi husababisha maoteo kwenye ngozi na sehemu zenye ute ute

Baadhi ya aina fulani ya virusi vya HPV husababisha saratani hatari ikiwepo pamoja na saratani ya koo, njia ya haja kubwa, uume, uke na mashavu ya uke na shingo ya kizazi. Maambukizi haya yamekuwa yakihusiana na maambukizi ya virusi vya ukimwi

Ikumbukwe kuwa kuna aina zaidi ya 100 ya virusi vya HPV vinavyofahamika duniani, licha ya kuwa na aina hizo nyingi baadhi ya virusi huwa hawa sababishi magonjwa na baadhi husababisha magonjwa mbali na saratani ikiwa pamoja na maoteo sehemu za siri, kweney kanyagio na kwenye viganja vya mikono, kuleta malengelenge kwenye ngozi n.k

 

Dalili za maambukizi ya kirusi huyu

Wakati mwingi mwili huweza kupambana na maambukizi haya na kuyaondoka kikamilifu endapo kinga ya mwili inajiwezza. Maoteo yanapotokea kwenye ngozi huweza kuwa ya aina tofauti ikitegemea ni aina gani ya kirusi cha HPV amesababisha maoteo hayo

Maoteo sehemu za siri, kwenye viganja, kwenye kanyagio n.k

​

Hutokea sana kwenye mashavu, njia ya haja kubwa, shingo ya kizazi na uke kwa wanawake na kwenye uume, mapumbu na maenezo ya kuzunguka haja kubwa kwa wanaume. Maoteo haya huwa na umbo kama la uyogaunaoota juu ya miti, wakati mwingine kama vichunusi virefu sana vyenye umbo lisilo laini

​

Saratani ya shingo ya kizazi

Mtu anapata dalili za saratani ya shingo ya kizazi, mara nyingi kirusi cha HPV namba 16 na namba 18 kinahusika katika kusababisha saratani kwa asilimia zaidi ya 70

​

Visababishi

Kirusi cha HPV anaingia mwilini kwa njia yangozi iliyopasuka kwa michubuko, kukatwa au kuchomwa majeraha yoyote yale. Kirusi husafirishwa kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia kugu sana ngozi na mtu aliyeathiriwa na kirusi huyu

Kirusi cha HPV anayesababisha maambukizi sehemu za siri huambukizwa kwa njia ya tendo la kujamiiana kwa njia ya uke, mdomo au haja kubwa.

​

Vihatarishi

​

  • Umri

Hutokea sana kwa watoto na vijana wadogo

​

  • Kinga ya mwili kuwa chini

Wakati wa ujauzito maoteo haya yanaweza kukua zaidi kutokana na kinga ya mwili kuwa chini na kusababisha shida kupitisha mtoto, na mara zingine maoteo yakiwa nje ya uke huwa hayahitaji matibabu mpaka mama ajifungue

Watu wenye maambukizi ya UKIMWI huwa hatarini kupata maambukizi ya HPV mara nyingi zaidi kuliko watu wa kawaida wasio na virusi vya ukimwi(VVU)

​

  • Ngozi iliyobomoka

Ngozi kupasuka au kuchanika kutokana na kujikana au kwa sababu yoyote huwa na hatari ya kupata maoteo kwenye maeneo hayo kwa sababu ya kirusi huyu wa HPV

​

  • Kugusana na mtu mwenye maambukizi haya

Kwa kuogelea kwenye swimming pool bila kuwa na vifaa zuizi vya kirusi hao ambapo huenda kuna mtu mwenye virusi hao wameogelea pia, kushika milango iliyoshikwa na mtu mwenye virusi hawa(vyoo vya jamii haswa ambavyo hutumiwa na watu weengi)

​

  • Idadi ya wapenzi

Kuwa na idadi kubwa ya wapenzi huwmeka mtu hatarini sana kupata maambukizi ya HPV. Epuka kuwa na mpenzi mwenye wapenzi wengi au kuwa na idadi ya wapenzi wengi.

 

Madhara

Madhara yanaweza kuwa kupata vinyama na vidonda kwenye tezi za tonsil, mdomoni kwenye koo na puani. Madhara makubwa kabisa ni saratani mbalimbali zikiwa pamoja na saratani ya shingo ya kizazi.

​

Kujikinga

Kujikinga na virusi vya HPV wa mikononi visisambae kwenye kinywa epuka kung’ata kucha au vidole. Usishike kidole kilichoathiriwana virusi hawa kwani maambukizi yatahamia sehemu nyingine ya mwili.

Maambukizi kwenye miguu yanaweza kuzuilika kwa namna fulani kwa kucaa viatu au ndala hasa unapokuwa kwenye maji maji yanayokanyagwa na watu wengi

​

Maambukizi ya kirusi maeneo ya siri yanaweza kuzuilika kwa kupunguza idadi ya wapenzi wengi na kuwa na mpenzi ambaye amepima na hana virusi hawa

​

Mwisho wa yote unaweza kupata chanjo dhidi ya kirusi huyu. Watu wanaoweza kupata chanjo ni hii ni wale 9 hadi 14 ambao bado hawajaanza kushiriki tendo la kujamiiana. Kwa Tanzania chanjo hii imeanza kutolewa kwa mabindi tu ili kuwakinga dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.

Shirika la chakula USA limeruhusi matumizi ya chanjo hii kwa watu wenye umri kuazia miaka 9 hadi 45

 

 

Utambuzi na vipimo

Utambuzi huanzia kwenye historian a kuangaliwa kwa maoteo sehemu mbalimbali na daktari wako. Baada ya uchunguzi awali basi dakatari ataagiza kuchukuliwa kwa vinyama kwa kukatwa ili kwenda kuvipima Vinasaba kuangalia ni aina gani ya kirusi. Kwa virusi walio kwenye shingo ya kizazi daktari atachukua vinywama na kufanya kipimo cha PAP ili kuona kama chembe za shingo ya kizazi zimebadilika na kuwa na sifa za saratani

​

Kuna kipimo cha kutumia tindikali ambapo ikiwekwa kwenye maoteo huyafanya yawe meupe na hizo kumjuza daktari kwamba maoteo hayo yanatokana na virusi vya HPV

 

Matibabu

Matibabu yapo ya aina mbalimbali ili kuondoa maoteo shemu mbalimbali za mwili. Mfano wa dawa ni hizi zifuatazo

  • Salicylic acid

  • Imiquimod (Aldara, Zyclara)

  • Podofilox (Condylox)

  • Trichloroacetic acid

​

Matibabuupasuaji

​

Matibabu haya hufanyika kukatamaoteo ambayo ni makubwa sana, huhusisha kukausha maoteo hayo, kuyakata kwa mwanga mkai au kuyagandisha kisha kuyatoa kirahisi

​

Toleo la 3

Imeboreshwa 15/2/2019

bottom of page