Ukiwa kwenye hali ya furaha na umetulia kimawazo wengine wanaita umeridhika, mwili huongeza uzalishaji wa kinga dhidi ya maradhi na uzito, hata hivyo unatakiwa kuwa na uzito wa kiafya.
Kinachoshangaza ni kwamba Tendo la ndoa linapofanyika kwa madhumuni ya afya huleta faida nyingi zikiwa hizo zilizotajwa hapo juu na zaidi na zaidi. Jambo hili linashangaza watu wengi, bila shaka tendo la ndoa na mapenzi huzungumziwa kila mahari katika vyombo vya habari. Ujumbe ni kwamba sisi ni viumbe tulioumbwa kushiriki tendo la kujamiiana na tendo la ndoa huongeza thamani na maana ya maisha.
Sasa tuangalie faida za kiafya za tendo la kujamiiana na upate kufunguwa macho yako kwa mtazamo mwingine. Faida za tendo la kujamiiana katika mwili huwa pamoja na kupunguza shinikizo la damu. Kutokana na utafiti uliofanyika huko Scotland ililipotiwa katika gazeti la Biology and Psychology.
Wanawake 24 na wanaume 22 walio weka kumbukumbu la shinikizo la damu kabla na baada ya kujamiiana, kuwekwa katika mazingira yaliyowapa msongo wa mawazo(hofu) kama vile kuongea mbele za watu wengi na kufanya mahesabu ya kichwa. Waliokuwa wamefanya tendo la ndoa walionekana wapo vizuri bila wasiwai na hofu zaidi ya wale ambao hawakufanya au walioepuka kufanya tendo la ndoa
Utafiti mwingine uliochapishwa kwenye gazeti la Biologia & fiziologia uligundua kwamba kufanya mapenzi maranyingi huambatana na shinikizo la damu la chini la aina ya diastoliki(namba ya chini au namba ya mwisho unayosoma ukipima shinikizo la damu). Utafiti huu ulifanyika kwa watu wanaoishi na wapenzi wao. Bado utafiti unaonyesha kukumbatiana na mpenzi wako kunahusiana na shinikizo la chini la damu kwa wanawake. Shinikizo la damu la juu huambatana na magonjwa ya mishipa ya moyo, magonjwa ya moyo, figo na kiharusi(stroke)
Kujamiiana kunaongeza chembe hai za kinga mwilini
Kujamiianahumaanisha kuwa vizuri kiafya ya mwili. Kufanya mapenzi maramoja au mbili kwa wiki imehusianishwa na kuongezeka kwa kinga mwilini zinazopambana na maradhi zinazoitwa antibobies ambayo ni immunoglobin A hii antibod huweza kukulinda kupata mafua na maambukizi mengine. Wanasayansi wa chuo kikuu cha Wilkes huko Wilkes-Barre walichukua mate yaliyokuwa na imunoglobin A kutoka kwa watu 112 wanachuo waliolipoti mara ngapi wamefanya tendo la ndoa.
Wale walioonekana kuwa wamefanya mara moja au mbili kwa wiki wameonekana kuwa na kiwango kikubwa cha immunoglobin A na wale ambao hawakufanya kabisa au kwa nadra sana au wamefanya zaidi ya mara tatu kwa wiki wameonekana kuwa na kiwango kidogo cha immunoglobin A
Tendo la Ndoa linahesabika kama mazoezi
Huwa ni kazi ya nguvu na akili na ya kisaikologia kufanya vema tendo la ndoa
Faida ya tendo la ndoa kama mazoezi ni nyingi, tendo la ndoa huimarisha mzunguko wa damu, humtia mtu nguvu na kuwa sawa kiakili.
Tendo la Ndoa hutumia kalori na hivyo huweza kupunguza uzito
Dakika 30 za tendo la ndoa hutumia kalori 85 au zaidi. Inawezekana kutoingia akilini, lakini ukiongeza kwa dakika 42 unatumia kalori 3,570, zaidi ya kupoteza nusu kilo. Kiwango cha nguvu inayotumika katika kufanya Tendo la ndoa ni sawa na mtu anayetembea mile 2 au kilomita 3 na nusu kasoro kwa lisaa limoja
Tendo la Ndoa huimarisha Moyo na mishipa ya damu
Wakati baadhi ya wazee wanaogopa kushiriki tendo la ndoa kwamba watapata kiharusi wakiwa wanashiriki ,sivyo hivyo kwa sababu ya ushahidi wa tafiti mbalimbali zilizofanyika. Utafiti uliofanyika England na kuandikwa katika gazeti la Epidermiology and Community Health unaonyesha kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara hakukuwa na uhusiano wa kuleta kiharusi ambapo watu 914 walichunguzwa kwa muda wa miaka 20.
Na faida za Tendo la ndoa kama mazoezi hazishii hapo, Watafiti pia waliona kuwa kufanya tendo la ndoa mara mbili au zaidi kwa wiki kunapunguza madhara mabaya ya ugonjwa wa moyo kama kushikwa kwa moyo (heart attack) yanayoweza kutokea kwa nusu ya watu hawa ukilinganisha na wale ambao wanafanya tendo la ndoa chini ya mara moja kwa mwezi .
Huleta heshima
Kuleta heshima zilikuwa ni sababu za watu 237 waliosema kwanini wanafanya tendo la ndoa, utafiti huu ulifanywa na chuo kikuu Texas na kuchapishwa kwenye makumbusho ya Sexual Behaviours.
Matokeo ya utafiti huo yanayonakubaliana na utafiti uliofanywa na bi Gina Ogdea mganga wa mapenzi familia na ndoa wa huko Cambridge aligundua kwamba, wale waliopata heshima wameendelea kuimarisha heshima hiyo kwa kufanya tendo la ndoa na wakati mwingine hushiriki tendo la ndoa ili kujihisi vizuri zaidi, alikuwa anazungumza na shirika WebMd.
Tendo la ndoa huimarisha Suhubu(intimancy)
Kushiriki tendo la ndoa na kuingia kileleni huongeza kiwango cha hormoni ya oxytocin, inayoitwa hormone ya mapenzi, inayosaidia kuimarisha mahusiano na uaminifu. Tafiti kutoka chuo kikuu cha Pittsburg na chuo kikuu cha North Carolina kilitafiti watu 59 waliokuwa ndo wameingia kukoma mzunguko wa mwezi wa hedhi. Walichunguzwa kabla na baada ya kupata ujoto wa kukutana na wenzi wao kimwili na kukumbatiana.Utafiti uliona kwamba kukutana ngozi kwa ngozi kulihusiana na kiwango kikubwa cha homoni ya oxytocin. Oxytocin inatufanya tutake kuwa na mtu uliyenaye na kuwa na muunganiko imara. Kiwango kikubwa cha hormone hii imehusianishwa na kuhisi ukarimu/suhubu na kama unahisi suhubu kwa mpenzi wako kuliko kawaida basi kubali ni matokeo ya homoni hii
Tendo la Ndoa hupunguza maumivu
Homoni ya Oxytocin inapoongezeka mwilini, kemikali zinazopooza maumivu ziitwazo endorphins huongezeka pia na maumivu hupungua. Na kama unamaumivu ya kichwa au maungio kama Ugonjwa wa (arthritis) au kusumbuliwa na dalili za mtu anayeingia kukoma kwa hedhi, huonekana kupunguza maumivu hayo baada ya tendo la ndoa na unaweza kushukuru kiwango kikubwa cha homoni hii.
Huongeza Kichochezi mwili cha upendo-Oxytocin
Utafiti uliochapishwa Bulletin of Experimental Biology and Medicine ulichunguza uhusiano wa kichochezi mwili cha upendo-Oxytocin kupunguza maumivu, watu 48 walijitolea. Waliojitolea walivuta hewa yenye homoni hii ya oxytocin na kisha walitobolewa vidole kwa pini. Na wale waliopata hormone hii walihisi maumivu kidogo zaidi ya wale ambao hawakuvuta homoni hii.
Tendo la ndoa hupunguza kuwa katika kihatarishi cha saratani ya tezi dume na kuvimba kwa tezi dume
Kumwaga mbegu mara kwa mara, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, hupunguza kwa wanaume kupata saratani ya tezi dume maishani mwao, mtafiti kutoka Australia alilipoti hilo katika gazeti la Britain Journal of urology International. Walipo wachunguza wanaume waliokuwa na saratani ya tezi dume na wale wasiokuwa nayo waliona hakuna mahusiano ya kuwa na saratani hii na idadi ya wapenzi waliyowahi kuwa nao maishani mwao alipofikia miaka ya 30 40 au 50. Lakini waliona kwamba mwanaume aliyemwaga mbegu mara 4 au 5 kila wiki kipindi alipokuwa na miaka 20 na zaidi walipunguza kihatarishi cha kupata saratani hii kwa 1/3
Utafiti mwingine ulilipotiwa na gazeti la the Journal Medical Association, uligundua kwamba kumwaga mbegu(ejaculation) mara 21 au zaidi kwa mwezi, kunahusiana na kupunguza saratani ya tezi dume kwa uzeeni ukilinganisha na kumwaga mbegu mara 4 au 7 kwa mwezi
Tendo la ndoa humfanya mtu kupata usingizi
Homoni ya Oxytocin inayotolewa wakati wa kufikia kileleni(orgasm) husabisha usingizi, hii ni kutokana na utafiti. Na kupata usingizi wa kutosha umehusianishwa na mambo mengi mazuri.
Kuwa makini endapo unashiriki tendo la ndoa, wasiliana na daktari kwa ushauri, kupata makala zingine ingia au vitabu vya elimu ya afya wasiliana nasi kwa namba zilizo hapo chini
Comments