top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Faida za maziwa ya mama kwa mtoto| ULY CLINIC

Updated: Nov 27, 2020

Faida za kunnyonyesha maziwa ya mama

Katika makala hii utajifunza kuhusu

  • Vilivyomo kwenye maziwa ya mamana maziwa ya fomula

  • Namna ya kuhifadhi maziwa yaliyokamuliwa

  • Namna ya kutumia maziwa yaliyohifadhiwa

  • Umuhimu wa maziwa ya mama



Maziwa ya mama yameonekana kuwa chanzo kizuri cha lishe kwa mtoto, wanasayansi wamekuwa wakiendelea kujifunza kuhusu mchanganyiko huo wa maziwa ya mama ili kuweza kutengeneza maziwa yanayofanana na mchanganyiko huo.

Kemikali za nukliotaidi zilizo kwenye maziwa ya mama na baadhi ya maziwa ya fomula, zimeonekana kufanya kazi kubwa katika kuimarisha mfumo wa kinga za mwili uitwao hyumoro baada ya kupewa chanjo. Mama mwenye maambukizi ya VVU hashauriwi kumnonyesha mtoto

Kunyonyesha inasemekana kuwa ni njia moja kubwa kumlisha mtoto aliyetimiza umri, hii ndio sababu wazalishaji wa maziwa wanaendelea kujifunza kutengeneza maziwa yanayotaka kufanana mchanganyiko wa maziwa ya mama.

Tazama katika jedwali kwa kubonyeza hapa ili kusoma kuhusu vilivyomo kati ya maziwa ya mama na maziwa ya fomula.

Maziwa ya mama huwa na umuhimu katika ukuaji wa ubongo wa mtoto na kukomaza mfumo wa tumbo ili mtoto asipate magonjwa ya kuharisha, hii ni kutokana na mchanganyiko wake wa viini ambavyo havipo kwenye maziwa ya fomula.

Namna ya kuhifadhi maziwa ya mama

Endapo unanyonyesha na unataka kwenda kazini lakini pia unahitaji mwanao anyone maziwa yako, unaweza kuhifadhi maziwa yako na akapewa baadae mwanao wakati wewe haupo. Fuata ushauri ulioandikwa hapa chini mara utakapofikiria kukamua na kuhifadhi maziwa yako

Maziwa ya mama yaliyokamuliwa yanatakiwa kuhifadhiwa kwenye chombo gani?

Kabla ya kukamua maziwa, hakikisha umenawa mikono kwa maji safi na sabuni, kausha mikono yako kwa kitambaa safi kisha anza kukamua ziwa moja baada ya jingine. Unaweza kutumia mashine ya kukamulia maziwa inayopatikana madukani, lakini endapo huna tumia mikono yako safi.

Wakati unakamua, hakikisha unakamulia maziwa katika kikombe kisafi chenye mfuniko, kinaweza kuwa cha plastiki (isiwe plastiki ya chupa za maji ya kunywa au soda au plastiki iliyotengenezwa kwa kemikali ya bisphenol A (BPA)) au cha glasi na iwe na kiwe na uwezo wa kufunikwa. Unaweza kutumia mifuko maalumu ya plastiki iliyotengenezwa huhusani kwa ajili ya kuhifadhia maziwa.

Unatakiwa uyahifadhi wapi baada ya kukamua?


Endelea kusoma makala hii kwa kubonyeza hapa au soma makala zingine kuhusu

ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya


Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa kupiga namba za simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.

47 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentários


bottom of page