top of page

Kujamiiana kipindi cha hedhi | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020

Kujamiiana wakati wa hedhi kunaweza kuwa na faida pamoja na hasara,


Mwanamke akiwa kwenye hedhi anaweza kupata mimba, haswa Kwa wale wenye mzunguko mfupi wa hedhi yaani chini ya siku 21.Hata hivyo lakini, kipindi hiki wanawake wengi huwa hawapo hatarini kupata mimba haswa wale wenye mzunguko wa hedhi siku kuanzia 28 na kuendelea.


Mwanamke anakuwa hatarini kupata mimba takribani siku 12 Hadi 16 kabla ya kuanza kuona damu ambapo kiwanda cha mayai-ovary huzalisha yai jipya.

Ukifanya mapenzi wakati wa hedhi pasipo kutumia kondomu, unahatari ya Kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi vya UKIMWI, Kwa sababu ya kugusana na damu na maambukizi ya fangasi na hepatitis. Ikumbukwe wakati wa hedhi kuna mabadiliko ya homoni kwenye mwili wa mwanamke.


Mwanaume anaweza kupata michomo kwenye kichwa cha uume, ugonjwa unaoitwa balanitis. Matumizi ya kondomu huweza kukukinga na maambukizi haya.


Hata hivyo faida ya tendo la ndoa kipindi cha damu ya hedhi endapo utachukua tahadhari ni pamoja na kupunguza maumivu ya hedhi na kurekebisha Hali ya moyo wakati wa kutokwa na damu ya hedhi.


Hasara nyingine ni kuchafua mashuka na kitanda kama unatoka damu nyingi, na pia endapo unatumia pedi za kuweka ndani ya uke inaweza kuingia kwenye uzazi endapo utasahau kuitoa wakati wa kujamiiaana na utahitaji kuinama na daktari Kwa ajili ya kuitoa.

Faida nyingine ni Kufupisha siku za kutokwa na damu ya hedhi, pia kujamiiana kipindi hiku hupunguza maumivu ya tatizo la kipanda uso yanayotokea Sana wakati wa damu ya hedhi.




Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC

Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.

540 views1 comment

Recent Posts

See All

1 комментарий


jjmsaki
jjmsaki
10 февр. 2020 г.

🙏

Лайк
bottom of page