top of page

Imeandikwa na madaktari wa ULY-CLINIC

 

Saratani ya kaposis

 

 

Saratani ya Kaposi (Kaposi's sarcoma, KS) ilielezewa kwa mara ya kwanza mwaka 1872 na mtaalamu wa ngozi wa Hungarian anayeitwa, Moritz Kaposi.

 

Saratani hii huathiri katika chembe hai za ukuta wa ndani wa mishipa ya damu. Saratani ya kaposis huwa na hatua tofauti kuanzia kwenye ngozi mpaka kuhusisha viungo vya ndani ya mwili.

 

Dalili za awali za saratani ya Kaposis sarcoma ni muonekano wa mabaka mekundu au zambarau juu ya ngozi.  kisha mabaka haya hukua na kutengeneza vimbe kama vinundu.
Inaweza kuleta uharibifu kuanzia kwenye ngozi laini ya midomo na viungo vya ndani ya mwili.

 

Saratani hii imegawanywa katika makundi  4 ambayo ni

  • Inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI

  • Inayohusiana na kushuka kwa kinga ya mwili

  • Classic au sproadic

  • Inayohusiana na Waafrika

 

Saratani ya kaosisi inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI, ukilinganisha na aina zingine huwa na madhara ya haraka na mabaya. Saratani aina hii inayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI hutokea mara nyingi ukilinganisha na zingine

 

Dalili za saratani ya kaposis

 

Saratani ya Kaposisi huathiri ngozi, ngozi laini ya midomo, mitoki, na viungo vya ndani ya mwili pia. Wagonjwa wengi hupata dalili za kwenye ngozi kama kwenye picha hapo pembeni. Saratani ya kaposis  huleta uharibifu wa  viungo vya ndani vya mwili, ambapo inaweza kusababisha aina mbalimbali za dalili, ikitegemea kiungo gani kimeathiliwa.

 

Dalili kama hizi huweza kutokea pia :
 

  •      Kushindwa kupumua-kupumua kwa shida-kama imeathiri mapafu

  •      Fizi kutoka damu

  •      Maumivu ya tumbo

  •      Uvimbe katika miguu

 

  • Madhara kwenye ngozi huweza kutokea hasa katika maeneo ya miguuni, kichwa na shingo.

  • Vinundu ama mapele ya saratani ya kaposis huweza kuwa ya saizi ya kati ama makubwa

  • Karibia vipele vyote huhisiwa kama vikishikwa na huwa haviwashi

  • Mapele na mabaka yanaweza kuwa na sentimeta chache hadi nyingi

  • Mapele ama vinundu huwa na rangi ya brown, zambarau, nyekundu, wakati mwingine ni vigumu kutambua kutokana na rangi ya ngozi ya mtu

  • Vipele hivi hutokea sana kwenye ngozi laini (mdomo, fizi, macho)

 

Saratani hii ikihusisha viungo vya mfumo wa chakula wakati mwingi vipele hivyo huwa havitoi dalili za kuonekana nje ya mwili, kama dalili zikionekana basi ugonjwa unakuwa umekua sana na husababisha dalili zifuatazo;

 

  • Kushindwa kumeza chakula, ama chakula kushindwa kufika tumboni

  • Kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo

  • Kutapika damu, kuonekana kwa damu kwenye haja kubwa ama kupata choo cheusi

  •  Kuziba kwa matumbo ama utumbo

 

Dalili za kwenye mapafu zinaweza pia kutoonekana na kama zikitokea huweza  kuwa zifuatazo;-

 

  • Kukohoa

  • Kupumua kwa shida

  • Kukohoa damu

  • Maumivu ya kifua

 

Matibabu

 

Matibabu ya kukinga madhara ya VVU kwa kutumia dawa za ARV ni moja ya mbinu za kutibu saratani ya kaposis. Dawa za ARV hutumika katika Matibabu  ya saratani ya kaposis isiyohusisha viungo vya ndani vya mwili. Kama mtu ana saratani hii katika viungo vya ndani ya mwili, matumizi ya dawa zinazoitwa chemotherapy huongezewa katika matibabu yake

 

Matibabu yafuatayo yanaweza kutumika kuongeza ubora wa maisha ya mgonjwa mwenye saratani ya kaposis ambayo imeharibu ngozi na kuondoa urembo

 

  • Matibabu ya mionzi

  • Matibabu ya kukata vipele kwa njia ya cryotherapy

  • Kukata vipele kwa kutumia mionzi ya Laser

  • Upasuaji wa kukata vipele

  • Matumiz ya dawa za saratani za vinka alkaloid

  • Matumizi ya dawa za kupaka aina ya retinoids

Imechapishwa 3/3/2015

imepitiwa upya 3/3/2016

Imeboreshwa 5/11/2018

bottom of page