top of page

Saratani ya koo

​

Imeandikwa na madaktari wa ulyclinic

​

Utangulizi

​

Saratani ni vimbe inayotokea kwenye sehemu yoyote ile ya mwili, vimbe hizi husababishwa na chembe hai za mwili kukua kwa haraka pasipo kudhibitiwa na mwili.

​

Saratani ya koo ni saratani inayotokea kwenye chembe hai za koo. Kwa kawaida koo huanzia usawa wa nyuma ya pua na kuelekea chini shingoni. Maeneo hayo yote yanaweza kupata saratani na kuesemekana kuwa ni saratani ya koo.

Saratani ya koo inaweza kuhusisha kiboksi kinachotengeneza sauti, kidaka tonge, njia ya hewa n.k

 

Dalili za saratani ya koo ni zipi?

  • Kukohoa

  • Kubadilika kwa sauti, kukwama kwa sauti au kutosikika vizuri

  • Kushindwa kumeza chakula

  • Maumivu ya masikio

  • Uvuimbe au vidond visivyopona kwenye koo

  • Koo kuwa kavuu

  • Kupoteza uzito/kukonda

 

Visababishi

Saratani ya koo na kioksi cha sauti hutokea endapo kuna shida ya kijeni kwenye chembe hai za koo, hivyo husababisha chembe hizo kukua pasipo kudhibitiwa na hivyo kuleta uvimbe.

 

Kuna aina tofauti za saratani ya koo, aina hizi hutegemea sehemu saratani ilipo katika koo

​

Vihatarishi

  • Vihatarishi vya saratani ya koo huhusisha

  • Uvutaji wa sigara, kula tumbaku

  • Ugonjwa wa kiungulia

  • Matumizi ya pombe yalikokithiri

  • Maambukizi ya virusi vya HPV ambavyo huambukizwa kwa kufanya mapenzi kwa njia yam domo(kulamba uke au uume)

  • Chakula kinachokosa matunda na mboga za majani kwa wingi

​

Kujikinga

Acha kuvuta sigara na usianze kuvuta sigara kama huvuti

Unaweza kupata msaada wa daktari akufundishe namna ya kuacha kuvuta sigara

​

Jikinge na virusi vya HPV

Acha kufanya mapenzi kwa njia ya kunyonya uke au uume na kuwa na wapenzi wengi, hakikisha mmepima Virusi hivi na hamna mnapokuwa mnafanya mapenzi kwani kirusi huyu huweza kusababisha saratani zingine ikiwa pamoja na saratani ya shingo ya kizazi. Ukipima na mpenzi wako ni vema ili kujikinga na saratani hizi, epuka wapenzi wengi au kufanya mapenzi na wanawake au wanaume wanaojiuza.

​

Kwa baadhi ya nchi kinga dhidi ya kirusi huyu hutolewa hospitalini, ongea na daktari wako ili akuelekeze  kama chanjo inapatikana kwenye hospitali yake. Kinga dhidi ya kirusi huyu humlinda mtu asipate madhara ya kirusi huyu na pia husaidia kupambana na kirusi huyu na kumwondoa mwilini.

​

Kunywa pombe kwa kiasi

Kuna tafiti zimefanywa zikionyesha kunywa pombe haina faida kimwili ya kukukinga na saratani, lakini tafiti zingine zinaonyesha unywaji wa pombe huhusiana na baadhi ya saratani kama saratani ini, koo n.k

​

Mtu anashauriwa kunywa uniti kati ya 14 na 21 kwa wiki, kwa mwanamke anaweza kunywa unit 14 za pombe kwa wikina mwanaume unit 21 za pombe kwa wiki. Muulize daktari wako akuambie unit hizi inamaanisha pombe za aina gani na ngapi au wasiliana na namba za simu chini ya tovuti hii

​

Kula chakula chenye afya njema

Chakula chako kihusishe mboga za majani kwa wingi na matunda, vyakula hivi vinasemekana kumkinga mtu ana saratani. Chagua matunda na vyakula vinavyosemekana kukinga mtu dhidi ya saratani

​

Vipimo na Utambuzi

Utambuzi wa saratani hii hutegemea dalili na uchunguzi wa koo. Daktari ataweka kifaa maalumu cha kamera kinachomwezesha kuona sehemu ya ndani ya koo lako, kisha atachukua baadhi ya chembe hai kwenye koo lako na kufanyia kipimo maalumu cha biopsy

​

Daktari anaweza kuagiza kipimo cha picha ya mionzi ya shingo ili kuangalia endapo saratani imesambaa sehemu zingine za mwili.

 

Matibabu

Matibabu ya saratani ya koo huhusisha matibabu mbalimbali kama zilivyo tiba za saratani mbalimbali,

Kuna tiba mionzi ya kuunguza saratani, upasuaji kwenye hatua za awali ili kuondoa tishu zenye saratani, au kuondoa sehemu ya koo na tiba dawa za kuua chembe za saratani.

​

Toleo la 2

Imepitiwa 15/2/2019

bottom of page